Shule zote za sekondari ziwe na masomo ya VETA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Niliwahi ongea na baadhi ya wazee waliosoma zamani wakaniambia zamani walisoma shule za msingi zilizokuwa na masomo ya Ufundi zote(TRADE SCHOOLS).Wakitoka walikuwa wanaweza kujitegemea kwani walikuwa wanaweza fanya kazi kama za useremala nk

Ili mwanafunzi akitoka awe na uwezo wa kujitegemea nashauri katika mipango ya elimu shule zote za sekondari masomo yaliyoko VETA yawe sehemu ya masomo ya lazima mwanafuzi kusoma.Masomo yatakayoingizwa kwenye mitaala yawe yale yanayohusiana hasa na mazingira yetu yanayotuzunguka.Masomo yanayoweza kuwemo ni kama kilimo,ufugaji wa mifugo mbali mbali ikwemo ufugaji wa samaki,Upishi,utengenezaji bidhaa mbali mbali kutokana na vile tunavyozalisha nchini au malighafi zake nyingi ziwe zile za nchini.

Watoto wengi wamekuwa wakionekana kama hawapendi kilimo na ufundi sababu ni kuwa hawafundishwi mashuleni.Mtoto kazaliwa gorofani kakulia gorofani unategemea atapenda kilimo na ufugaji wakati saa zote anasoma vitabu tu vya tuition kutwa? Ndio maana lazima kama nchi iwasaidie masomo yawepo sekondary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Nimependekeza sekondary sababu walau watoto wanakuwa wakubwa kidogo ndio umri wa kufundishwa kujitegemea
 
Mkuu, kinachotakiwa ni kubadili mtazamo wa kifikra tu wa wanafunzi waambiwe ingali wakiwa chekechea kwamba "wanasoma kutafuta maarifa ili wakajiajiri".

Hii ikijengeka akilini mwao wakimaliza wataelekea ktk shughuli ambazo babu na bibi zao wanazifanya na kuendesha maisha pasipo kupiga kelele ya kutaka ajira.

Hatuwezi tukafundisha skills zote za maisha ktk elimu ya msingi na sekondari. Mengine watajiongeza tu wakiwa mtaani.
 
Mkuu kumbe kuna wakati unaongea vitu vya maana namna hii .... Just kidding

Kwakwel tuna changamoto kubwa saana kwenye mfumo wetu wa elimu, watoto wanafundishwa vitu vizuri tu (content) lakin wanatoka hawajaelewa kitu, japo wengine wamefaulu hivo hivo.

Shule zimekuwa sehem ya kuharibu vijana wakawa watu wa hovyo kuliko ambao hawajaenda....

Shughuli kubwa anayoweza kuifanya aliyeishia form four ni bodaboda, kunyoa saloon, kubet ni mengine kama hayo. Hawezi akalima kitaalam wala kufufa, hajui hata dawa moja kusaidia kuku wasife japo yote hayo yapo kwenye vitabu vyake vya shule. Hana mbinu yoyote ya kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikumba jamii yake, japo lengo la elimu ilikuwa kuongeza ubunifu ili tuwe na watu wa kusaidia kupunguza changamoto kwenye jamii..

Me ningeona hiki kilimo tufundishane kwa Kiswahili, huenda walimu wenyewe hawajaelewa wanachokifundishaga. halafu mwanafunzi anayemaliza kidato cha nne awe pia na stashahada kilimo na ufugaji, yaani wajue hasa, ili hata mengine yakishindikana basi walime na wafuge.

Somo la stadi za kazi lifundishwe, ili mwenye kipaji chake atokee kidato cha nne.
 
Niliwahi ongea na baadhi ya wazee waliosoma zamani wakaniambia zamani walisoma shule za msingi zilizokuwa na masomo ya Ufundi zote(TRADE SCHOOLS).Wakitoka walikuwa wanaweza kujitegemea kwani walikuwa wanaweza fanya kazi kama za useremala nk

Ili mwanafunzi akitoka awe na uwezo wa kujitegemea nashauri katika mipango ya elimu shule zote za sekondari masomo yaliyoko VETA yawe sehemu ya masomo ya lazima mwanafuzi kusoma.Masomo yatakayoingizwa kwenye mitaala yawe yale yanayohusiana hasa na mazingira yetu yanayotuzunguka.Masomo yanayoweza kuwemo ni kama kilimo,ufugaji wa mifugo mbali mbali ikwemo ufugaji wa samaki,Upishi,utengenezaji bidhaa mbali mbali kutokana na vile tunavyozalisha nchini au malighafi zake nyingi ziwe zile za nchini.

