Si tuliambiwa GSM ataishia kwenye mabango? Imekuwaje tena nembo yake iwe kwenye jezi za Simba?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
- Klabu ya Simba imekataa kuvaa logo ya mdhamini mwenza wa ligi kuu (GSM)

- CEO wa klabu hiyo Barbara Gonzalez amesema wameandika barua bodi ya ligi kuomba ufafanuzi baada ya kuambiwa kuanzia mchezo ujao wanapaswa kuvaa logo ya mdhamini mwenza wa ligi kuu (GSM)

- Kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu Tanzania bara 🇹🇿, ukikataa kuvaa logo ya mdhamini unapigwa faini ya Tsh milioni 3 kwa mechi.

- Ukiendelea kukaidi, unashushwa daraja.

- Mkataba waliosaini GSM na TFF masharti yaliyopo kutoka GSM ni kuwa, logo yao inapaswa kukaa upande wa kushoto wa jezi.

- Tayari Simba SC walishapewa logo hizo na mamlaka za soka nchini wazitumie kuanzia mchezo unaofuata wa derby ya Kariakoo.
 
Jamani kwani GSM Ni Yanga sc? Huyo CEO wenu akapimwe kichwa si bure
Kwamba kila mdhamini anapaswa kuweka nembo yake kwenye jersey? Kama mkataba unzihusu moja kwa moja team kwanini mkataba usainiwe bila kushirikisha team za ligi kuu kupitia Bodi ya ligi? Yani mkataba usainiwe na TFF bila kuzishirikisha team Kisha ipelekwe nembo kwenye hizo team?

Inajulikana GSM ni mzalishaji wa jersey za UTOPOLO, SIMBA SC nayo ina mzalishaji wake ambaye ni VUNJABEI, inakuwaje wazalishaji wawili wahusike kwenye jersey moja yani kwamfano PUMA na NIKE wakae kwenye jersey moja?

Mpira wa TZ hautafika popote kwa style hii, ndio tunahitaji wadhamini lakini si katika hali ambayo haina utaratibu.Kama kula mdhamini atataka akae kwenye jersey itakuwaje Sasa😅.

Wao wawekwe hata kwenye mango huko, hela yenyewe kidogo wanataka wavaliwe kwenye jersey , wangetoa mpunga kama wa AZAM ingekuwaje Sasa.
 
Acheni maneno ya mtaani, nani/wapi ilitoka taarifa kuwa hiyo logo itakaa kwenye jezi au itawekwa kwenye mabango tu?hayo masharti uliyaona wapi?soka la bongo bana ni pasua kichwa sana.
Sasa kama team yenyewe inayotakiwa kuvaa hizo jersey hakushirikishwa katika hayo makubaliano kupitia BODI YA LIGI , inategemea kusitokee mgongano? Kama zitaishia kwenye mabango hapo ni sawa, lakini kama SIMBA SC itatakiwa kuvaa hiyo nembo basi haikuwa sahihi wao kutoshirikishwa kupitia wawakilishi wao ambao ni Bodi ya LIGI.
 
Kwamba kila mdhamini anapaswa kuweka nembo yake kwenye jersey? Kama mkataba unzihusu moja kwa moja team kwanini mkataba usainiwe bila kushirikisha team za ligi kuu kupitia Bodi ya ligi? Yani mkataba usainiwe na TFF bila kuzishirikisha team Kisha ipelekwe nembo kwenye hizo team?

Inajulikana GSM ni mzalishaji wa jersey za UTOPOLO, SIMBA SC nayo ina mzalishaji wake ambaye ni VUNJABEI, inakuwaje wazalishaji wawili wahusike kwenye jersey moja yani kwamfano PUMA na NIKE wakae kwenye jersey moja?

Mpira wa TZ hautafika popote kwa style hii, ndio tunahitaji wadhamini lakini si katika hali ambayo haina utaratibu.Kama kula mdhamini atataka akae kwenye jersey itakuwaje Sasa😅.

Wao wawekwe hata kwenye mango huko, hela yenyewe kidogo wanataka wavaliwe kwenye jersey , wangetoa mpunga kama wa AZAM ingekuwaje Sasa.
Hayo Sasa Ni masuala ya kimkataba Baina ya hao GSM na waendeshaji wa ligi husika. Ninachopinga Ni kusema GSM Ni Yanga sc
 
Back
Top Bottom