Siasa Vs. Taaluma: Anguko la elimu nchini

Siasa Vs. Taaluma: Anguko la elimu nchini

Kwanza sio wengi kama udhaniavyo, pili pipe line yetu ina vipande hakuna kitu cha kuflow ndio maana serikali inahangaika na retirement age ya wahadhiri. Walianza 55, wakaenda 60 na leo ni 65. Juilize kwa nini kama ingekuwa rahisi kuwa replace wahadhiri.
Hoja ya kuongeza miaka ya kustaafu kwa wahadhiri sio kwamba ni wachache bali ni kwamba kwa kawaida wengi wao wanapokua wametunukiwa hiyo ngazi wanakua tayari umri umeshasogea hivyo kustaafu wakiwa na 60 inakua kama wamekatishwa kwa makusudi kulihudumia Taifa kwa ngazi waliyoihangaikia kwa muda mrefu

Mara nyingi kutokana na Hicho kigezo cha umri wa kustaafu wahadhiri wengi wamekuwa wakifanya kazi yao wakiwa maprofesa kwa miaka michache sana na serikali imekua ikiwaajiri kwa mikataba baada ya kustaafu sababu bado wanahitajika, kutokana na hiyo hali ndio serikali imeamua kuongeza umri wa kustaafu kwa maprofesa kuliko kufanya kazi kwa mikataba kutokana na sheria kubana umri.

Hilo jambo lipo katika mataifa mengine sio Tanzania ya kwanza kufanya hivi
 
Jambo gumu kabisa kwa wengi wetu kulielewa ni kuwa serikali ya Tanzania imekuwa serikali tegemezi kabisa kwenye kusomesha watalaamu wake baada ya kiwango cha degree ya kwanza. Tumekuwa tunategemea wahusani na sasa tumefikia hatua bila miradi ya nje au scholarship hatuna uwezo kabisa kusomesha masters na phd. Hata vyuo vina wakati mgumu kupanga programu za kuongeza utalaamu wa walimu wake. Tuna waliobobea kwenye fani A lakini sasa wanafundisha fani B kwani hicho (A) ndiyo walichosoma ingawa walitakiwa wakachukue fani B. Kuna idara zimepoteza maprofesa wa kutosha na hii ina athiri ufundishaji.
Dawa ni moja serikali itenge fedha za kutosha za kusomesha wahadhiri nje na ndani ya nchi. Kumbuka pia wengi hutumika kufanya kazi za ushauri na zikizidi zina athiri ufundishaji wao. Kwa hiyo idara inaweza kuonekana iko sawa maprofessa wengi lakini kuwakuta darasani inakuwa kazi.

Wee jamaa una vision kubwa sana.
Halafu kuna mtu anakuja anauliza who cares? Seriously!!!
Hawajui jinsi ilivyo ghali, na ngumu kutengeneza hawa wataalamu. Mwisho wa siku wamelazimika mpaka kuongeza miaka ya wao kustaafu ili waendelee kutumika
 
Kimsingi, hatukatai mtuyeyote kuwatumia hawa wataalamu, lakini fikiria
Katika uhaba mkubwa wa madaktari, Mh Kigwangalaa na Mh Kebwe (hawa ni mfano tu) wako kwenye nafasi za kisiasa.
Unachukua ma prof na Dr wabobeza wote unapeleka kwenye chama, political positions n.k. Nani atawapika wataalamu wengine?
 
Ni bora nipate mwanasiasa muuza duka anayeweza kueleza shida ya kodi, ugumu wa mikopo ya kibiashara, hatari za mafuriko, gharama za afya n.k badala ya kuwa na Professors wanaosoma speech na kutokubadilisha chochote. Ni lazima tuelewe usomi hasa wa PHD hauna uhusiano wowote na wanachofanya PHD unapata kwa kufanya reseach na reseach yako inaweza isiwe hata kuhusu TZ au Mambo ya maendeleo. Mfano Mafufuli PHD ya Chemistry haina uhusiano wowote wa siasa inawezekana alichunguza dawa... wadudu..hivyo siasa na usomi ni vitu tofauti
 
