singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
JANUARI 13, mwaka huu, yapata siku tatu kuanzia leo, shule za msingi nchini kote zitafunguliwa huku mpango wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za serikali za msingi na sekondari ukianza kutumika.
Mfumo wa aina hii ulikuwepo miaka ya nyuma, hususani kipindi chote cha utawala wa rais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere kabla ya nchi kuingia kwenye mfumo wa kuchangia gharama.
Hatua hii ya kutoa elimu bure inafungua ukurasa mpya wa fursa ya elimu kwa wale wasio na uwezo na pia kunaondoa visingizio kwa wazazi na walezi vya kushindwa kupeleka watoto wao shuleni.
Hii ni hatua nzuri, ambayo kwa kila mpenda maendeleo, anapaswa kuipongeza serikali kwa kuamua jambo hili, ambalo limekuwa likipendekezwa mara kwa mara kutokana na changamoto za mfumo wa kuchangia gharama za elimu.
Kwa utaratibu huu ni matumaini ya serikali kwamba watoto wote wenye umri wa kuanza darasa la kwanza, wataandikishwa. Juzi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alizungumzia hatua zitakazochukuliwa na serikali kwa wazazi wote na walezi watakaoshindwa kupeleka watoto shule.
Alisema watawajibishwa kwa kupelekwa mahakamani kwa maana ya kwamba hakutakuwa na sababu ya mzazi kumnyima mwanawe elimu. Ni vyema basi wazazi na walezi mlio na watoto wanaostahili kwenda shule mkahakikisha mmewaandikisha ili wakapate elimu itakayowasaidia kwenye maisha yao ya baadaye na kuachana na tabia ya kuwatumikisha kazi za nyumbani.
Wapo baadhi ya walezi na hata wazazi ambao kwa makusudi wanawashurutisha watoto wao wasifanye vizuri kwenye masomo yao, ili wasifaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari, kwa lengo la kuwatafutia kazi au kuolewa, jambo ambalo limewafanya watoto hao kuwa watumwa.
Ni vyema wazazi wakatambua kwamba watoto wana haki ya kusoma. Wanatakiwa pia wafuatilie maendeleo yao shuleni na kuwa na ushirikiano na walimu ili kuhakikisha watoto hao wanahudhuria masomo, na kupata mrejesho wao.
Tukumbuke kwamba, nchi zote zilizoendelea zimewekeza kwenye elimu na hivyo kila anayependa maendeleo ni wajibu kuhakikisha elimu kwa watoto wake inakuwa ni jambo la kwanza.
Kumuelimisha mtoto haimaanishi kumpa maisha mazuri yeye pekee, bali ni njia mwafaka ya kupata wataalamu mbalimbali nchini. Kwa msingi huo basi, shule zinapofunguliwa hiyo Januari 13, ni wajibu wa wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa walimu na kuhakikisha watoto wanasoma badala ya kuwaacha wazurure mitaani na kujiingiza kwenye makundi mabaya, yatakayoharibu maisha yao.
Ikumbukwe kwamba mwaka huu, mwitikio wa wazazi na walezi kuandikisha watoto kuanza elimu ya msingi ni mkubwa hivyo ni vyema hilo likaendelezwa kwa wazazi hao kufuatilia mienendo yao ili kuhakikisha wanamaliza masomo yao kwa tija.
Kuna baadhi ya wazazi na walezi ambao wamekuwa wakiwatumikisha watoto wao au wa ndugu zao kama mtaji wa kupata fedha, kwa kuwatafutia kazi kwa waajiri mbalimbali ambao huwatumikisha kinyume na sheria tena kwa ujira mdogo.
Watanzania tuamke, na sote tushikamane kwenye suala la elimu kwa watoto kwa sababu watoto waliokosa elimu tumewaona kwenye mitaa mbalimbali wakiwa katika makundi mabaya, na wakati mwingine, wanawageuka hata wazazi wao na kuwadhuru.
Serikali imeongeza fursa ya mtoto kusoma hivyo ni wajibu wetu wananchi kutumia fursa hiyo kuhakikisha watoto wanaelimika kwa manufaa yao, familia zao na kwa taifa. Pia ni vyema tukatoa ushirikiano kwa serikali na mamlaka zake kwa kutoa taarifa pale wazazi au walezi wanapowanyima watoto wao haki ya elimu, kwani tusipowafichua unyanyasaji kwa watoto hautaisha.