Watoto wengi wamekuwa wakionekana kama hawapendi kilimo na ufundi sababu ni kuwa hawafundishwi mashuleni.Mtoto kazaliwa gorofani kakulia gorofani unategemea atapenda kilimo na ufugaji wakati saa zote anasoma vitabu tu vya tuition kutwa? Ndio maana lazima kama nchi iwasaidie masomo yawepo sekondary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Nimependekeza sekondary sababu walau watoto wanakuwa wakubwa kidogo ndio umri wa kufundishwa kujitegemea
Wahitimu wa shule za sekondari/msingi iwe kwa yoyote ya certification kama hakuna mazingira ya kuwa-absorb baada ya masomo ya Carpentry, automotive, plumbing bado tunakuwa hatujafanya kazi ya kutosha.

Tusitafute quick fix kwa kudhani VETA au Technicians wa vyuo kama Mbeya Tech, Arusha Tech na Dar Tech kama zitarejeshwa kama kuongeza ufanisi wa hawa vijana kufanya miujiza.

Ni lazima Taifa lije na ubunifu wa kufanya liwalo na liwe ili kuzalisha kampuni za hawa wajuvi wa VETA wafanye kazi kama kampuni na sio in isolation.

Kwanini tuna garage za wachina wanaengeneza magari yetu mengi second hand na hatuwapi graduates wa VETA?

Ukienda SINO garage wana tools, equipment za kisasa na management system ya kuhudumia wateja.

Ilitakiwa VETA kwa kushirikiana na Brela na baadhi ya wahitimu wa vyuo vya biashara kujenga team ambayo inasailiwa kama kampuni. Then wanapewa mikopo ya equipment na all working tools na eneo la kujenga uzio ili kufanyia kazi magari yetu yakiharubika.

haina maana garage za waswahili ni chini ya miti na wana spanner chache, kwanini wasikopesheke chini ya usimamizi walimu wa VETA on how to start business, manage and scale up.

Sasa iwe ni plumbing, electrical au carpentry na serikali kupitia VETA wanawapa tenda walau kwa level ya kuwa sub-contract kwenye miradi ya serikali au wawekezaji wa private sector.

That is how we should build inclusive economy.

Ushuri wangu, ili mbegu iote na kuzaa matunda ni lazima kuwa na supportive system; temperate, oxygen na moisture.

Mbegu ikiota lazima ilindwe, imwagiliwe na kuwekewa mbolea ili kupata maximum production kutoka kwenye mbegu.

Nadhani wizara ya Ajira ina Waziri ambaye ka-focus kwenye kazi za kibunge na hana DNA na innovation kuzalisha ajira kwa vijana sio kufanya kazi za kujiri mmoja mmoja ila kuwa na organized working team ambayo ni kampuni.

Nadhani kama wizara ya kazi na ajira kwa kushirikiana na wizara ya viwanda & biashara, kilimo, uvuvi, mifugo na madini kuna lots of organized jobs could be created ili vijana washinde in the course tax base inakuwa na tunapunguza imports na kuongeza exports.

Kama ni export za mahindi au korosho lazima zifanywe na makampuni. So vijana kama ni kuwa na cheti cha olevel na maarifa ya vocation kwenye kilimo, lazima iwe ni kilimo cha kibiashara na kinafanywa na kampuni lenye kulima hekta kadhaa, wanavuna kwa combined harvester wanaweza kuchakata na kuuza funal products.

Ukulima au ufugaji wa kutojua unamuuzia nani na kwa ubora gani, sio sehemu ya dunia yenye ushindani.

Kuna watu kujifichia tunatengeneza mifumo, yet hatuoni mifumo ikiwa na msaada kama watu hawafikiri "nje ya box".

