Si unajida unajua Kiswahili!!

Si unajida unajua Kiswahili!!

Jamaa mmoja alikuwa akiishi na mdogo wake na mama yake, pia wakawa na kambwa ambako jamaa alikapenda mno.

Siku moja akapata safari ya wiki moja, siku aliporudi tu kabla hajaingia ndani, mdogo wake akamuwahi;

DOGO: Kaka mbwa wako kafariki juzi......jamaa alisikitika sana, na zaidi hakupenda jinsi alivyopewa taarifa ya msiba huu

MJAMAA: We vipi unaona nilivyoshtuka,
ilitakiwa jambo la msiba kama hili ungeanza kunambia, mbwa wako yuko juu
kwenye paa, halafu unanambia mbwa kadondoka toka kwenye paa, nakuwa nimejitayarisha kisaikolojia

DOGO: Sawa kaka ntajirekibisha

MJAMAA: Mama yuko wapi?

DOGO:
Mama yuko juu kwenye paa

MJAMAA: Ehh!(akapoteza fahamu)
tafsiri ya jamaa; hapo mother ameishadead tiyari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom