Si kila kitu kinahitaji jibu leo

Joined
Apr 6, 2024
Posts
65
Reaction score
62
πŸŒ™ SAIKOLOJIA YA JIONI | R.J. COUNSELLING & ROBERT JAMES PODCAST

β€œSi kila kitu kinahitaji jibu leo.”


Wakati mwingine akili huchoka si kwa sababu ya kazi nyingi tu, bali kwa sababu tunajaribu kutatua kila jambo kwa wakati mmoja.

Jioni inapofika, usilazimishe akili yako kupata majibu ya matatizo yote. Baadhi ya mambo yanahitaji muda, utulivu na mtazamo mpya.

🧠 Ushauri wa kisaikolojia:
Chagua jambo moja linalokusumbua zaidi, jiulize β€œNi sehemu gani ya hili ninayoweza kuidhibiti?”
Shughulikia hiyo sehemu na yale ambayo yako nje ya uwezo wako, jifunze kuyaacha kwa muda.

Utulivu wa akili hauimaanishi matatizo yamekwisha; wakati mwingine humaanisha umeacha kuyabeba yote kwa wakati mmoja.

🌿 Pumzisha akili. Kesho endelea.

R.J. COUNSELLING & ROBERT JAMES PODCAST
Counselling Psychology β€’ Mental Well-being β€’ Psychological Education
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…