Hoja ya kuongeza miaka ya kustaafu kwa wahadhiri sio kwamba ni wachache bali ni kwamba kwa kawaida wengi wao wanapokua wametunukiwa hiyo ngazi wanakua tayari umri umeshasogea hivyo kustaafu wakiwa na 60 inakua kama wamekatishwa kwa makusudi kulihudumia Taifa kwa ngazi waliyoihangaikia kwa muda mrefu

Mara nyingi kutokana na Hicho kigezo cha umri wa kustaafu wahadhiri wengi wamekuwa wakifanya kazi yao wakiwa maprofesa kwa miaka michache sana na serikali imekua ikiwaajiri kwa mikataba baada ya kustaafu sababu bado wanahitajika, kutokana na hiyo hali ndio serikali imeamua kuongeza umri wa kustaafu kwa maprofesa kuliko kufanya kazi kwa mikataba kutokana na sheria kubana umri.

Hilo jambo lipo katika mataifa mengine sio Tanzania ya kwanza kufanya hivi
Wanahitajika kwa sababu ni vigumu kuwareplace. Kama huna wa kuchukua nafasi hizo bado utakuwa na uhitaji. Hizo nyingine ni story za mitaani waliopo jikoni wanajua. Gharama ya mkataba ni kubwa kuliko ile ya aliyeko kazini kwa kuhamia 65 serikali inategemea itapunguza gharama. Swali ni je hatua hii itatosha au ni yale yale? Bila kupanga na kulipia gharama za human capital development ya vyuo hatutafika mbali.
 
Ni bora nipate mwanasiasa muuza duka anayeweza kueleza shida ya kodi, ugumu wa mikopo ya kibiashara, hatari za mafuriko, gharama za afya n.k badala ya kuwa na Professors wanaosoma speech na kutokubadilisha chochote. Ni lazima tuelewe usomi hasa wa PHD hauna uhusiano wowote na wanachofanya PHD unapata kwa kufanya reseach na reseach yako inaweza isiwe hata kuhusu TZ au Mambo ya maendeleo. Mfano Mafufuli PHD ya Chemistry haina uhusiano wowote wa siasa inawezekana alichunguza dawa... wadudu..hivyo siasa na usomi ni vitu tofauti

Sasa haya ndio matumizi mabaya ya degree kama PhD. PhD ni research degree inatumika zaidi kwa wale watakaofanya research au kufundisha vyuo vikuu. Duniani kote hilo ndiyo dhumuni la kufanya PhD kama ninavyo ifahamu. Sasa kama sisi PhD zetu hazina uhusiano na kazi tunazofanya basi tumepotoka. Sisemi kila mwenye PhD lazima afanye hivyo lakini statistically wengi wao wanatakiwa wawe hivyo vinginevyo ni utumiaji mbaya wa rasilimali watu hasa ukijua kuwa vituo vya utafiti na vyuo vikuu vina upungufu wa watu wenye elimu hiyo.
 
Haya soma mawazo ya huyu kutoka QUORA
Is doing a PhD worth it these days?

Daniel Dvorkin
, Ph.D. Bioinformatics & Biostatistics, University of Colorado School of Medicine (2013)
Answered Apr 7

The answer depends purely on what you hope to get out of it.

Do you want to be a researcher? Then absolutely, it’s worth it. You can do research without a PhD, of course. Plenty of people do, and some of them are quite successful. But the research skills you will learn in the course of writing your dissertation are hard to replicate outside that environment, and your defense will test those skills in a way that almost nothing else can. Writing papers is easy by comparison to standing up in front of a group of people, all of them skilled and deeply knowledgeable in your field, who will tear you to shreds if you can’t prove you know your stuff.

Do you want to be a professor? That might seem like the same question as above, but not all professors are researchers and most definitely not all researchers are professors. Not all professors have doctorates, either, but that’s the way to bet. If a faculty appointment is your goal, a PhD is the most likely way to get there—but be aware that it’s no guarantee. The number of available junior faculty positions is much smaller than the number of new PhD graduates every year. So the answer here is a cautious yes, but have a fallback plan.

