Siasa Vs. Taaluma: Anguko la elimu nchini

bhikola

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,133
Reaction score
1,668
WINO WA DHAHABU..... NILIWAHI KUANDIKA.

SIASA INAVYOVUNA WATAALAMU.

Na Thadei Ole Mushi.

Pale alipo Dr. Mwakyembe, Dr. Tulia,Pro Kabudi, Pro Mbarawa na huko anakokimbilia Prof Kitila Mkumbo na sasa Dr Bashiru Ally ndiko kwenye pesa ya maana.

Kwa Taarifa yako Katika ukanda wa Afrika mashariki Tanzania ndio nchi pekee yenye maprofesa na watu wenye Phd wachache kuliko nchi giants za A. Mashariki na kusini mwa jangwa la sahara. Pamoja na uchache wao Siasa inazidi kuwavuna kila siku... huko ndiko kuliko na Maslah mapana.

Kwa statistics za mwaka 2016 Vyuo vikuu binafsi nchini vilikuwa 35 ila vilikuwa na maprofesa 74 tu hawa ni wale maprofesa kamili. Associate walikuwepo 56 hawa ukijumlisha na hao 74 unapata 130. Associate maana yake ni accademic rank iliyopo kati ya assistant professor na Full professor (operational meaning)

Ambao wana Phd kwenye vyuo vya binafsi ambao wanafundisha ni 138. Ukijumlisha na idadi ya maprofesa unapata 268. Hawa ndio wanaohudumia karibu zaidi ya nusu ya wadahiliwa wote Tanzania wanaosoma vyuo vya binafsi.

Kwa upande wa serikali Full Prof walikuwepo 204 huku associate wakiwa 309 na Phd wakiwa 514 wote hawa wanatengeneza staff ya watu 1,027. Hawa ndio wataalamu wabobezi wanaohudumia vyuo vyote vya Seriali nchini hadi kufikia 2016.

Hadi kufikia 2016 kuliwa kuna vyuo vikuu zaidi ya vinne havina Prof hata mmoja huku kimoja cha serikali kikiwa na Prof mmoja.Nafikiri hivi ni vile vilivyonyimwa udahili wa wanafunzi.

Chuo kilichokuwa kinaongoza kwa kuwa na maprof wengi ni chuo cha SUA kikiwa na maprof 75 huku UDSM ikiwa na maprof 67 hadi kufikia 2016. Kwenge vyuo vya binafsi kuna balaaa kubwa....

Kenya wao miaka 3 iliyopita walikuwa na maprofesa kwenye vyuo vyao vya Serikali 5,189, jumlisha hawa wakwetu kama hata wanafika nusu.

Kenya Kwa mwaka wanazalisha Phd 1,000 huku Tanzania tukizalisha chini ya 500 kwa mwaka.

Tanzania Imefikia mahali umri wa kustaafu wa maprofesa chuoni umeongezwa hadi karibu kufikia miaka 80. Hiki ni kiashiria cha Tatizo kubwa lililopo.

Vyuo vyetu vya binafsi vimeanza kuajiri maprofesa toka nchi jirani kama Kenya huku tukipigana kusema ajira hakuna....

Ni wakati sasa wa Serikali kufikiri namna bora ya kuboresha maslahi ya hawa wataalamu wanaokimbilia kwenye siasa ili wabaki kuzalisha wataalamu wengine.

Wanavyuo wengi wanaomaliza vyuo vikuu kwa sasa hata kuandika barua ya kuomba kazi hawawezi inawezekana ni ukisefu wa wataalamu bora mavyuoni.... .... mimi Sijui.

Ukiangalia bidhaa zinazotengenezwa hapa kwetu ni za kuhesabu ila kila mwaka vyuo vyetu vikuu na vyuo vya kati vinamwaga maelfu ya wahandisi mtaani..... jamani hata Toroli mmeshindwa kulitengeneza....

Hata wataalamu waliobakia wameshaanza kuwa na element za siasa inawezekana nao wapo njiani kutoka. Siku hizi wanajitokeza hadharani kabisa na kusifia chama fulani bila woga... wanakaa karibu na wanasiasa ili kuambulia chochote.......

