Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Tuliposema hapo awali ya kwamba udhamini wao haukuja kusaidia klabu zote kuendeleza mpira Tanzania ila walilenga kuweka logo yao kwenye Brand ya Simba SC baadhi walipinga vilivyo.
Ukisoma sababu ya kujiondoa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania kwenye barua yao kwenda TFF zipo sababu 8, lakini Simba SC wameitaja mara 4, wakiamini kuwa Simba ndo amevuruga lengo.
Moja ya paragraph ambayo wameitaja Simba SC katika zile sehemu 4 wamesema, Nanukuu "GSM kwa makusudi tumenyimwa haki ya kuonekana kwenye bega la kushoto la jezi ya Simba SC". mwisho wa kunukuu.
Logo ya GSM kuwa kwenye jezi ya Simba SC sio shida, lakini inakaa kwa misingi ipi? Yakisheria ya mkataba, ilhali TFF walisema mkataba ni wa kificho (Siri) baina ya TFF na GSM na hapo ndo mashaka yalianzia.
Kwahivyo nia ilikuwa Simba SC amtangaze kwa bei rahisi Kitaifa na Kimataifa hivyo akajipenyeza kwenye udhamini wa Ligi Kuu, lakini lengo ameilenga Simba SC ndo maana unajiuliza mbona kuna timu zipatazo 15 kwenye Ligi Kuu na zimekubali kudhaminiwa, iweje kukataa timu moja ndo ujiondoe kudhamini vilabu 15 vilivyosalia..?!
Neno letu la mwisho TFF pamoja na TPLB wasimamie kulipwa vilabu vyote 15 vilivyo kubali udhamini, kwani kuna vilabu vimevaa jezi zenye matangazo na baadhi ya michezo inarudiwa kwenye Tv na kuacha kumbukumbu isiyofutika.
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
...Ghazwat....