SHY-ROSE BHANJI: Wanawake msikate tamaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SHY-ROSE BHANJI: Wanawake msikate tamaa

Discussion in 'Celebrities Forum' started by nngu007, Mar 8, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Amana Nyembo

  [​IMG]
  KILA ifikapo Machi 8 ya kila mwaka, dunia nzima huadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, ikiwa ni pamoja na kupinga unyanyasaji dhidi yao.
  Wakati dunia ikiwa inaadhimisha siku hii, wanaharakati wa masuala la kijinsi na haki za binadamu wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawake wanapata haki sawa na wanaume katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kielimu na kiuongozi.
  Mapambano hayo yameshamiri kutokana na kuwepo kwa mfumo dume, unaowaona wanawake kama watu wasio na thamani mbele ya jamii, wakati kuna wanawake wengi wenye michango mikubwa katika jamii hii, kuliko hata wanaume.
  Akizungumzia siku hii jijini Dar es Salaam, Shy-Rose Bhanji, ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya kijamii anasema hapa nchini Siku ya Wanawake imechukuliwa kirahisi sana wakati ina umuhimu mkubwa katika kuleta mabadiliko kupitia wale wanawake waliopata maendeleo kuwaelimisha wengine.
  Shy-Rose (40), ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, anasema katika maisha yake hapendi kukumbuka mazingira ya shida aliyopitia, ndiyo maana amekuwa mstari wa mbele kusaidia wale wasiojiweza ili nao wapate faraja na kusahau shida.
  “Namshukuru Mungu amenipa moyo wa kuchukia pale ninapoona jamii inataabika…ndiyo maana nimekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii na kuhamasisha vijana na wanawake katika masuala mbalimbali ili waweze kujiamini katika kila kitu wanachofanya.
  “Binafsi huwa natenga asilimia 10 ya mshahara wangu wa kila mwezi kusaidia makundi ya wasiojiweza, ninasomesha watoto kadha kwa kuwalipia ada ya shule na vitu vingine vingi, ambavyo nilipokuwa mdogo sikuweza kuvipata...pia sipendi kuona watu wakipata matatizo. Huwa ninaamini kuwa pesa yoyote unayoipata inakuwa si yako bali inapitia kwako kusaidia wenye matatizo. “Nikiwa na umri mdogo nilifiwa na wazazi wangu, hivyo huwa sipendi kukumbuka mazingira ya shida niliyopitia wakati huo,” anasema Shy-Rose ambaye amezaliwa jijini Dar es Salaam na kukulia na kusomea elimu ya msingi jijini Mwanza, sekondari, elimu ya juu na kupata shahada ya uandishi wa habari.

  Baadaye alipata stashahada kwenye uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Wales, Cardiff, Uingereza.
  Shy-Rose ambaye ni mchanganyiko wa damu; baba yake akiwa Mhindi na mama yake akitokea Mkoa wa Mara, Musoma Vijijini, anazungumza Kihindi bila matatizo na Kijita kidogo.
  Akizungumzia baadhi ya vyombo vya habari kubeba habari mbaya kuhusu yeye, anasema huwa hapendi kufikiria mabaya tu kwani hata anapoona ameandikwa vibaya kwenye magazeti huwa anamshukuru Mungu, kwa sababu hajawahi kumwangusha hata mara moja.
  “Nikiandikwa vibaya kwenye gazeti huku kukiwa na habari iliyobeba sura yangu huwa nalia sana. Unajua sijawahi kuandikwa vizuri, vyote vinavyoandikwa ni vibaya tu…mbona vizuri kuhusu mimi haviandikwi?”anahoji Shy-Rose na kusema kuwa anaamini alipotoka ni mbali na anapoelekea anakaribia kufika.
  Anasema watu hawamjui Shy- Rose ni nani, hivyo hakuna kitu kinachomuumiza moyo kama kupotosha yeye ni nani, lakini akiwa mwanamke shupavu huwa anajitahidi kufanya mambo yake na kuyasahau hayo.
  “Mimi ni binadamu, naomba jamii inielewe kuwa siku hizi kumekuwa na habari zinapikwa kuhusu mimi, lakini hazina ukweli wowote,” anasema na kuongeza kuwa:
  “Unajua mimi najiamini, katika wanawake waliojitahidi mimi ni mmoja wao. Siamini kama nimewahi kufanya kitu kibaya katika dunia hii.”
  Anasema amekuwa mfano wa kuhamasisha vijana kujaribu katika masuala mbalimbali, kama vile alipothubutu kupambana ili kupata tiketi ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Shy- Rose anasema ingawa alishindwa kwenye kura za maoni lakini ana imani kuwa hiyo ni sehemu ya mafunzo kwake na vijana wengine.
  Hata hivyo anasema anajivunia kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake (UWT-CCM), kuwakilisha vijana Mkoa wa Dar es Salaam hadi taifa, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Dar es Salaam, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutoka Wilaya ya Kinondoni na Kamanda wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Kata ya Kijitonyama.
  Anasema amejikuta akiwa mbele kwa kila kitu, lengo likiwa ni kuwasaidia watu.
  “Mwaka 2007 niligombea viti vya kifo Nec…Hivi viti wanawake huwa hawagombei lakini mimi nilijitosa, mwisho wa siku nilishindwa na wanaume kwa kura chache sana. Sikukata tamaa, tulifanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya Jaka Mwambi, aliyejiuzulu, baada ya kuteuliwa na rais kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, mwanamke nikiwa pekee,” anasema na kuongeza kuwa aliopambana nao ni aliyekuwa meya wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa na Peter Serukamba.
  Anasema suala la yeye kujiingiza katika siasa limetokana na mazingira aliyoyapitia hususan kuanzia shuleni, kwani alikuwa akipewa nafasi za kuwaongoza wenzake.
  “Kuingia katika siasa kumetokana na mazingira, nilipokuwa sekondari nilikuwa kiranja. Nilipojiunga na masomo ya uandishi wa habari niliteuliwa kuwa Waziri wa Habari na Utangazaji,” anafafanua Shy-Rose.
  Akitoa ushauri kwa wanawake, anasema wasikate tamaa kwa kile wanachokifanya kwa sababu kila jambo linakuja baada ya kujaribu, huwezi kukaa kisha mafanikio yakaja bila jitahada zozote. “Lazima u-struggle ndipo ufanikiwe, wengi huwa wanafanya vitu lakini hawafanikiwi kutokana na kukata tamaa,” anasema. Anasema kupitia Siku ya Wanawake Duniani, wale waliokuwa juu kiuongozi wawe njia ya kuwasaidia wengine ili nao wafike hapo walipo wao.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  March 8th - Ni Tarehe ya kuashiria Mafanikio ya Wanawake.
   
Loading...