Haya tunayazungumza huku kada ya Siasa ikiwa inadharau kazi nyingi za wataalamu. Jiulize ni Tafiti ngapi zipo kwenye maktaba zetu za vyuo vikuu na jiulize zinatumika wapi. Katika hali hiyo unafikiri kuna haja ya hawa wataalamu kuumiza kichwa huku kazi zao zikiwa hazitambuliki au wavae Suti wakapige mabenchi makofi pale Dodoma huku wakiingiza mamilioni.??

Ni aibu kwa profesa aliyebaki pale Muhimbili kuzidiwa mshahara na kibajaji na kina mlinga hahahahaha, Natania tu ila unaweza kuona ni kwa namna gani hawa wataalamu wetu wanavyojiongeza. Unamwona Dr. Bana anavyojitutumua? Nani anataka kustaafu na kiinua Mgongo cha ajabu ajabu?

Angalia Umri wanaoondoka nao hawa kina Kitila mkumbo, Dr Tulia na Sasa Bashiru Ally. Ni Umri uliokuwa unahitajika haswa katika kuzalisha wataalamu. Ila tujiulize nini kingeweza kuwashawishi kubaki pale mlimani zaidi ya kukimbilia kwenye Siasa? Jambo pekee ni Maslahi. Kwa maana hiyo tusiwalaumu hata kidogo wamewaza njee ya Box

Kila La kheri Dr Bashiru

Ole Mushi.
0712702602.
 
Ngoja wafanye siasa kwa sababu hicho ndio kitu tunachokiweza kwa kiasi fulani, hayo mengine tunasindikiza tu.
 
Kwa asili binadamu wanao ubinafsi kabla ya kuwajali wengine

Ngoja washibe kwanza kisha wakisaza watawakumbuka MAKAPUKU wanaohitaji maisha bora kupitia elimu

Nami nasema Hongera Dr Bashiru Ally kwa nafasi hiyo,achana na mahitaji ya wengi pigania yako kwanza
 
Kwakweli mkuu kwa wakati ni mwingine kwa yule anayepigania tumbo lake, lakini pia inauma kwa upande wa taifa. Watoto wetu watasoma vyuo hivihivi, wadogo zetu pia. Ndiyo maana haina maana kumsomesha mtoto shule ya msingi mpaka sekondari kwa mamilioni, kisha anakuja kuishia kwenye vyuo vyetu hivi!!
 
WINO WA DHAHABU..... NILIWAHI KUANDIKA.

SIASA INAVYOVUNA WATAALAMU.

Na Thadei Ole Mushi.

Pale alipo Dr. Mwakyembe, Dr. Tulia,Pro Kabudi, Pro Mbarawa na huko anakokimbilia Prof Kitila Mkumbo na sasa Dr Bashiru Ally ndiko kwenye pesa ya maana.

Kwa Taarifa yako Katika ukanda wa Afrika mashariki Tanzania ndio nchi pekee yenye maprofesa na watu wenye Phd wachache kuliko nchi giants za A. Mashariki na kusini mwa jangwa la sahara. Pamoja na uchache wao Siasa inazidi kuwavuna kila siku... huko ndiko kuliko na Maslah mapana.

Kwa statistics za mwaka 2016 Vyuo vikuu binafsi nchini vilikuwa 35 ila vilikuwa na maprofesa 74 tu hawa ni wale maprofesa kamili. Associate walikuwepo 56 hawa ukijumlisha na hao 74 unapata 130. Associate maana yake ni accademic rank iliyopo kati ya assistant professor na Full professor (operational meaning)

Ambao wana Phd kwenye vyuo vya binafsi ambao wanafundisha ni 138. Ukijumlisha na idadi ya maprofesa unapata 268. Hawa ndio wanaohudumia karibu zaidi ya nusu ya wadahiliwa wote Tanzania wanaosoma vyuo vya binafsi.

