Shule za kata zapata vifaa vya maabara, JWTZ yapewa kazi ya kuvisambaza nchini.

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imepokea vifaa vya maabara ya masomo ya Fizikia, Kemia na Baolojia vyenye thamani ya Sh bilioni 16.9 kwa ajili ya shule za sekondari nchini.

Vifaa hivyo vimetolewa na Kampuni ya Lab Equip Ltd ambayo ni miongoni mwa wazabuni watano walioshinda kusambaza vifaa hivyo kwa kanda 11 ambazo ni Kanda ya Kaskazini Mashariki na Kanda ya Kaskazini Magharibi.

Nyingine ni Kanda za Magharibi, Kati, Kusini, Ziwa, Nyanda za Juu, Dar es Salaam, Mashariki, Ziwa Magharibi na Nyanda za Juu Kusini.

Akipokea msaada huo Dar es Salaam, Kaimu Kamishna wa Elimu wizarani hapo, Nicolas Buretta alisema vifaa hivyo vitasambazwa kwa shule za sekondari 1,696 nchini, kati ya hizo, shule 1,625 ni za kata na shule 71 ni shule kongwe za Serikali.

Alisema vitasambazwa katika shule zilizokamilisha ujenzi wa vyumba vya maabara na kwamba, hiyo ni changamoto kwa shule ambazo hazijakamilisha majengo yao ili zikamilishe.

Kaimu Kamishna huyo alisema vifaa hivyo vitasambazwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), na kwamba kazi hiyo ya usambazaji itakamilika mwishoni mwa mwezi huu.

“Vifaa hivi vitaleta matokeo chanya katika masomo ya sayansi. Ujifunzaji wa vitendo utainua ari kwa wanafunzi katika kujifunza. Italifanya taifa kuwa na wataalam wa kutosha kwa kuwa hatutakuwa na changamoto ya vifaa,” alisema.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya Lab Equip Ltd, Hassan Raza aliishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na timu yake kwa kuwaamini.

Wakati huo huo serikali inatoa ajira kwa walimu 3,104 wenye fani ya sayansi huku akiendelea kusaka walimu wengine 46,382 wenye fani ya sayansi ili kukidhi mahitaji katika masomo ya sayansi nchini.

VIDEO:
 
Ni jambo jema kabisa na la kupongeza na hii habari ilitangazwa jana usiku katika taarifa ya habari ya ITV au Channel Ten ila nilichojiuliza hiyo tender ya kuingiza hivyo vifaa kutoka nje ilitangazwa?

Nilijuliza hili swali baada ya kuona ni kampuni binafsi ndio imeingiza hivi vifaa kutoka nje ya nchi(kampuni ya wageni).4
 
Ni jambo jema na la kupongeza na hii habari ilitangazwa jana usiku katika taarifa ya habari ya ITV au Channel ila nilichojiuliza hiyo tender ya kuingiza hivyo vifaa kutoka nje na kuvisambaza hapa nchini ilitangazwa?
''Vifaa hivyo vimetolewa na Kampuni ya Lab Equip Ltd ambayo ni miongoni mwa wazabuni watano walioshinda kusambaza vifaa hivyo kwa kanda 11 ambazo ni Kanda ya Kaskazini Mashariki na Kanda ya Kaskazini Magharibi''.
 
''Vifaa hivyo vimetolewa na Kampuni ya Lab Equip Ltd ambayo ni miongoni mwa wazabuni watano walioshinda kusambaza vifaa hivyo kwa kanda 11 ambazo ni Kanda ya Kaskazini Mashariki na Kanda ya Kaskazini Magharibi''.
Jana nilipokuwa naangalia hiyo taarifa niliikuta katikati sikujua kumbe ni msaada mimi nilifikiri ni serikali imenunua.
 
Pongezi kwa Serikali.

Ila Natoa ushauri....

Morali ya waalimu Je?

Walimu walipe madeni yao...

Vinginevyo hata kubalance equation itakuwa fyongo...atafundisha tu ili mradi amemalize kipindi

Tumejali sana Maendeleo ya Vitu....ufahari wa vitu ili Utu wa watu wa Tanzania tumesahau
 
Ni muda muafaka sasa maslahi ya walimu kuthaminiwa.....Hata kama shule inakila kitu, kama mwalimu maisha yake ni ya kuungauunga ni kazi bure.
 
Tumpongeze tu lakini hizi sio dalili nzuri sana... Leo jeshi linapewa kazi Kama hiyo huwezi jua kesho na keshokutwa watapewa hukumu gani
Mkuu;
Kwa nini unasema hivyo?

Kama kutumiwa kwa mambo mengine ''mabaya'' wanaweza tu kutumiwa kwa sababu moja ya nidhamu ya jeshi ni kukubali kwanza amri halafu maswali baadaye.

Serikali imetumia JWTZ ili kusaidia kubana matumizi.
 
Back
Top Bottom