Siasa ni maendeleo si uhasama: Tulinde amani na mshikamano wa taifa kwa maendeleo endelevu

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
81
Reaction score
95
Katika kipindi hiki tumeshuhudia mijadala ya kisiasa ikizidi kuwa mikali na yenye hisia kali. Hali hii inatukumbusha umuhimu wa kurejea kwenye misingi imara ya taifa letu: amani, umoja na mshikamano. Kwa maslahi ya Taifa, ni vyema wanasiasa, wanaharakati wa haki za binadamu na wadau wote wa kisiasa kujiepusha na lugha ya uchochezi inayoweza kuhatarisha utulivu wa nchi na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Tanzania imejijengea sifa ya kuwa kisiwa cha amani barani Afrika tangu enzi za waasisi wake, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume. Msingi wa taifa letu umejengwa juu ya utu, kuheshimiana na kutanguliza maslahi ya nchi mbele ya itikadi binafsi. Leo tunaposhuhudia mvutano wa kimtazamo, ni muhimu kujiuliza: je, tunalinda urithi huo au tunauweka rehani?

Siasa ni Njia ya Maendeleo

Lengo la siasa si kugombanisha watu bali kuleta maendeleo. Vyama vya siasa vipo ili kutoa dira mbadala za kiuchumi, kijamii na kisera. Ushindani wa kisiasa unapaswa kuwa wa hoja — nani ana sera bora za kupunguza umaskini, kuboresha elimu na afya, kuongeza ajira, kukuza uchumi, kuboresha miundombinu na kuweka mazingira rafiki kwa biashara na uwekezaji.

Katika mfumo wa vyama vingi, ni jambo la kawaida kwa vyama vya siasa kama Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Wananchi (CUF), ACT Wazalendo, NCCR-Mageuzi au Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutofautiana kimtazamo. Tofauti hizo hazipaswi kuwa chanzo cha chuki, bali kichocheo cha mjadala mpana unaolenga kuboresha maisha ya wananchi.

Msisitizo wa Uongozi wa Taifa

Mara kadhaa,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa ukosoaji wenye nidhamu, akieleza kuwa serikali inahitaji maoni na ushauri wa kujenga ili kuimarisha utendaji na demokrasia. Amekuwa akihimiza siasa za ustaarabu, akisisitiza kuwa amani, mshikamano na maridhiano ni mtaji mkubwa wa Taifa letu.

Kauli hizi zinatukumbusha kuwa ukosoaji si uadui. Ukosoaji unapofanywa kwa hoja, husaidia kurekebisha kasoro, uwajibikaji na kuboresha mifumo ya uongozi. Lakini ukosoaji unapogeuka kuwa matusi au uchochezi, hupoteza lengo lake na kuhatarisha umoja wa kitaifa.

Athari za Lugha ya Uchochezi

Lugha kali na za kudhalilisha huongeza mgawanyiko wa kijamii, hujenga chuki na kuondoa imani miongoni mwa wananchi. Wakati mwingine, maneno yanaweza kuchochea vitendo visivyotarajiwa vya vurugu. Historia inaonesha kuwa migogoro mingi huanza kwa maneno — maneno yanayopandikiza hofu, hasira na taswira hasi dhidi ya wengine.

Taifa linapofika mahali pa kuhalalisha lugha ya uchochezi, huanza safari ya kuyumba kwa mshikamano wake na heshima yake kimataifa.

Wajibu wa Viongozi na Wananchi

Wanasiasa na wanaharakati wana ushawishi mkubwa kwa jamii. Wanapozungumza, wafuasi wao husikiliza. Hivyo, ni wajibu wao kupima maneno yao na kutambua athari zake. Ukosoaji uwe wa hoja, si wa matusi, upotoshaji, uchochezi au kutweza utu.

Wananchi pia wana wajibu wa kuchuja taarifa wanazokutana nazo, hasa katika mitandao ya kijamii. Si kila taarifa ni sahihi, na si kila ujumbe una nia njema kwa Taifa. Busara ya pamoja inahitajika ili kulinda amani tuliyonayo.

Tanzania Ndiyo Nyumbani

Mwisho wa yote, tukumbuke kuwa Tanzania ndiyo nyumbani kwetu sote. Hatuna taifa jingine la kukimbilia pale mambo yanapoharibika. Tofauti za kisiasa ni za msimu; taifa ni la kudumu. Leo tunaweza kutofautiana kwa sera, kesho tunakutana sokoni, ibadani, shuleni, kazini au kwenye shughuli za kijamii.

Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa siasa zinabaki kuwa chombo cha maendeleo, si chanzo cha mafarakano. Tuwe na ushindani wa hoja, si wa chuki. Tuwe na mijadala ya sera, si ya matusi. Tuwe na ukosoaji wenye nidhamu na ustahimilivu kama ambavyo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anavyosisitiza.

Tulinde amani, tuimarishe mshikamano, na tujenge taifa lenye maendeleo endelevu. Tusisahau Tanzania ni nyumbani.

Kwa Maoni Na Ushauri
0768497974
 
The best article of the day,
well done gentleman:KasugaYeah:
 
Huu uchawa mtupu. Kuna mambo mhimu ya kushughulikia wakati huu:
1. Waliouwa vijana wetu O29 wawajibishwe. (Kama ni suala la kuzuia vurugu , kulikuwa na nafas ya kutumia risasi za mpira, gesi ya machozi, maji ya upupu etc)
2. Maiti wakabidhiwe kwa ndugu zao wazikwe kwa heshima.
3. Ule uchafuzi ufutwe, iundwe tume huru, uchaguzi mkuu ufanyike haraka iwezekanavyo.
4. Mchakato wa kuandika katiba mpya urejewe haraka, tupate uhuru kwa mara ya ili(second liberation).
 
Back
Top Bottom