JPM kama angeweza, kama jinsi alivyo na official TISS kama DSO, RSO na DG wa TISS, hawa wanafahamika, ila ana vijana ambao hawafahamiki who is who.

Aje na parrel system ya kufanya kazi hasa za kujenga uchumi, ili kama hawa known portfolio ministers wanashindwa kukimbizana na kazi yake, hawa vijana wa kitaa wampe how it takes to get there ili kuzalisha organized system za kujenga uchumi jumuishi na endelevu. Ofcourse ikifikia hatua ya mwisho ya ku-execute, hawa portfolio ministers watafanya kama wajibu wao.

Maana ugumu ni project/investment design hapo bila shaka wenye DNA ya kufikiri bila shaka tunao wachache.

Ukitaka kujua, sikiza radio, soma magazeti, tembelea social media na network few people speaks, writes and shares outbox innovations. Wengi bla bla na kusifiana na kukandiana pas kuonesha solution.

We got a lot to do kama mazingira yatajengwa ili hata hao wahitimu wa sekondari wenye kujengewa vocational training wawe functional kitaa wakimaliza shule.
 
Zingine ni za ufundi tayari.
Semea shule za kata.
 
ushauri wako ungezingatiwa tatizo la ajira lingekua historia kwa wahitim wengi.
 
Mi nadhani wangeongeza Technical schools ili wale wanaoamua kutoendelea na A. Level wasome technical schools watoke ma maujuzi yao
 
Nilidhani JPM atatoa maelekezo kwenye hili tuachane na mfumo wa kikoloni.
A:primary+ secondary school 7 years.

B:Kisha majengo sekondari olevel yote yawe Veta 70% ya A

C: A level waende 30% vipanga wa A

D: 10% ya C waende university

E: 20% ya C waende others diploma.

Tutapunguza tatizi la ajira na kuongeza tija nguvu kazi.
Kwasasa droplets wa mifumo yetu elimu 80% ni mizigo.
 
Wahitimu wa shule za sekondari/msingi iwe kwa yoyote ya certification kama hakuna mazingira ya kuwa-absorb baada ya masomo ya Carpentry, automotive, plumbing bado tunakuwa hatujafanya kazi ya kutosha.

Tusitafute quick fix kwa kudhani VETA au Technicians wa vyuo kama Mbeya Tech, Arusha Tech na Dar Tech kama zitarejeshwa kama kuongeza ufanisi wa hawa vijana kufanya miujiza.

Ni lazima Taifa lije na ubunifu wa kufanya liwalo na liwe ili kuzalisha kampuni za hawa wajuvi wa VETA wafanye kazi kama kampuni na sio in isolation.

Kwanini tuna garage za wachina wanaengeneza magari yetu mengi second hand na hatuwapi graduates wa VETA?

Ukienda SINO garage wana tools, equipment za kisasa na management system ya kuhudumia wateja.

Ilitakiwa VETA kwa kushirikiana na Brela na baadhi ya wahitimu wa vyuo vya biashara kujenga team ambayo inasailiwa kama kampuni. Then wanapewa mikopo ya equipment na all working tools na eneo la kujenga uzio ili kufanyia kazi magari yetu yakiharubika.

haina maana garage za waswahili ni chini ya miti na wana spanner chache, kwanini wasikopesheke chini ya usimamizi walimu wa VETA on how to start business, manage and scale up.

Sasa iwe ni plumbing, electrical au carpentry na serikali kupitia VETA wanawapa tenda walau kwa level ya kuwa sub-contract kwenye miradi ya serikali au wawekezaji wa private sector.

That is how we should build inclusive economy.

Ushuri wangu, ili mbegu iote na kuzaa matunda ni lazima kuwa na supportive system; temperate, oxygen na moisture.

Mbegu ikiota lazima ilindwe, imwagiliwe na kuwekewa mbolea ili kupata maximum production kutoka kwenye mbegu.

Nadhani wizara ya Ajira ina Waziri ambaye ka-focus kwenye kazi za kibunge na hana DNA na innovation kuzalisha ajira kwa vijana sio kufanya kazi za kujiri mmoja mmoja ila kuwa na organized working team ambayo ni kampuni.

Nadhani kama wizara ya kazi na ajira kwa kushirikiana na wizara ya viwanda & biashara, kilimo, uvuvi, mifugo na madini kuna lots of organized jobs could be created ili vijana washinde in the course tax base inakuwa na tunapunguza imports na kuongeza exports.

Kama ni export za mahindi au korosho lazima zifanywe na makampuni. So vijana kama ni kuwa na cheti cha olevel na maarifa ya vocation kwenye kilimo, lazima iwe ni kilimo cha kibiashara na kinafanywa na kampuni lenye kulima hekta kadhaa, wanavuna kwa combined harvester wanaweza kuchakata na kuuza funal products.

Ukulima au ufugaji wa kutojua unamuuzia nani na kwa ubora gani, sio sehemu ya dunia yenye ushindani.

Kuna watu kujifichia tunatengeneza mifumo, yet hatuoni mifumo ikiwa na msaada kama watu hawafikiri "nje ya box".

JPM kama angeweza, kama jinsi alivyo na official TISS kama DSO, RSO na DG wa TISS, hawa wanafahamika, ila ana vijana ambao hawafahamiki who is who.

Aje na parrel system ya kufanya kazi hasa za kujenga uchumi, ili kama hawa known portfolio ministers wanashindwa kukimbizana na kazi yake, hawa vijana wa kitaa wampe how it takes to get there ili kuzalisha organized system za kujenga uchumi jumuishi na endelevu. Ofcourse ikifikia hatua ya mwisho ya ku-execute, hawa portfolio ministers watafanya kama wajibu wao.

Maana ugumu ni project/investment design hapo bila shaka wenye DNA ya kufikiri bila shaka tunao wachache.

Ukitaka kujua, sikiza radio, soma magazeti, tembelea social media na network few people speaks, writes and shares outbox innovations. Wengi bla bla na kusifiana na kukandiana pas kuonesha solution.

We got a lot to do kama mazingira yatajengwa ili hata hao wahitimu wa sekondari wenye kujengewa vocational training wawe functional kitaa wakimaliza shule.

Nyerere alikufa na visions zake na hawa waliofuata walikuja na utitiri ambao wamekuwa wakipokezana wanachokiita kijiti,

Kwa wale tuliosoma enzi hizo leo hatuna shida na ufundi mdogo mdogo
ndani ya nyumba, kama ni kupika nikiingia jikoni ni zaidi ya masaptasapta na nikiingia shambani hawa wa leo wafanye kazi
 
Niliwahi ongea na baadhi ya wazee waliosoma zamani wakaniambia zamani walisoma shule za msingi zilizokuwa na masomo ya Ufundi zote(TRADE SCHOOLS).Wakitoka walikuwa wanaweza kujitegemea kwani walikuwa wanaweza fanya kazi kama za useremala nk

Ili mwanafunzi akitoka awe na uwezo wa kujitegemea nashauri katika mipango ya elimu shule zote za sekondari masomo yaliyoko VETA yawe sehemu ya masomo ya lazima mwanafuzi kusoma.Masomo yatakayoingizwa kwenye mitaala yawe yale yanayohusiana hasa na mazingira yetu yanayotuzunguka.Masomo yanayoweza kuwemo ni kama kilimo,ufugaji wa mifugo mbali mbali ikwemo ufugaji wa samaki,Upishi,utengenezaji bidhaa mbali mbali kutokana na vile tunavyozalisha nchini au malighafi zake nyingi ziwe zile za nchini.

Watoto wengi wamekuwa wakionekana kama hawapendi kilimo na ufundi sababu ni kuwa hawafundishwi mashuleni.Mtoto kazaliwa gorofani kakulia gorofani unategemea atapenda kilimo na ufugaji wakati saa zote anasoma vitabu tu vya tuition kutwa? Ndio maana lazima kama nchi iwasaidie masomo yawepo sekondary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Nimependekeza sekondary sababu walau watoto wanakuwa wakubwa kidogo ndio umri wa kufundishwa kujitegemea
Wasome umeme, useremala, uashi, makenika, uhunzi, uchomeleaji, ufundi rangi, kilimo, na mafunzo mengine eti ehhhh
 
Mawazo mufilisi....
Mtoto kuzaliwa ghorofani unateseka?....watu wamezaliwa ghorofani na wapo vizuri tu.
Peleka ujinga wako huko.
VETA ndio nini...
 