Kwa upande wa serikali Full Prof walikuwepo 204 huku associate wakiwa 309 na Phd wakiwa 514 wote hawa wanatengeneza staff ya watu 1,027. Hawa ndio wataalamu wabobezi wanaohudumia vyuo vyote vya Seriali nchini hadi kufikia 2016.

Hadi kufikia 2016 kuliwa kuna vyuo vikuu zaidi ya vinne havina Prof hata mmoja huku kimoja cha serikali kikiwa na Prof mmoja.Nafikiri hivi ni vile vilivyonyimwa udahili wa wanafunzi.

Chuo kilichokuwa kinaongoza kwa kuwa na maprof wengi ni chuo cha SUA kikiwa na maprof 75 huku UDSM ikiwa na maprof 67 hadi kufikia 2016. Kwenge vyuo vya binafsi kuna balaaa kubwa....

Kenya wao miaka 3 iliyopita walikuwa na maprofesa kwenye vyuo vyao vya Serikali 5,189, jumlisha hawa wakwetu kama hata wanafika nusu.

Kenya Kwa mwaka wanazalisha Phd 1,000 huku Tanzania tukizalisha chini ya 500 kwa mwaka.

Tanzania Imefikia mahali umri wa kustaafu wa maprofesa chuoni umeongezwa hadi karibu kufikia miaka 80. Hiki ni kiashiria cha Tatizo kubwa lililopo.

Vyuo vyetu vya binafsi vimeanza kuajiri maprofesa toka nchi jirani kama Kenya huku tukipigana kusema ajira hakuna....

Ni wakati sasa wa Serikali kufikiri namna bora ya kuboresha maslahi ya hawa wataalamu wanaokimbilia kwenye siasa ili wabaki kuzalisha wataalamu wengine.

Wanavyuo wengi wanaomaliza vyuo vikuu kwa sasa hata kuandika barua ya kuomba kazi hawawezi inawezekana ni ukisefu wa wataalamu bora mavyuoni.... .... mimi Sijui.

Ukiangalia bidhaa zinazotengenezwa hapa kwetu ni za kuhesabu ila kila mwaka vyuo vyetu vikuu na vyuo vya kati vinamwaga maelfu ya wahandisi mtaani..... jamani hata Toroli mmeshindwa kulitengeneza....

Hata wataalamu waliobakia wameshaanza kuwa na element za siasa inawezekana nao wapo njiani kutoka. Siku hizi wanajitokeza hadharani kabisa na kusifia chama fulani bila woga... wanakaa karibu na wanasiasa ili kuambulia chochote.......

Haya tunayazungumza huku kada ya Siasa ikiwa inadharau kazi nyingi za wataalamu. Jiulize ni Tafiti ngapi zipo kwenye maktaba zetu za vyuo vikuu na jiulize zinatumika wapi. Katika hali hiyo unafikiri kuna haja ya hawa wataalamu kuumiza kichwa huku kazi zao zikiwa hazitambuliki au wavae Suti wakapige mabenchi makofi pale Dodoma huku wakiingiza mamilioni.??

Ni aibu kwa profesa aliyebaki pale Muhimbili kuzidiwa mshahara na kibajaji na kina mlinga hahahahaha, Natania tu ila unaweza kuona ni kwa namna gani hawa wataalamu wetu wanavyojiongeza. Unamwona Dr. Bana anavyojitutumua? Nani anataka kustaafu na kiinua Mgongo cha ajabu ajabu?

Angalia Umri wanaoondoka nao hawa kina Kitila mkumbo, Dr Tulia na Sasa Bashiru Ally. Ni Umri uliokuwa unahitajika haswa katika kuzalisha wataalamu. Ila tujiulize nini kingeweza kuwashawishi kubaki pale mlimani zaidi ya kukimbilia kwenye Siasa? Jambo pekee ni Maslahi. Kwa maana hiyo tusiwalaumu hata kidogo wamewaza njee ya Box

Kila La kheri Dr Bashiru

Ole Mushi.
0712702602.

