Siasa ni uchumi, miundombinu Dar Es Salaam inaua uchumi, tubadili masaa ya kazi!

siyabonga

Senior Member
Jan 25, 2012
125
35
Wakuu, kwa hali ilivyo sasa na hasa kwa wakazi wa Dar Es Salaam, Jiji linalochangia kwa kiasi kikubwa mapato katika Tanzania, hali ya msongamano wa magari na foleni barabarani inatisha. Watu wanalala na kuamka barabarani!

Siasa zinatakiwa zijielekeze katika kujenga uchumi, lakini katika eneo hili uchumi umeachwa uteketee.

Kwa hakika muda ambao wakazi wengi wanatumia kwenda na kurudi katika kazi zao za ujenzi wa Taifa ni mkubwa mno { Ukiacha wale wachache ambao labda hawaoni kwa kuwa wanakimbiza na vimuli muli!}. Masaa mengi yanapotezwa barabarani. Tathmini za kiuchumi zinaonyesha Taifa linapata hasara kubwa na kuzidi kudorora kwa utendaji kazi na utoaji wa huduma.

Kwa upande mwingine, kazi mbalimbali za ujenzi na uboreshaji wa miundombinu Dar Es Salaam, zinazofanyika kwa hivi sasa zinakwenda kwa spidi ya kinyonga na hazionyeshi kutoa suluhisho la muda mfupi na mrefu katika tatizo hili ambalo ni sugu kwa hivi sasa.

Ni vema basi wakati suluhisho la muda mrefu likiendelea kufanyiwa kazi,ikiwamo ujenzi wa miundombinu, ujenzi wa miji midogo, kupeleka baadhi ya huduma nje ya mji, nk, tupunguze msongamano kwa kubadili masaa ya kazi ili kutoa nafasi ya kupishana na kupunguza foleni.

Muda wa kazi ubaki kuwa masaa 8 kwa siku, lakini kazi zianze saa 3 asubuhi kwa maofisi yatakayoainishwa baada ya tahmini kufanyika.
 
Back
Top Bottom