Siasa mpaka kwenye maisha ya watu, soma hii tafadhali-mwananchi


commited

commited

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,617
Points
1,195
Age
28
commited

commited

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,617 1,195
Ubabaishaji kila sehemu..

1. Kuna mzaiwa ya kopo miaka ya 1995 yalisambazwa sana madukani watoto wetu wakayanywa mwaka 2000, wakasema maziwa yale yanasumu
2. Juzi arv bandia
3. Miaka ya 2008 zilikuja fansida watu wakachubuka mpaka basi
4. Sasa hivi bidhaa feki kila sehemu
5. Mwezi wa 5 mwaka 2012 vikafungiwa vipimo feki vya kujipima ukimwi baada ya watu kuvitumia kwa zaidi ya miezi 6

wataalamu wapo, sisi ni wakupokea kila kinachokuja mbele yetu... Serikali imetulia tu tutakufa sana


HAYA LEO MWANANCHI LIMEIBUKA NA HILI

Sindano uzazi wa mpango balaa

UTAFITI umebaini kuwa sindano za uzazi wa mpango zinachangia kasi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kuwa zina vichocheo vingi ambavyo vinahuisha virusi vya Ukimwi katika nyumba ya uzazi na kuvipa nguvu ya kusambaa.

Inaelezwa kuwa walio katika hatari zaidi ya maambukizi hayo ni wanawake walioko katika ndoa kwa kuwa ndiyo wanaotumia zaidi sindano hizo.

Utafiti huo uliofanywa na wanasayansi wa Marekani na kuripotiwa na gazeti la The Guardian la Uingereza, umebaini kuwa wanawake wanaotumia sindano za uzazi wa mpango wapo katika hatari mara mbili ya kupata maambukizi ya Ukimwi au kuwaambukiza wenzi wao, kuliko wengine.

Katika utafiti huo uliofanywa katika nchi saba zinazoendelea barani Afrika ikiwamo Tanzania, wanasayansi hao kutoka Chuo Kikuu cha Washington, walipendekeza ushauri zaidi utolewe kwa wanandoa kabla mtu hajajiingiza kwenye matumizi ya sindano kama njia ya kupanga uzazi.

Utafiti huo ulifanyika kwa wanandoa 3,790 kutoka nchi za Tanzania, Afrika Kusini, Zimbabwe, Uganda, Kenya, Rwanda na Botswana, ulichapishwa kwa mara ya kwanza katika Jarida la Afya la Lancet kabla ya kunukuliwa na gazeti la The Guardian.

Utafiti umebaini pia kuwa zaidi ya wanawake 140 milioni duniani wanatumia njia mbalimbali za uzazi wa mpango, huku wanandoa wengi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, wanaoishi na VVU wakichagua kutumia sindano kama njia ya kuzuia mimba zisizotarajiwa.

Wanasayansi hao walikusanya taarifa kati ya wanandoa 3,790 ambao mmoja wao anaishi na VVU na mwenza wake akiwa hana maambukizo.

Aidha, wanawake ambao wanaishi na VVU na wanatumia sindano hizo pia walikuwa katika hatari zaidi ya kuwaambukiza wenzi wao.

Vipimo vilionyesha kuwa sindano hizo ambazo zina vichocheo ambavyo vinavipa nguvu virusi ndani ya nyumba ya uzazi (cervix).

Imeelezwa kuwa njia za uzazi wa mpango zinazohamasishwa zaidi na kupendwa zaidi na wanawake ni sindano, ambazo wanawake wanasema kuwa zinadumu kwa muda mrefu na zinaweza kutumika bila ya ruhusa au mume kufahamu.

Kiongozi mkuu wa utafiti huo, Renee Heffron wa Chuo Kikuu cha Washington alisema sindano za uzazi wa mpango zina vichocheo vingi ambavyo huvihuisha vijidudu vya Ukimwi katika nyumba ya uzazi na kuvipa nguvu ya kusambaa.

"Ni vyema sasa kama tutasisitiza njia za uzazi wa mpango ambazo ni salama zaidi kama vile mipira ya kiume au njia nyingine ambazo hazina vichocheo (hormones) au zina kiasi kidogo cha vichocheo," alisema Dk Heffron.

Mwanasayansi mwingine, Charles Morrison wa Kituo cha Afya cha Durham, nchini Marekani alisema uhamasishaji wa matumizi ya sindano za uzazi wa mpango unachochea maambukizi zaidi katika nchi za Jangwa la Sahara.

"Ushauri wangu kwa nchi zinazoendelea ni kuacha matumizi ya njia za uzazi wa mpango zenye vichocheo, ili tupunguze maambukizi, jibu la tatizo hili linatakiwa litafutwe sasa, nchi zinazohusika zinatakiwa zishiriki katika hili," alisema.

Alivitaka vituo vya afya vitoe ushauri kwa wanawake kutumia kondomu badala ya sindano au vidonge.

Mara nyingi watu wanaotumia vidonge, wengi si wanandoa, mtu anayemeza vidonge vya kuzuia mimba anaogopa zaidi mimba, si Ukimwi.

Huchoche hamu ya mapenzi

Mfamasia katika Kitengo cha Dawa kwa watu wanaoishina VVU katika Hospitali ya Amana, Christopher Masika alisema anaafiki kuwa sindano na hata vidonge vinaweza kuwa ni sababu inayochochea maambukizi kwa sababu ya uhuru.

