Msulibasi
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 5,957
- 8,005
Ndugu wanabodi,
Baada ya serekali kutangaza kufunga shule zote za msingi na sekondari , Uongozi wa shule za Tusiime ulitangaza kuathirika kiuchumi hivyo kushindwa kulipa mishahara ya watumishi kwa shule zake za msingi na sekondari zilizopo Tabata Saanene..
Watumishi wakiwemo wapishi , madereva ,waalimu na matrons walipewa likizo bila malipo iliyoanza tarehe moja April hadi 29 June shule zilipofunguliwa.
Chakusikitisha baada ya watumishi kuripoti kazini walikumbana na barua za kusitishiwa mikataba yao ya ajira na hawakupewa stahiki zao ikiwemo mishahara ya Aprili , May na June.
Zoezi la kuondoa wafanyakazi limeendelea kushamiri toka hiyo June hadi sasa. Watumishi wengi wamepeleka madai mahakama ya kazi na wengine wameamua kunyamaza baada ya kupatiwa kiasi kidogo cha fedha.
Swali langu ni je ?Iweje Tusiime pekee ndio iathiriwe na Korona kwa haraka kiasi hicho hata kushindwa kulipa japo robo mshahara kwa miezi mitatu.
Iweje hata baada ya kufungua shule watumishi wasipewe japo nauli ya kuendea kazini mpaka waombe advance ya mshahara wa mwezi wa saba.
Hivi Tusiime inawezaje kufanya vurugu za kiwango hichi katikati ya jiji la Dar es Salaam na kuachwa kama kisiki?
Je, Serikali imepata kodi yake ya Aprili , May na June?
NSSF wamekusanya mafao ya Aprili May na June kutoka Tusiime?
Bodi ya mikopo je ?/mmepata 15% yenu?
Haki ya wanafunzi kupata huduma bora kutoka kwa watumishi kwenye uwiano sawa na wanafunzi inazingatiwa? Ni wajibu wa serekali yetu tukufu kumulika na kuondosha ubabe huu wa Tusiime . Patrobas Katambi anzia Tusiime.