Kaka Tanzania bado tuna struggle na madawati makazi ya waalimu na stahiki zao.

Shule za kata zipo hoi...hazina waalim wa kutosha, maabala, vitabu nk

Kufanya shule hizo kuwa za ufundi utahitaji waalimu pamoja na karakana za kisasa...

Wazi lako zuri ila Serikali ya CCM labda ingeuza ile Dreamliner iliyopaki ikapata hizo 260billion ni kweli ingefanikisha mpango huu nchi nzima Kwa sasa sahau!! CCM hawataki maendeleo ya watu wao bali wamejikita kwenye maendeleo ya vitu.
 
Niliwahi ongea na baadhi ya wazee waliosoma zamani wakaniambia zamani walisoma shule za msingi zilizokuwa na masomo ya Ufundi zote(TRADE SCHOOLS).Wakitoka walikuwa wanaweza kujitegemea kwani walikuwa wanaweza fanya kazi kama za useremala nk

Ili mwanafunzi akitoka awe na uwezo wa kujitegemea nashauri katika mipango ya elimu shule zote za sekondari masomo yaliyoko VETA yawe sehemu ya masomo ya lazima mwanafuzi kusoma.Masomo yatakayoingizwa kwenye mitaala yawe yale yanayohusiana hasa na mazingira yetu yanayotuzunguka.Masomo yanayoweza kuwemo ni kama kilimo,ufugaji wa mifugo mbali mbali ikwemo ufugaji wa samaki,Upishi,utengenezaji bidhaa mbali mbali kutokana na vile tunavyozalisha nchini au malighafi zake nyingi ziwe zile za nchini.

Watoto wengi wamekuwa wakionekana kama hawapendi kilimo na ufundi sababu ni kuwa hawafundishwi mashuleni.Mtoto kazaliwa gorofani kakulia gorofani unategemea atapenda kilimo na ufugaji wakati saa zote anasoma vitabu tu vya tuition kutwa? Ndio maana lazima kama nchi iwasaidie masomo yawepo sekondary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Nimependekeza sekondary sababu walau watoto wanakuwa wakubwa kidogo ndio umri wa kufundishwa kujitegemea
Katoe ushauri kwenye chama mkuu, hapa itakuwa ni majungu....na vile Tz yote ni ya kijani, mawazo yako yatafanyiwa kazi!
 
Watoto wengi wamekuwa wakionekana kama hawapendi kilimo na ufundi sababu ni kuwa hawafundishwi mashuleni.Mtoto kazaliwa gorofani kakulia gorofani unategemea atapenda kilimo na ufugaji wakati saa zote anasoma vitabu tu vya tuition kutwa? Ndio maana lazima kama nchi iwasaidie masomo yawepo sekondary kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Nimependekeza sekondary sababu walau watoto wanakuwa wakubwa kidogo ndio umri wa kufundishwa kujitegemea
Nakubaliana na wewe lakini sio kivileeee. Kikubwa ni mazingira ya kufanya kazi na sehemu ya kuuza product yako. Mfano rahisi, kutokana na ukosefu wa ajira watanzania wengi wemejiongeza kwenye kilimo na ufugaji. Tatizo la soko ,na bei kuwa duni ambayo hailingani na gharama za uzalishaji zimefilisi wengi. Hali ya uchumi wa nchi ikiwa nzuri na mzunguko wa pesa niwa uhakika na usalama, automatically kila mtu ataji attach sehemu na watapiga pesa tu. Lakini hoja yako nikutaka kulazimisha watu wasome lakini hakuna maandalizi yoyote uraini.
 
Mtoa mada unadhani vijana wakiwa na skill za ufundi mchundo ndo watapata ajira? Je ni mafundi wangapi wako mtaani hawana kazi? Je ni watu wangapi wamesoma VETA na hawana kazi?

Je ni nani aliyeshindwa kufanya jambo lake kwa sababu hakuna mafundi?

Mimi nadhani jambo la kwanza ni kutengeneza opportunitiea. Opportunies kama zipo watu watajifunza na kuzichangamkia.
 
Back
Top Bottom