Sioni kwa nini tuwe na hofu ya kutumia wanataaluma kwenye civil service na hata inapotokea kazi maalumu za kisiasa. Hawa ni watu ambao wanauelewa mpana wa mambo na ni fursa kwao kutumia upande wa pili wa taaluma yao. Wakati mwingi wamekuwa watu wa kufanya tafiti na kutoa mapendekezo " reccomedations". Sasani wakati wao kuja kwenye utekelezaji.

Pili, sioni haja ya kuwa na hofu kwa chuo kikongwe kama UDSM au SUA kuwa na wasiwasi kinapoondokewa na mwana taaluma mmoja kwenda kuisaidia nchi kuwa na wasi wasi. Vile ni Vyuo vikongwe vina hazina kubwa ya wataalam , na vinazalisha vipaji kila siku
 
Baba wa Taifa mwalimu JK N aliacha kufundisha sekondari akaenda kuwa mwanasiasa;

Elimu haikuanguka!!
 
Halafu sasa, huko kwenye siasa hakuna lolote la maana wanalofanya. wasomi wa nchi hii hawana faida yoyote. Wamelitia hasara taifa kwa kuwasomesha.......ndio hawa akina Lipumba.
 
Imagine gharama inayotumika kumtengeneza dr au prof, halafu anakuja kuishia kutumika kama sijui nani wa chama. anakwenda kushindana hoja na yule wa Geita au wa Mtera
 
Sioni kwa nini tuwe na hofu ya kutumia wanataaluma kwenye civil service na hata inapotokea kazi maalumu za kisiasa. Hawa ni watu ambao wanauelewa mpana wa mambo na ni fursa kwao kutumia upande wa pili wa taaluma yao. Wakati mwingi wamekuwa watu wa kufanya tafiti na kutoa mapendekezo " reccomedations". Sasani wakati wao kuja kwenye utekelezaji.

Pili, sioni haja ya kuwa na hofu kwa chuo kikongwe kama UDSM au SUA kuwa na wasiwasi kinapoondokewa na mwana taaluma mmoja kwenda kuisaidia nchi kuwa na wasi wasi. Vile ni Vyuo vikongwe vina hazina kubwa ya wataalam , na vinazalisha vipaji kila siku

Mkuu hofu ipo kwenye student profession ratio. Wanafunzi laki 6 kwa Ph.D. 1000 kweli??
Halafu tunashangaa kwanini elimu haitukomboi.
Halafu tunashangaa kwanini wahitimu hawana maarifa?!!
Halafu tunashangaa kwanini wahitimu hawaajiriki?!!
haya bana, tuendeleage tu
 
Imagine gharama inayotumika kumtengeneza dr au prof, halafu anakuja kuishia kutumika kama sijui nani wa chama. anakwenda kushindana hoja na yule wa Geita au wa Mtera
Jambo gumu kabisa kwa wengi wetu kulielewa ni kuwa serikali ya Tanzania imekuwa serikali tegemezi kabisa kwenye kusomesha watalaamu wake baada ya kiwango cha degree ya kwanza. Tumekuwa tunategemea wahusani na sasa tumefikia hatua bila miradi ya nje au scholarship hatuna uwezo kabisa kusomesha masters na phd. Hata vyuo vina wakati mgumu kupanga programu za kuongeza utalaamu wa walimu wake. Tuna waliobobea kwenye fani A lakini sasa wanafundisha fani B kwani hicho (A) ndiyo walichosoma ingawa walitakiwa wakachukue fani B. Kuna idara zimepoteza maprofesa wa kutosha na hii ina athiri ufundishaji.
Dawa ni moja serikali itenge fedha za kutosha za kusomesha wahadhiri nje na ndani ya nchi. Kumbuka pia wengi hutumika kufanya kazi za ushauri na zikizidi zina athiri ufundishaji wao. Kwa hiyo idara inaweza kuonekana iko sawa maprofessa wengi lakini kuwakuta darasani inakuwa kazi.
 
