Siasa za aina hii si msaada kwa nchi yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa za aina hii si msaada kwa nchi yetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anfaal, May 25, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa Watanzania wengi sasa hivi wimbo ni siasa. Hakuna jambo jingine linalojadiliwa zaidi ya siasa kila uchao. Lakini siasa hizi licha ya kuaminika kuwa ndio suluhu ya baadhi ya matatizo katika baadhi ya nchi, siasa za nchi kwetu ni tofauti saana. Katika mazungumzo ya Watanzania kwao siasa ni kuzungumzia ufisadi, ukabila na udini na hasa vyama vikuu vinavyopingana huu ndio umekuwa wimbo wa kila siku. Lakini maelezo ya namna hii yanaanza kuwazoea Watanzania maana ni kila siku mjadala umekuwa huo.
  Tukijiuliza maelezo/mikutano/mihadhara inayohusu hayo mpaka sasa hivi imelisaidia nini Taifa? Wengi majibu yao yatakuwa kuongezeka kwa wabunge wa upinzani. Lakini, je ni nini mahitaji ya Watanzania wa sasa hivi? Watanzania wanahitaji maendelea na si kelele tena. Vyama hivi kama vingeweza kujikita na kuwaletea maendeleo Watanzania kwa rasilimali hizo chache zilizokuwa nazo, Watanzania wangewaelewa kwa urahisi kuliko hata rasilimali zinazopotezwa kwa matusi ya majukwaani.
  Ni vyema tuyataje matatizo ya Watanzania japo kwa uchache na tuone kama njia zinazotumika zimeweza kuyasaidia. Watanzania wanalalamika mfumuko wa bei wa kutisha usioendana na vipato vya wengi hii ni katika mafuta, vyakula na hata sasa hivi ardhi inayouzwa na serikali. Lakini pia mfumo wetu wa elimu ni kama nguo chakavu, wangependa nguo mpya inayoendana na wakati wa sasa, Msemo wa kilimo kwanza usio na tija-wenye kukurupuka bila hata kufanya utafiti wa mahitaji ya wakulima na soko la bidhaa, viwango vya mishahara visivyokidhi hali ya sasa, kufanya kazi kwa mazoea na matumizi mabaya ya rasilimali zetu.
  Hili la matumizi mabaya ndio ufisadi, linapigiwa kelele kila siku. Kuna haja ya kubadili mbinu sasa kuona mafisadi wanawajibika. Lakini pia wanasiasa watambue wanawajibu wa kuwahimiza watu kufanya kazi kama wanavyowahimiza kuwapigia kura.
  Mwisho, siasa za sasa hivi zinatakiwa zibadilike, zije na suluhu mbadala wa matatizo yetu. Wananchi wameshashtakiwa saaana, kwa kifupi wameamka. Kuna matatizo ya umeme, waseme njia mbadala, elimu nk. Tuone Taifa letu linahitaji kwenda mbele kabla ya vyama vya siasa.
  Hivi kila mtu ajiulize; Baada ya kufuata mfumo wa vyama vingi, Tanzania imekuwa na afadhali au ndio imeharibika zaidi?
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Huwezi kulaumu upinzani kwani hawana rasilimali za kutosha kufanya vitu na hata rasilimali zilizopo si za CCM bali ni za serikali.
  Mimi kwa mawazo yangu nakubaliana na wewe kwamba kuna mambo mengi ambayo upinzania ingeweza kuongeza kwenye agenda za taifa.
  Mfano elimu Elimu: Mimi ningependa kuona upinzani uhimize sera za elimu (a) Kama shule zinafelisha hasa za binafsi wapewe muda na kama hakutakuwa na mabadiliko zifunge. Hatuwezi kuendelea na shule ambazo kila mwaka zinatoa division 4 na 0 huu ni uizi wa pesa na upotevu wa muda wa watototo wetu wa Kitanzania. (b) Kwasababu vijana wengi wanamaliza vyuo na hawalipi madeni ya chuo bado tuweke sera ya vijana wote wanaomaliza vyuo na wamechukua mikopo ya serikali wanatakiwa kufundisha kwa miezi sita. Kama shule ni ya serikali itagharamia chakula na malazi na kama ni ya binafsi itatoa posho kusaidia hawa vijana. Kwa shule za private ambazo zinafanya vizuri ni uamuzi wao lakini kwa shule za private ambazo hazifanyi vizuri ni lazima wachukue hawa wana vyuo mpaka hapo itakapo onyesha maendeleo ya kutosha.
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Umeorodhesha matatizo hapo juu lakini wakulaumiwa sio wapiga siasa. Wakulaumiwa ni watawala wanaotekeleza sera zao na ilani zao za kuwaletea maendeleo Watanzania. Hebu jiulize miaka hamsini ya utawala wa CCM imeleta ahueni au tabu kwa maisha ya Watanzania. Kama jibu ni ndiyo je ahueni hiyo ina value ya miaka 50 ya utekelezaji wa ilani na sera hizo? Kama hapana kwa nini wanang'ang'ania kutawal hata miaka hamsini ya sera zao zilizoshindwa kumkwamua mwananchi toka lindi la umasikini?
   