Do you want it for a job outside academia? Then probably not, because (with a few exceptions in computers and pharmaceuticals) most companies really aren’t looking for PhDs. They might hire you, but there’s probably nothing you bring to the table, from their point of view, that someone with a Master’s degree doesn’t. And it might actually hurt your chances of getting hired if they think you’re “overqualified.”

Do you want it for the prestige? Then hell no. Doctoral studies will eat years of your life, and leave your brain feeling like a wrung-out sponge. You could do almost anything else with that amount of time and effort that will get you more in the way of money, ego, and bragging rights.

I’m glad I got my PhD, because that was the only way to get where I wanted to be. If that’s the case for you, then go for it. It’s a very personal decision, and only you can make it for yourself. Just be as sure as you can be before you start that the destination is worth the journey. (Source
https://www.quora.com/)
 
Halafu kuna juha mmoja anaenda vyuoni na kukataza siasa, huyu ni very shithole.Elimu hoi kabisa kisa wooote wanaojifanya wachambuzi wa siasa tena Kwa kujinasibu kuwa hawana vyama kuingia ktk siasa.
 
I care, thats why nimeiweka hapa.
Elimu inazidi kudidimia, watoto wetu watasoma katika vyuo hivihivi ambavyo havina wabobezi
mkuu we need critical thinkers like u.
Mimi ngoja nikasome Kenya coz huku ni siasa tu na sina interest nayo.. ..
 
Nimekaa na kufikiria kwa KIPINDI sasa,mwisho Nimegundua ukweli kuwa tatizo la wasomi Tanzania BADO lipo.
Kwa akili yangu, mtaalamu ni mtu huru asiye na ushabiki Wala upande kwa nafasi YAKE ya utaalam.
Mfano, daktari bila kujali Hali ya mgonjwa anastahili kuokoa MAISHA YAKE kwa kumtibia kwa UJUZI wake.
Leo nimeona wataalamu wanakuwa na upande ,wanatumia utaalam WAO kwa ushabiki na wanasahau kuwa WAO NI tunda la Taifa ZIMA.
Mfano hii Unaweza KUNIONA ktk maeneo mbalimbali ,Leo uzalishaji wa wataalamu ktk vyuo vyetu vikuu Unaelekea kusimama baada ya wataalamu hao kuondoka na kuenda kutumikia maeneo YAO wanayoshabikia na kuacha Jamii KUBWA inayowategemea wasijue cha KUFANYA.
Wataalamu waliobaki nao Naamini wanaelekea kuacha Fani ZAO za Kuitumikia Jamii na kuenda Kuendeleza ushabiki WAO.
WAPO wataalamu waliokuwa na mvuto MKUBWA HAPA nchini na walikuwa wakisimamia mambo ya watu WENGI kimtizamo, na walisifika kwa misimamo, Leo wamewaacha watu na kubadili misimamo na mitazamo YAO ili kuenda kuendeleza ushabiki.
Taifa litajengwa na watu (wasomi,wafanya kazi, na wakulima),Kama hawa WOTE wataacha jukumu HILI na kuenda kushabikia ni dhahiri kuwa Taifa litasimama!
Hakika Taifa linasinyaa
 
WINO WA DHAHABU..... NILIWAHI KUANDIKA.

SIASA INAVYOVUNA WATAALAMU.

Na Thadei Ole Mushi.

Pale alipo Dr. Mwakyembe, Dr. Tulia,Pro Kabudi, Pro Mbarawa na huko anakokimbilia Prof Kitila Mkumbo na sasa Dr Bashiru Ally ndiko kwenye pesa ya maana.

Kwa Taarifa yako Katika ukanda wa Afrika mashariki Tanzania ndio nchi pekee yenye maprofesa na watu wenye Phd wachache kuliko nchi giants za A. Mashariki na kusini mwa jangwa la sahara. Pamoja na uchache wao Siasa inazidi kuwavuna kila siku... huko ndiko kuliko na Maslah mapana.

