Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,807
- 730,157
Kuna post yenye footage ya tukio la kupora, kuua na kujeruhi hapa jukwaani. Inasemekana marehemu alitoka bank kuchukua kiasi cha 15,000,000/=. Kiulaini kabisa jamaa wamempiga risasi na kuchukua begi la mihela na kutokomea kusikojulikana.
Nataka kuzungumzia kwa upande mwingine matukio ya namna hii, majambazi wapo na wanapora kujeruhi na kuua kila siku lakini mara nyingi ukiwa mpole bila kubishana nao huwa hawakufanyi chochote (sio wote lakini ).
Kuna matukio ya kushangaza mtu kavamiwa nyumbani au kwenye gari hakuna purukushani yoyote lakini watu wanaua na kuchukua pesa, hapa kuna zaidi ya tukio la uporaji hapa kuna kudhulumiana na kuzidiana ujanja.
Tunafahamu watu wanavyoishi mishahara ni midogo haitoshi na changamoto ni nyingi na kwakweli hauwezi kukidhi mahitaji yote... kwahiyo watu huishi kwa dili za wizi rushwa ten percent na ubadhilifu mbali mbali, hakuna kitu kinachoumiza kama mwenzenu mmoja kuwadhulumu pesa ya dili kwa namna yoyote ile.
Kuna wengine husamehe na kubaki na kinyongo rohoni
Kuna wengine hupotezea na kusubiri dili nyingine ili naye alipizie
Kuna wengine huenda kwa waganga kufanya yao
Kuna wengine huunguza picha polisi ofisini au popote patakapokuharibia
Lakini kuna hawa ambao hawana roho ya huruma hawa wanakumaliza tena kwa risasi , ambayo ndio njia rahisi zaidi
Iwe ni pesa halali au ya wizi au ya dili ridhika na mgao wako usitake zaidi kwa njia ya kudhulumu, kila mtu ana matatizo yake kila mtu anahitaji pesa kila mtu anaijua pesa....usifanye ujinga utakaoigharimu familia yako ukaacha mjane na yatima.