ESPRESSO COFFEE
JF-Expert Member
- Sep 6, 2014
- 6,170
- 7,661
Kampuni Ya GSM, Leo Tarehe 07/02/2022 imetangaza kujiondoa Kwenye Udhamini Mwenza Wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ikimbukwe kuwa Kampuni Ya GSM iliingia Makubaliano Ya Kuidhamini Ligi Kuu Tanzania Bara Na Kuweka Dau la Bilioni 2.5.
Lakini Udhamini Huo Ulipingwa Vikali na Simba Sc huku Vilabu vingine 16 vyote vya Ligii kuu Tanzania Bara Vikiridhia Udhamini Huo, Lakini Kwa Sasa GSM wamejiondoa Na Si wadhamini Tena.
Leo Kampuni Ya GSM imeeleza Ya Sababu Ya Kujitoa kuwa ni Kwasababu, TFF na Bodi La Ligi Kushindwa Kutimiza Matwaka ya Kimkataba.
Bado Haijaelezwa Wazi Matakwa Hayo ya Kimkataba ni Yapi Ambayo TFF na Bodi Ya Ligi Hawajatimiza hadi kupelekea Mkataba kuvunjwa. Lakini moja Ya Matakwa ya Kimkataba ilikuwa ni Vilabu Vyote kuvaa Nembo ya Mdhamini Upande Mmoja Wa Bega katika Jezi na Simba Sc Ndio Club Pekee iliyokuwa haijafanya Hayo.
Takwa jingine ilikuwa ni Mabango ya Mdhamini mwenza kuwepo Uwanjani lakini Simba Sc Ilipinga vikali na kutokuweka mabango hayo katika Mechi Zake.
Kwenu Studio