Siasa na Sheria: Dada na Kaka..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa na Sheria: Dada na Kaka.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, May 5, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika hali ya kawaida na maisha ya kila siku ni vigumu kutenganisha vitu hivi viwili. Haviwezi kutenganishwa kwa sababu aidha kimoja kinasaidia kingine au kimoja kinaharibu kingine.

  Hapa kwetu malalamiko mengi yanatokana na aidha sheria au wanasheria au siasa na wanasiasa.

  Huko Uganda wanasheria wametamka kwamba hawataenda mahakamani kwa siku tatu kupinga vitendo vya unyanyasaji na ukiukaji wa haki za binadamu vinavofanywa na serikali. Hili jambo la kupongeza.

  Endapo sisi wanasheria tungeweza kugoma angalau kwa siku moja kupinga malipo ya Dowans, Mikataba mibovu, hali ngumu ya maisha nk basi jamii yetu ingetuthamini zaidi na tungekuwa tumetekeleza wajibu kwao.

  Niko kwenye dilemma, kama mwanasheria na mwanasiasa.....what a mix to be in!
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mkuu, interesting point. Lakini nadhani sheria inaingia katika kila angle ya maisha. Sio kwenye siasa tu. Siasa ina-determine mwelekeo wa jamii ambao mwishowe huishia katika kuwekwa katika sheria. Mfano ni taxation. Taxation sio ishu kubwa hapa bongo, lakini ni ishu kubwa sana katika nchi zilizoendelea. Kila chama kina policy zake tofauti katika hili. Na kila chama kinachoshika madaraka lazima kitaweka/kitabadilisha sheria ya tax kuendana na policies zake. Wanasheria hawawezi kugoma pale ambapo hizi tax laws zinabadilishwa.
  At the end of the day, mwanasheria una jukumu kwa mahakama na client. Hayo ndio majukumu yako makubwa. Kwangu mimi, kwa mwanasheria kugoma kutokana na siasa ni kuvuka mpaka. Badala yake: Kwa nini mshiishtaki serikali kwa kuvunja sheria?
   
Loading...