Shule za Msingi Temeke yasemekana nafasi zimejaaa

Shule za Msingi Temeke yasemekana nafasi zimejaaa

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Posts
4,873
Reaction score
1,221
Habari za kuamka wanajamvi?

Leo katika pita pita zangu asubuh hii hasa maeneo ya TEmeke,kata za keko magurumbasi,keko machungwa,Tandika,kumekua na malalamiko katika uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa mwaka wa masomo unaonza mwakani,ambao Mh Rais Pombe J Magufuli kuwa Elimu hiyo itakua bure,wakuu wa shule hizo wamekua wakiwambia kuwa Nafasi zimejaa,lakini kwa Mgongo wa Elfu Arobaini unatoa unapata Nafasi ya mwanao.

Natoa. Angalizo serikali jambo hili isilipuuzie kabisa yawezekana lipo kabisa,kikubwa Wakurugenzi waweke sanduku la Maoni katika shule zote na Sanduku hilo na Maoni hayo yachukuliwe na wasaidizi wake ili ajionee hali halisi ya Uandikishaji.
 
Aisee........kumekucha.........
 
Wazungu walianza na sifuri miaka ya 1900 mpaka 1961 yaani miaka 60 baadae walikuwa wameanza kupata mwelekeo. Kuanzia 1961 Mwalimu alitaka kujenga aina fulani ya nchi na kufikia miaka ya katikati ya sabini alikuwa keshaanza kupata mwelekeo pia. Cha kusikitisha baada ya Mwalimu either bila ya kujua tukafuta kila alichokusudia kufanya lakini hata tulivyovifanya Dr. Magufuli kalibia anavionyesha kuwa na kasoro na anataka kuvirekebisha!

Nini maana hi hizi hadithi, ni kwamba tunaanza kama vile ndio mwaka 1961 kupambana na matatizo ya Watanzania. Tofauti ni kwamba mwaka 61 nchi ilikuwa na watu milioni 9 leo tuna watu millioni 50+
Mwaka 1961 tulikuwa na watu wasiosoma lakiniwanategemea busara kufanya mambo yao leo hii tuna idadi kubwa ya watu waliokuwa brainwashed wakiwa na vyeti huku wakikosa hata kiwango cha chini kabisa cha busara.

Kwa hiyo tunavyoongelea standard ya darasa kuwa na wanafunzi -40 kwa mwalimu mmoja utaweza kukubaliana na hawa walimu wa shule hii!?
#hapakazitu
 
Nafasi zipo vyumba na madawati vimejaa.Elimu ina changamoto sana hasa katika kata za watu wa kipato cha chini ambapo watoto wengi wanasoma government schools.
 
Hapa kazi tu ,wakati mtu hana kazi.ukshangaa ya kiwete utayaona ya haambiliki a k a komeo
 
Ni leo Jumamosi au wiki hii umeshuhudia wanaomba hiyo rushwa?

Andika zaidi ili mambo yasomwe na kufatiliwa.
 
Huku mtaani kwetu manispaa Ilala kuliitishwa kikao cha wazizi wakiambiwa shughuli zimekwama zinazohusisha michango ya wanafunzi. Wazazi wamegoma kutoa wakidai magufuli kasema elimu bure. Mwl. Mkuu anasema haki bin haki itafuatwa, kwamba mtoto akizidi au kupungua miaka 7 hakuna kuandikishwa, pia inabidi ajue kusoma vizuri na kuandika.
Mtoa maada yupo sahihi.
 
Back
Top Bottom