emmanuel1976
JF-Expert Member
- Jun 17, 2011
- 301
- 80
Poleni sana kwa mafuriko hasa wale waliokutwa nayo!
Wana jamvi habarini za asubuhi. Natumaini hamjambo. Kwa miaka mingi hapa kwetu Tanzania kumekuwa na dhana kwamba viongozi wa dini hawapaswi kuingilia masuala ya siasa kwa maana ya ama kukemea viongozi wa kisiasa wanapopotoka ama wakati wa kuwaweka viongozi madarakani (chaguzi mbali mbali). Hali hii imeenda umbali hadi kufikia wana siasa kuwakemea viongozi wa dini kutojihusisha na masuala yanayohusu siasa hasa pale viongozi wa dini wanapokuwa kinyume na watawala wetu.
Mwaka 2005 wakati Mhe. Dr. Jakaya Kikwete alipokuwa anawania uongozi wa juu kabisa wa nchi hii (urais) baadhi ya viongozi wa dini walisikika wakiushawishi umma wa watanzania kuwa Mh. Dr. Kikwete ndiye aliyekuwa chaguo la Mungu. Kampeni hii ilifanikiwa sana na hivyo kumwingiza Rais Kikwete madarakani kwa zaidi ya 80% ya kura zote za watanzania. Hapo hakuna aliyesema siasa na dini havichangamani wala kuhusiana, hakuna aliyekemea wala aliyekemewa.
Katika siku za karibuni viongozi hao hao wa kidini kwa nafasi zao na kwa uzalendo wao kwa mara nyingine wamejitokeza kuikosoa serikali na chama tawala kwa mambo wanayodhani yamekiukwa na moja kati ya mambo hayo ni kutupwa kwa rasimu ya Jaji Joseph Waryoba ambayo kimsingi ndiyo maoni ya wananchi. Hilo limezua balaa hadi kufikia wizara ya mambo ya ndani ya nchi kutishia kuzifuta NGOs, TAASISI ZA DINI ZIKIWA WALENGWA ikiwa zitabainika kujihusisha na mambo ya uchaguzi mkuu 2015 ama kuipinga katiba pendekezwa.
Je ni kweli kwamba siasa na dini haziingiliani? kama jibu ni ndiyo, kivipi?
Asanteni na karibuni kutoa mchango muhimu kwa wakati muhimu..tunapoelekea uchaguzi mkuu 2015.