Imagine gharama inayotumika kumtengeneza dr au prof, halafu anakuja kuishia kutumika kama sijui nani wa chama. anakwenda kushindana hoja na yule wa Geita au wa Mtera
Hayo ni mapendekezo binafsi ya mtu mwenyewe afanye wapi kazi usijekuwageuza watu mali ya umma kwa kigezo cha kupewa mkopo na serikali wakati wengine mkopo wenyewe walishaulipa wote.
 
Kujenga human capital kunahitaji planning na investment kubwa sana. Huwezi ukawekeza kwenye asilimali watu halafu akaja mwingine akaharibu ile mipango hata kama kila mmoja wetu ana uhuru wa kwenda kuuza mbongo zake apendapo. Linalotokea sasa ni serikali kuchomoa watu bila kuwa na njia maalum ya kujazia nafasi zile kwa mtiririko unao faa. Matokeo yake kuna idara katika vyuo vya serikali zina athirika. Na sirahisi kuwapata wengine nje ya vyuo kuja kuziba nafasi hizo kwa muda uafaka.

Imagine gharama inayotumika kumtengeneza dr au prof, halafu anakuja kuishia kutumika kama sijui nani wa chama. anakwenda kushindana hoja na yule wa Geita au wa Mtera
 
Kujenga human capital kunahitaji planning na investment kubwa sana. Huwezi ukawekeza kwenye asilimali watu halafu akaja mwingine akaharibu ile mipango hata kama kila mmoja wetu ana uhuru wa kwenda kuuza mbongo zake apendapo. Linalotokea sasa ni serikali kuchomoa watu bila kuwa na njia maalum ya kujazia nafasi zile kwa mtiririko unao faa. Matokeo yake kuna idara katika vyuo vya serikali zina athirika. Na sirahisi kuwapata wengine nje ya vyuo kuja kuziba nafasi hizo kwa muda uafaka.
Amekuwa Einstein Albert mpaka awe hadimu kiasi Hicho kuwa replaced.? Bado wapo wengi kwenye pipeline
 
Kwanza sio wengi kama udhaniavyo, pili pipe line yetu ina vipande hakuna kitu cha kuflow ndio maana serikali inahangaika na retirement age ya wahadhiri. Walianza 55, wakaenda 60 na leo ni 65. Juilize kwa nini kama ingekuwa rahisi kuwa replace wahadhiri.
 
Professor kahigi na Baregu hawajatajwa,wametajwa waliopo ccm tu,hii inafanya bandiko liwe irrelevant
 
Nimekaa na kufikiria kwa KIPINDI sasa,mwisho Nimegundua ukweli kuwa tatizo la wasomi Tanzania BADO lipo.
Kwa akili yangu, mtaalamu ni mtu huru asiye na ushabiki Wala upande kwa nafasi YAKE ya utaalam.
Mfano, daktari bila kujali Hali ya mgonjwa anastahili kuokoa MAISHA YAKE kwa kumtibia kwa UJUZI wake.
Leo nimeona wataalamu wanakuwa na upande ,wanatumia utaalam WAO kwa ushabiki na wanasahau kuwa WAO NI tunda la Taifa ZIMA.
Mfano hii Unaweza KUNIONA ktk maeneo mbalimbali ,Leo uzalishaji wa wataalamu ktk vyuo vyetu vikuu Unaelekea kusimama baada ya wataalamu hao kuondoka na kuenda kutumikia maeneo YAO wanayoshabikia na kuacha Jamii KUBWA inayowategemea wasijue cha KUFANYA.
Wataalamu waliobaki nao Naamini wanaelekea kuacha Fani ZAO za Kuitumikia Jamii na kuenda Kuendeleza ushabiki WAO.
WAPO wataalamu waliokuwa na mvuto MKUBWA HAPA nchini na walikuwa wakisimamia mambo ya watu WENGI kimtizamo, na walisifika kwa misimamo, Leo wamewaacha watu na kubadili misimamo na mitazamo YAO ili kuenda kuendeleza ushabiki.
Taifa litajengwa na watu (wasomi,wafanya kazi, na wakulima),Kama hawa WOTE wataacha jukumu HILI na kuenda kushabikia ni dhahiri kuwa Taifa litasimama!
 
Back
Top Bottom