Si sahihi kutumia jina "Mkuu" kwa kila mtu.

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,051
3,255
Hili neno limeshamiri huku JF.
Mwanzoni lilianzia humu , lakini sasa limeshika kasi na watu wanaitana Mkuu .
Imekua tofauti kwa watu wa JF kwani humu unakuta hadi mwanamke anaitwa "mkuu".

Je,binafsi nimelijulia wapi neno hili "mkuu" ?

Arusha ndipo Kumbukumbu zangu zinanipeleka , kipindi hiko Apolo wa Migodi ya Mererani Walikua wakiwaita wakuu wao wa kazi Majina Kama Fogo, Renga,Taita na Mengineyo mengi , maneno hayo hayo yalikua yakitumika pale mtu tajiri sana alipokua anazungumziwa especially wenye Utajiri uliotikana na Biashara ya Mawe/Madini. Hivyo basi kadiri mda ulivyosonga neno "Mkuu" lilibuka wakiwa na maana hizo hizo za awali.

Nimejiuliza , humu JF ni wote wanaoitana "mkuu" wanastahili Heshima hiyo . ?
Je ni sahihi kwa Jinsia zote kulitumia neno "mkuu" ?

Kwa heshima ya watu wa Mererani/Arusha Boys/Gentles nalifananisha Neno "mkuu" msabaha kabisa na neno "Sir"

Ni vigumu Mzungu kumtunuku mtu neno Hilo pasi kua kapamvania Jambo Fulani .

Naomba tungalie namna Ya Kulitumia neno hili.
Ahsanteni.
 
Mkuu Mandella kila mtu ni mkuu kwenye eneo husika ukiwa baba au mama wa familia tayari ni mkuu hata ukiwa kaka au dada kwenye familia yenu tayari ni mkuu siyo lazima uwe tajiri kama mabilionea wenu wa Arusha au uwe mwanasiasa ndiyo uwe mkuu.
 
JF hakuna watu. Tuna ID za watu. Sasa hauwezi kujua nani ni nani kiuhalisia. Ili kupata neno linaloweza kutumika kwa watu wote bila kujali hinsia wala hali zao, nakutokuathiri heshima za watu wenye hizi ID, Mkuu limeonekana kuwa bora zaidi kutumika JF.
 
Mkuu, neno mkuu au utambulisho huu hutumika hapa JF kwa sababu :
-kuweka aina ya heshima miongoni mwa wana JF,
-kutochanganya jinsi ya mwana JF (ke au me),
-kuongoza mijadala na mada/nyuzi zote kwa adabu, utangamano na weledi. Kwa maana palipo na heshima kuna maridhiano. Na palipo wengi kuna mengi pia.
Hivyo basi, neno au kitambulisho cha mkuu kina maana kubwa sana kwa JF! Asante mkuu.
 
Back
Top Bottom