Siasa ya Tanzania ina unafiki mkubwa

Siasa ya Tanzania ina unafiki mkubwa

Kofia Baya

Member
Joined
Sep 28, 2017
Posts
9
Reaction score
38
Habari za wakati huu

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, kusema ukweli sijaona nia ya dhati ya wanasiasa wetu katika kulikomboa taifa letu (chama tawala vs upinzani) zaidi ya ushabiki wa simba na yanga.

Kitu ambacho nimejifunza katika vyama vyetu hivi ni kwamba kila kitu kinachofanyika aidha na chama tawala au cha upinzani kinakuwa kina malengo fulani ya kisiasa na sio kulikomboa taifa letu bali inakuwa ni kama kiki.

Na mwisho wa siku sisi walaji wa hizo siasa au mashabiki huwa tunaegemea maamuzi yetu kutokana na mlengo wa vyama tunavyovipenda na sio ukweli wa mambo.

Kwa mfano tukio la Nyalandu kutaka kuhamia upinzani akitokea CCM au kipindi kile cha Lowasa alipohamia upinzani unaweza kuona ni namna gani chama alichotoka kikijitahidi kumchafua wakati chama kinachompokea kikijitahidi kumpamba kana kwamba mwanzo chenyewe hakujawahi mkashifu/mtuhumu.

Hapa picha ninayoipata hapa kwamba mtu anakuwa mbaya tu akiwa sio upande wako na mzuri akiwa upande wako bila kujali maslahi ya taifa bali maslahi ya vyama.

Kwa hiyo siku Ndugai atakapohamia chadema atakavyopambwa na rangi za kila aina na wanachadema huku akipakwa tope la kila aina na ccm na matokeo yake ni kwamba mtu anahama chama A kwenda B si kwa sababu ya uzalendo bali maslahi yake binafsi.

Je haya sio maigizo ambayo kwa namna moja ama nyingine yanasababisha maendeleo yetu kusuasua kwa nini tusiwe na mfumo wa kama wa China kuliko kutufanya watanzania wajinga
 
Back
Top Bottom