Si bure!

Si bure!

dalalitz

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
3,476
Reaction score
2,087
Najua na ninafahamu wapo watakaokataa,
Wapo watakaoponda na kubeza hoja hii kwa kuwa huionea aibu ingawa ina ukweli na pengine wao ni wafuasi wazuri pia.

Ni ukweli usiopingika kuwa wenye mafanikio wengi (Si wote) Ukichekecha upenuni siri ya mafanikio yao baadhi ni Uozo na Kichefuchefu kitupu na pengine aibu.
Wameyapata mafanikio hayo kwa njia zisizo za kiungwana na wanayalinda hivyohivyo pia,
Na vilevile maisha yao yanaonekana kwenda sawa kila siku yaani wapo vizuri.

Fikiria:

Una Mke/Mume ambae umeridhika nae, mmeshajenga familia nzuri tu,mmedumu kwa muda wakutosha na maisha yanakwenda wote mkiwa na furaha.
-Lakini kumbe yeye (mwenza wako) Kuwa nawe/kukupata na kufanikiwa kuishi nawe, Upo mkono wa kishirikina
(Kakufanyia Madawa ili kukupata na anakuweka/kakutuliza kwa madawa hayohayo)
-Haya Yapo na ni Maisha watu wanaishi.
AU
Ili, Mambo ya mwenza wako yaende sawa,
Shurti afanye ushirikina na wewe ukijua kabisa na kwa kuwa umo tayari katika ndoa na unajua kuwa hiyo ndio njia ya kupata mkate wa watoto unashirikishwa unakubali katika kufanya hayo makitu.
-Ni maisha pia.

Unaishi na Mumeo/Mkeo mmedumu si kidogo, Maisha yanaenda unafahamu kazi anayoifanya kumuingizia kipato siku zote.
Lakini, Kumbe kazi hiyo ni Kichaka cha shughuli nyingine Chafu na isiyosemeka katika hadhara pengine Mwizi ama Jambazi.
-Nayo ni maisha na watu wanaishi.

Ili upate mkate wako wa kila siku na 'ka-extra' inakubidi umdanganye Boss au Kumhadaa Mteja, Kufanyia wengine Fitna, Majungu, Uchonganishi,Uongo na wakati mwingine Ugombanishi-Na hatimae mkate wako unapatikana.
-Ni maisha na watu wanaishi.

Waswahili wanasema Si bure!
 
Ni kweli na pengine uwongo, ila ungelijua alacho bata usingetamani nyama yake, ila je unaweza kuishi bila kumla bata?? na kingine..Unatambuaje ushirikina tuseme kwenye ndoa kama na wewe hutatumia ushirikina??

Kuhusu kazi:
Ili mradi unapata ugali mezani kila siku, ya nini uanze kuchunguza kazi ninayoifanya??(Hapa ndo napowapenda wanawake wa kichagga) hata kama kazi ni ya ajabu namna gani as long as inatunza familia, she will keep her mouth shut jambo linalowashinda wanawake wa kiswahili atapenda aanze kujisifia oooh mume wangu hivi, ooh mume wangu kazini kwake oooh kapandishwa cheo...woooiii!

Hata kama si bure...KWANI SH NGAPII??
 
Tanzania kuna USHIRIKINA wa ajabu. Angalia hivyo vibao njiani, utasikia mganga wa asili, anatibu nguvu za kiume, kumleta mpenzi karibu, kusafisha nyota, kupandishwa cheo.

Hayo makanisa ya kisasa ndo usiseme, all they preach now is money...wealth...success... Jinsi ya kuvipata hivyo ndo ujiulize sasa, then majibu yake utapata.
 
Ushirikina katika mapenzi upo lakini sio katika kiwango kikubwa.
 
Ushirikina katika mapenzi upo lakini sio katika kiwango kikubwa.

Mind your language! Zaidi ya asilimia themanini ya wanawake wanaoenda kwa waganga wanaendea sababu za mapenzi. Aidha wapate ndoa haraka, au watulize waume zao, kuwapumbaza kiakili wapunguze ukali, wapewe mali nyingi na hao waume zao pamoja na kuwaroga baada ya kuachwa. Hayo ni machache tu kati ya mengi
 
Na wewe ni mganga?
 
Pesa ndo kila kitu haijarishi najituma vp kuzichanga!
inasikitisha sana ke kumwendea me kwa waganga kumfanya poyoyo asitoke kwenda kuhangaika kutafta salarii. Haya mambo yanafanyika sana ukanda wa mwambao hasa Tanga! Siku zote ntamkubali ke anaenishurtsha kutafta mkate, sio anaependa muda wote nimpakate!
 
Ni kweli na pengine uwongo, ila ungelijua alacho bata usingetamani nyama yake, ila je unaweza kuishi bila kumla bata?? na kingine..Unatambuaje ushirikina tuseme kwenye ndoa kama na wewe hutatumia ushirikina??

Kuhusu kazi:
Ili mradi unapata ugali mezani kila siku, ya nini uanze kuchunguza kazi ninayoifanya??(Hapa ndo napowapenda wanawake wa kichagga) hata kama kazi ni ya ajabu namna gani as long as inatunza familia, she will keep her mouth shut jambo linalowashinda wanawake wa kiswahili atapenda aanze kujisifia oooh mume wangu hivi, ooh mume wangu kazini kwake oooh kapandishwa cheo...woooiii!

Hata kama si bure...KWANI SH NGAPII??
Duu!! Unauliza shing' ngapi tena?,
Kama 'Unavyowadekia' madada wa kaskazini a.k.a 'Pesa-Kwaaa,PesaKwanza aisei',
Itakuwa Manka ulienae keshakuambukiza 'UjasiliaPesa' wewe.
Safi kuona ujumbe umefika.
 
Mind your language! Zaidi ya asilimia themanini ya wanawake wanaoenda kwa waganga wanaendea sababu za mapenzi. Aidha wapate ndoa haraka, au watulize waume zao, kuwapumbaza kiakili wapunguze ukali, wapewe mali nyingi na hao waume zao pamoja na kuwaroga baada ya kuachwa. Hayo ni machache tu kati ya mengi
Tell dem,
 
Back
Top Bottom