Kwa statistics za mwaka 2016 Vyuo vikuu binafsi nchini vilikuwa 35 ila vilikuwa na maprofesa 74 tu hawa ni wale maprofesa kamili. Associate walikuwepo 56 hawa ukijumlisha na hao 74 unapata 130. Associate maana yake ni accademic rank iliyopo kati ya assistant professor na Full professor (operational meaning)

Ambao wana Phd kwenye vyuo vya binafsi ambao wanafundisha ni 138. Ukijumlisha na idadi ya maprofesa unapata 268. Hawa ndio wanaohudumia karibu zaidi ya nusu ya wadahiliwa wote Tanzania wanaosoma vyuo vya binafsi.

Kwa upande wa serikali Full Prof walikuwepo 204 huku associate wakiwa 309 na Phd wakiwa 514 wote hawa wanatengeneza staff ya watu 1,027. Hawa ndio wataalamu wabobezi wanaohudumia vyuo vyote vya Seriali nchini hadi kufikia 2016.

Hadi kufikia 2016 kuliwa kuna vyuo vikuu zaidi ya vinne havina Prof hata mmoja huku kimoja cha serikali kikiwa na Prof mmoja.Nafikiri hivi ni vile vilivyonyimwa udahili wa wanafunzi.

Chuo kilichokuwa kinaongoza kwa kuwa na maprof wengi ni chuo cha SUA kikiwa na maprof 75 huku UDSM ikiwa na maprof 67 hadi kufikia 2016. Kwenge vyuo vya binafsi kuna balaaa kubwa....

Kenya wao miaka 3 iliyopita walikuwa na maprofesa kwenye vyuo vyao vya Serikali 5,189, jumlisha hawa wakwetu kama hata wanafika nusu.

Kenya Kwa mwaka wanazalisha Phd 1,000 huku Tanzania tukizalisha chini ya 500 kwa mwaka.

Tanzania Imefikia mahali umri wa kustaafu wa maprofesa chuoni umeongezwa hadi karibu kufikia miaka 80. Hiki ni kiashiria cha Tatizo kubwa lililopo.

Vyuo vyetu vya binafsi vimeanza kuajiri maprofesa toka nchi jirani kama Kenya huku tukipigana kusema ajira hakuna....

Ni wakati sasa wa Serikali kufikiri namna bora ya kuboresha maslahi ya hawa wataalamu wanaokimbilia kwenye siasa ili wabaki kuzalisha wataalamu wengine.

Wanavyuo wengi wanaomaliza vyuo vikuu kwa sasa hata kuandika barua ya kuomba kazi hawawezi inawezekana ni ukisefu wa wataalamu bora mavyuoni.... .... mimi Sijui.

Ukiangalia bidhaa zinazotengenezwa hapa kwetu ni za kuhesabu ila kila mwaka vyuo vyetu vikuu na vyuo vya kati vinamwaga maelfu ya wahandisi mtaani..... jamani hata Toroli mmeshindwa kulitengeneza....

Hata wataalamu waliobakia wameshaanza kuwa na element za siasa inawezekana nao wapo njiani kutoka. Siku hizi wanajitokeza hadharani kabisa na kusifia chama fulani bila woga... wanakaa karibu na wanasiasa ili kuambulia chochote.......

Haya tunayazungumza huku kada ya Siasa ikiwa inadharau kazi nyingi za wataalamu. Jiulize ni Tafiti ngapi zipo kwenye maktaba zetu za vyuo vikuu na jiulize zinatumika wapi. Katika hali hiyo unafikiri kuna haja ya hawa wataalamu kuumiza kichwa huku kazi zao zikiwa hazitambuliki au wavae Suti wakapige mabenchi makofi pale Dodoma huku wakiingiza mamilioni.??

Ni aibu kwa profesa aliyebaki pale Muhimbili kuzidiwa mshahara na kibajaji na kina mlinga hahahahaha, Natania tu ila unaweza kuona ni kwa namna gani hawa wataalamu wetu wanavyojiongeza. Unamwona Dr. Bana anavyojitutumua? Nani anataka kustaafu na kiinua Mgongo cha ajabu ajabu?

