Kuna habari kwamba serikali yetu ya Jamhuri ya Tanzania imeiangukia ile ya Uingeleza (iliyotutawala miaka hiyo) watusaidie kutupatia mabehewa na vichwa vya train ambavyo hawavitumii.
Napata shida mno kuliafiki jambo hili, hivi ni kweli kabisa kwa karne hii ya 21 ya Sayansi na Technologia bado tunaomba vitu ambavyo wenzetu wameziona havifai kutumika kwa wananchi wao ila sisi ndiyo tunaona vinatufaa?
Kwa raslimali tulizonazo lukuki tunashindwa kujenga reli ya kisasa ya takribali km 1200 tu? naongelea hii moja tu ya Dar es salaam hadi Mwanza.
Je kuna haja ya kujivunia Uhuru wetu ambao umetimiza miaka 51 kama hata kujenga Reli ya km 1200 hatuwezi kuijenga?. maana hii tunayoitumia walitujengea Wajerumani enzi za utawala wao wa Tanganyika miaka takribani 100 na ushee iliyopita.
Je nikisema watanzania tunajiaibisha wenyewe na tunaziaibisha pia nchi za ki- africa kwa kuendekeza omba omba - yaani kutembeza BAKULI kwa wazungu nitakuwa nimekosea?
Hebu tufumbuane macho kama wazo hili lina mashiko.