 4. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lazima tukubaliane kwamba mwanasiasa anaandaa hoja zenye kipao mbele kwake.
  Ndiyo maana ya wao kutofautiana.
  Kwa mfano:-
  1. CHADEMA kipao mbele chao ni Kupambana na ufisadi pamoja na kuongeza makusanya ya kodi.
  2. CCM ni kupanua miundombinu na kusisitiza kwa wafadhili kwamba bado Tanzania inahitaji misaada [ndiyo sababu watendaji wakuu wa nchi wanasafiri sana nje ya nchi na lugha yao ni moja MISAADA]
  3. Kipao mbele chao ni kuimarisha serikali ya mapinduzi zanzibar pamoja na ujenzi wa haki sawa
  4. n.k
  Huo ni mfano wa vipao mbele kwa mujibu wa majukwaa ya wanasiasa wa vyama husika.
  Pia siasa ni kuibua mapungufu ya mpinzani wako ili kumuondolea uaminifu kwa wapiga kura. Mfano:-
  a. Ndiyo sababu Republican waliibua hoja ya Monica dhidi ya Clinton
  b. Ndiyo sababu Republican waliibua utata wa uraia wa Obama
  Kwa mtazamo wako hayo a&b yana tija gani kwenye utendaji wa kiongozi husika?
   
 5. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Miea nadhani kuna kitu kwenye mfumo wetu hakipo sawa ambacho ni zaidi ya siasa. Ukiachana na miaka 50 ya uhuru, hivi tujiuliuze miaka 20 baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, hali za Watanzania walio wengi zimebadilika? Kuna haja ya kuendelea kupoteza mabilioni kwenye siasa badala ya kuangalia Watanzania watasongaje mbele. Hivi pesa kiasi gani zinaingia kwenye siasa? Kwanini sasa tusianze kuzungumza maendeleo? Haya mambo hayatenganishiki?
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe mkuuu.


  Kuna tatizo kubwa ndio maana hakuna mbunge awe wa chama cha magamga au wa vyama inzani hawahoji.

  • Kwa nini mbunge apate mshahara mkubwa kuliko afisa kilimo wa mkoa RPC wa mkoa . Afisa madini, Mhandisi wa Mkoa, Afisa Elimu wa Mkoa. Mganga mkuu wa Mkoa .
  Kamaw hata wabunge na hata wa upinzani hawaoni tatizo wala kuhoji hilo kuna tatizo.

  Simply bcs wanasiasa wengi na watu wengi tumejisahau kudhani siasa ndo zitatatua matatizo yetu. No wonder hata maprof na mdr wote wanaimbilia kwenye siasa.

  Siasa inatakiwa kuleta Uamsho tu but mtu kama Mbunge hawezi kutatua matatizo ya jimbo. Matatizo ya jimbo ni kazi za Afisa alimu. Afya, Mhandisi, Afisa Biashara.... etc.
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Watawala ni wanasiasa. Hivi tujiulize, tutazungumzia chaguzi for the next 5 years? Kasi hii inayotumika sasa hivi kwenye siasa ingetumika kuhamasiha maendeleo miaka mitatu, tungekuwa wapi? Hivi wananchi wanapowachagua wabunge, wanataka kuona jimbo lao limeshikwa na mbunge fulani au wanataka maendeleo? Naona tunajisahau, kila mtu anageuka mwanasiasa kuanzia watoto wa shule. Bora zingekuwa siasa za changamoto ya maendeleo. Sasa hv ni siasa za kabila, dini na matusi. Hatuwezi kusonga mbele kwa kujadili uchaguzi ujao baada ya uchaguzi wa sasa.
   
Loading...