"Ninachokiona mimi katika hilo ni uhuru. Mtu anapotumia sindano huwa huru kufanya ngono kwa kuwa hana hofu ya mimba, hicho kinaweza kumfanya apate maambukizi kwa urahisi, tofauti na anapotumia kondomu," alisema.

Alisema wapo baadhi ambao wakitumia sindano hizo vichocheo vinawafanya wapate hamu zaidi ya kufanya mapenzi, hivyo huanza kutembea na wanaume wengine.

Aliongeza kuwa mtu anayeishi na VVU akizuia mimba kwa njia ya sindano, ni rahisi kupata maambukizi mapya kutoka kwa mwenza wake.

Masika alisema wanawake wapewe elimu zaidi kwani wapo ambao wanadanganywa kuwa njia za uzazi wa mpango kama sindano, povu zinaweza kuzuia maambukizi, jambo ambalo si la kweli.

Wakati huohuo baadhi ya wanandoa wanaoishi na VVU wanaopata matibabu katika Hospitali ya Amana wamesema kuwa tangu waanze kutumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) hamu ya kufanya mapenzi imeongezeka kwa kasi kubwa.

Mkuu wa Kitengo cha Utafiti cha Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Dk Arodia Mulokozi, alisema taasisi yake haiwezi kuzungumza lolote kuhusu utafiti huo, badala yake alilitaka Mwananchi kuzungumza na Kitengo cha Afya ya Uzazi wa Mpango cha Muhimbili.

"Hatuhusiki na masuala ya uzazi wa mpango, nafikiri unaweza kuzungumza na Kitengo cha ‘Reproductive Health' cha Muhimbili," alisema Dk Mulokozi.

Waziri wa Afya hakupatika, lakini msemaji wa wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja alisema ni mapema mno kuchangia kuhusu utafiti huo, atafanya hivyo pindi atakapopata taarifa zaidi.

Mratibu wa Mpango wa Uzazi wa Mpango Tanzania (Umati), Dk Morris Hiza amekiri kuufahamu utafiti huo, lakini akaeleza kuwa haujajitosheleza na bado una maswali mengi.

"Nilikuwapo wakati Heffron anawasilisha utafiti wake mjini Geneva, lakini nakumbuka mkutano ule wa WHO (Shirika la Afya Duniani) uliukataa," alisema.

Alieleza kuwa Heffton alifanya utafiti huo kwa nyani na wanawake makahaba pekee.
 
M

mwinukai

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Messages
1,448
Points
1,225
Age
35
M

mwinukai

JF-Expert Member
Joined May 3, 2011
1,448 1,225
Sasa tumekuwa biashara ya CCM, WAMEUZA madini na raslimali sasa wanatuuuza na sisi wenyewe

Haya MADABIDA mwenye kiwanda cha ARV feki si huyo sasa amekuwa Mwenyekiti wa CCM, Dar Es Salaam, kwa kifupi bila skendo huwezi pata jina CCM
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
33,240
Points
2,000
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
33,240 2,000
Kuleta siasa kwenye maisha ya watu ni makosa---Mrisho Mpoto
 
mauro

mauro

Senior Member
Joined
Nov 28, 2011
Messages
109
Points
195
mauro

mauro

Senior Member
Joined Nov 28, 2011
109 195
MM nimesoma Mwananchi kuhusu sindano za majira nimegwaya mwenyewe. Sisi ni watu wanafanyia majaribio hizi dawa zao_Only in Tanzania.
 
OLESAIDIMU

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2011
Messages
19,165
Points
1,250
OLESAIDIMU

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2011
19,165 1,250
Haitoshi kuwa ni Taarifa kamili juu ya hili...............kuna mengi sana ya kujibiwa

1. Ni vipi vichocheo hivyo vinasababisha mihemko????

2. If so kwa wenye mihemko inayochelewa au passive wanaweza kutumia vichocheo hivyo kama msaada????

2. Mtu akikubali na kuanza kutumia ARVs sio tu huongeza hamu ya mapenzi bali pia hata kula, kufanya kazi, mazoezi na juhudi za maisha kwa ujumla......ni kama psychological response/ counselling effect on the fact that maisha yanaweza kuendelea despite the sero +ve status so yaweza kuwa ni more of psychology kuliko ARV as in chemical effects
 
S

Savannah

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
239
Points
0
Age
67
S

Savannah

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
239 0
Hayo ndiyo matokeo ya kuwa na serikali ya mafisadi na wala rushwa was CCM.
 
sindano butu

sindano butu

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2012
Messages
484
Points
225
Age
31
sindano butu

sindano butu

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2012
484 225
PINDA ALISHASEMA; liwalo na liwe na hamna mjadala kwa kuwa kesi ipo bungeni!
 
B

Bahati Risiki

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Messages
530
Points
0
B

Bahati Risiki

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2012
530 0
Ukiona watu wanaendelea jua kuna wanaorudi nyuma kuwaachia nafasi. Wachina hawalali na wameshajua Tanzania ni shamba la mazezeta ambayo hayana mwenyewe. Angalieni kampuni za simu sinavyovuna nchi utadhani bustani ya shemeji. Angalieni mavitu feck kila upande. Kinachofurahisha watanzania wanajisemea serikali itaangalia. Ninajiuliza serikali ni nani? Tangu lini Tanzania ikawa na serikali au kiongozi mwenye uchungu hata na maisha ya watu kama sii madini, wanyama, ardhi, mashirika ya umma na kadhaklika? Tunauawa huku tunaangalia tu!!!!!!!!!!
 

Forum statistics

Threads 1,296,597
Members 498,672
Posts 31,253,387
Top