Shule zakutwa na mabweni kama magofu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,735
2,000
Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu, kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera, wamezifungia shule mbili za msingi ambazo ni Kido na Talent kutoa huduma ya bweni, kutokana na majengo yanayotumika kuwalaza wanafunzi kuwa na hali mbaya isiyofaa kutoa huduma hiyo.

Shule hizo mbili za msingi ambazo usajili wake ni wa kutwa lakini zimebainika kulaza watoto kimya kimya, zimegundulika katika ukaguzi uliofanywa na jeshi la zimamoto na uokoaji kuanzia Februari 05 hadi 23 mwaka huu, unaolenga kubaini kama wamiliki na wasimamizi wa shule wanazingatia kinga ya ajali za moto katika shule.

Akizungumza baada ya ukaguzi huo Kaimu Mkuu wa jeshi hilo mkoa wa Kagera, Mkaguzi Thomas Majuto, amesema kuwa katika ukaguzi huo baadhi ya shule walikuta zina mapungufu kidogo yanayoweza kurekebishika, lakini nyingine zimekutwa miundombinu yake imeharibika na haifai kulaza wanafunzi.

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu, amewataka wamiliki na wasimamizi wa shule zilizokaguliwa na kubainika kuwa na mapungufu ikiwamo kutokuwa na ving'amua moto na vizimia moto, kutakiwa kubadilisha milango na kuweka milango ya dharura kwa mabweni yenye mlango mmoja, kufanya marebisho hayo katika muda waliopewa, vinginevyo watachukuliwa hatua zaidi.

1615207221469.png
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,602

View attachment 1720185
Hii mbona nzuri, kuina shule hazina madirisha,milango, sakafu, lipu nk.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,596
2,000
Mtoto wa shule ya msingi anapelekwa boarding school kufanya nini? wazazi wengine nao bora wangefungwa vizazi na serikali.
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,657
2,000
Duuuuuuhhh. Mzazi alifanya utafiti kujua kitanda anacholalia mwanae shule?
Hizi shule haziruhusu wazazi mabwenini, 90% ya hizi shule za boarding hata za O na A level haziruhusu wazazi kuzuru mabweni, mzazi mwisho ofisini, sababu ni hizo facilities nyingi ni kama mabanda.

Labda kama ni International kweli.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom