Shule Zetu za Kidato cha Tano na cha Sita ziwe.....

SolarPower

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
223
27
Wakuu,

Napendekeza shule zetu za kidato cha tano na cha sita kila moja iwe na combination moja tu. Maana yangu ni kuwa kama shule ni ya PCM basi wanafunzi wote katika shule husika wanasoma PCM. Hii itatusaidia kuwa na shule maalum kwa kila combination.

Nawasilisha.
 
Hiyo ni ngumu sana! Jaribu kufikiria waalimu, vitabu, majengo, maabara, muingiliano wa combination n.k. Je vitendea kazi vitakuwepo?
 
Yaani kila A-level iwe na combination moja tu ni ngumu sana.Imagine enzi zile za Mkwawa High School wewe ungepata wapi wanafunzi wa kujaza shule ile yote kwa combination moja
 
wakuu,

napendekeza shule zetu za kidato cha tano na cha sita kila moja iwe na combination moja tu. Maana yangu ni kuwa kama shule ni ya pcm basi wanafunzi wote katika shule husika wanasoma pcm. Hii itatusaidia kuwa na shule maalum kwa kila combination.

Nawasilisha.
uwezo mdogo wa kufikiri 1.5 kb
 
Wakuu,

Msiogope mawazo mapya. Hili linawezekana ni suala la uamuzi la kusimamia utekelezaji wake. Kama unaweza kuwa na wanafunzi say 100 wa PCM kwenye shule zaidi ya 10 kwa kila shule kuwa na wanafunzi 100 wa PCM kwa nini ushindwe kuwa na wanafunzi 600 wa PCM kwenye shule moja.

Suala la Walimu Vitabu na Maabara sioni kama ni tatizo. Ni suala la kupanga na kutekeleza kwa ufanisi kile kilichopangwa.
 
Hiyo ni ngumu sana! Jaribu kufikiria waalimu, vitabu, majengo, maabara, muingiliano wa combination n.k. Je vitendea kazi vitakuwepo?

Mkuu Kimbori asante kwa maswali yako ila naomba nikwambie kuwa nchi hii tatizo letu ni kuwa hatuna dhamira ya dhati ya kutoa elimu bora kwa vijana wetu. Rasimali si tatizo hata kidogo. Kwa mfano bajeti ya BUNGE ni zaidi ya Sh bilioni 83 kwa mwaka wakati fedha ya kuendesha shule zote za sekondari na msingi, zaidi ya shule 19,000 zenye zaidi ya mwanafunzi milioni 9.8, inayotolewa na serikali kwa mwaka hafiki shilingi bilioni 26. Pia usisahau kuwa bajeti ya Benki Kuu kwa Mwaka mmoja tu ni zaidi ya shilingi bilioni 570.
 
uwezo mdogo wa kufikiri 1.5 kb
Uwezo mdogo wa kufikiri kutoka kwako au kwa aliyeanzisha thread...kumponda mtu bila kutoa hoja mbadala ni kuanika utupu wa bongo wako.Acha uzembe na uvivu toa hoja zako sio tu kumtukana mwenzako bila kuelezea sababu.
 
Back
Top Bottom