Si kweli swala hili wapinzani wanachokiongea

Si kweli swala hili wapinzani wanachokiongea

Joined
Aug 25, 2025
Posts
16
Reaction score
9
Nchi ya Tanzania ni nchi ambayo imekuwa katika msingi ya haki na demokrasia na haya ndio yanayoleta matokeo ya amani.

Lakini amani ambayo ndani ya nchi tunayo ni kitu ambacho kinawaumiza wale ambazo hawapendi kuona Tanzania inayoongozwa na Dkt.Samia suluhu ikiwa nayo na hapa ndio inakuwa kutokea wanaandaa dhana mbalimbali ili tu wafifishe na kuchafua utawala wa Mama yetu Raisi wa jamhuri na hapa Kuna baadhi ya vitu nitagusia.

1. Ishu ya kusema kuwa hakuna uhuru wa kuongea ni swala ambalo limekaa kupotosha watu kwa sababu tunashuhudia taasisi mbalimbali zikitoa maoni Yao kuhusu serikali na serikali imekuwa ni sikivu, vyombo vya habari vinaongea, vyama vya kisiasa vina uhuru wa kuongea na hata mwananchi mmoja mmoja. Je Leo hii hatua wapinzani wanaongea mfano mpina, heche, mwalimu, n.k

2. Swala la pili ni swala la utekaji. Hilo swala linapingwa vikali sana na serikali ya Mhe.Dkt. Samia suluhu na amekuwa hata akitoa amri kwa jeshi la polisi kuzidi kupambana na hili janga na mfano wa hutuba mbalimbali za mama mmoja wapo ni akiwa anavunja bunge. Lakini sasa ndo wanakuja watu ambao si wema na uongozi huu wa sasa na kuchafua kwa kusema ni Jeshi la polisi ndilo linalohusika. Hapa Kuna baadhi ya matukio nitajaribu kuyafafanua

SATIVA: Huyu jamaa bwana kama tunavyoelewa kuhusu sakata lake ni alichukuliwa na kwenda kutupwa Katavi na alipatikana akiwa na majeraha mbalimbali likiwemo na Hilo la risasi, kutokana na maelezo yake anasema ni Jeshi la polisi ingawa hakuna ushahidi unaonesha au kuthibitisha kuwa ni kweli jeshi la polisi limehusika.

Yule alikuwa anajihusisha na maswala ya betting katika makundi mbalimbali pengine alimdhurumu mtu katika hayo maswala na hakuna anayejua Kati yetu Ila yeye anasema watekaji ni polisi kwa sababu walijitambulisha hivyo, jamani hakuna mtekaji atakayekuja kujitambulisha mbele ya umati kama yeye ni mtekaji ni lazima watumie mwamvuli wa jeshi ili kurahisisha kazi yake mfano kwenye hili Kuna sakata LA (Yule aliyetaka kuchukuliwa na vijana watatu maeneo ya kibamba lakini ikashindikana, na wale pia walijitambulisha kama ni maaskari lakini kiuhalisia hawakuwa maaskari) kupitia hapa tu unaona ni mbinu gani ambayo watekaji wanatumia ili kuchafua Jeshi la polisi na serikali kwa ujumla.

Na hapa ili kuona serikali haikupenda tukio la sativa kutekwa Mhe. Raisi alimchangia Sativa kiasi cha Tsh 30M kwa ajili ya matibabu na bado jeshi liliendelea kuhakikisha linatafuta haki ya Sativa. Kwaiyo Kuna baadhi ya watu au vyombo vimelipwa ili kujakuchafua taswira nzima ya serikali bora ya Dkt. Samia suluhu
 
Back
Top Bottom