Angalia Umri wanaoondoka nao hawa kina Kitila mkumbo, Dr Tulia na Sasa Bashiru Ally. Ni Umri uliokuwa unahitajika haswa katika kuzalisha wataalamu. Ila tujiulize nini kingeweza kuwashawishi kubaki pale mlimani zaidi ya kukimbilia kwenye Siasa? Jambo pekee ni Maslahi. Kwa maana hiyo tusiwalaumu hata kidogo wamewaza njee ya Box

Kila La kheri Dr Bashiru

Ole Mushi.
0712702602.
HIyo inaitwa political transaction Mkuu.
Unawaondoa kule ili kupunguza wapinzani. NA kizuri zaidi hujulikana kuwa wasomi wengi wako Hoi kiuchumi. So, ni cheap products kisiasa.
Kijana hawezi piga kelele mbele ya baba. So, mawazo yao, ndio mawazo ya Nchi. Unfortunately, wengi walishafeli kimawazo. Na ndio maana wakishanunuliwa, basi huyakana maneno yao waliyoyazungumza na kuyatamka siku za nyuma.
Na kutokana na hilo, hili litakuwa ni taifa la wagonjwa amba hawawezi kunyanyua midomo yao mbele ya Ma dr na ma Prof. Wachache sana wenye guts ya kupingana nao kimawazo.

Tunatitia.
 
Nchi hii wataalamu hawapewi kipaumbele kabisa ndiyo maana walimu wengi wanatiisha huruma. Kwenye siasa nirahisi kufanya wizi mkubwa na wapumbavu wakakutetea kwanguvu zote japo wengine hawajapata chochote.
Hizi hoja za kuwashtaki no vimbwanga vya kujionesha kuwa wako serious lkn najua huu upepo utapita tuu kama pepo nyingine
 
Haya soma mawazo ya huyu kutoka QUORA
Is doing a PhD worth it these days?

Daniel Dvorkin
, Ph.D. Bioinformatics & Biostatistics, University of Colorado School of Medicine (2013)
Answered Apr 7

The answer depends purely on what you hope to get out of it.

Do you want to be a researcher? Then absolutely, it’s worth it. You can do research without a PhD, of course. Plenty of people do, and some of them are quite successful. But the research skills you will learn in the course of writing your dissertation are hard to replicate outside that environment, and your defense will test those skills in a way that almost nothing else can. Writing papers is easy by comparison to standing up in front of a group of people, all of them skilled and deeply knowledgeable in your field, who will tear you to shreds if you can’t prove you know your stuff.

Do you want to be a professor? That might seem like the same question as above, but not all professors are researchers and most definitely not all researchers are professors. Not all professors have doctorates, either, but that’s the way to bet. If a faculty appointment is your goal, a PhD is the most likely way to get there—but be aware that it’s no guarantee. The number of available junior faculty positions is much smaller than the number of new PhD graduates every year. So the answer here is a cautious yes, but have a fallback plan.

Do you want it for a job outside academia? Then probably not, because (with a few exceptions in computers and pharmaceuticals) most companies really aren’t looking for PhDs. They might hire you, but there’s probably nothing you bring to the table, from their point of view, that someone with a Master’s degree doesn’t. And it might actually hurt your chances of getting hired if they think you’re “overqualified.”

Do you want it for the prestige? Then hell no. Doctoral studies will eat years of your life, and leave your brain feeling like a wrung-out sponge. You could do almost anything else with that amount of time and effort that will get you more in the way of money, ego, and bragging rights.

I’m glad I got my PhD, because that was the only way to get where I wanted to be. If that’s the case for you, then go for it. It’s a very personal decision, and only you can make it for yourself. Just be as sure as you can be before you start that the destination is worth the journey. (Source
https://www.quora.com/)
Daah
Natamani wahadhirina wanasiasa wangeweza kuisoma hii.
Ama kwahakika, PhD haina maana yoyote katika utendaji wa kawaida.
Pia ni upotezaji wamuda na rasilimali kufanya phd kama hautaki au hauna nia ya kuwa academia
 
Back
Top Bottom