Shule za kata ndio, umoja wa kitaifa je?

Shule za kata ndio, umoja wa kitaifa je?

Umoja wa Kitaifa hauko hatarini kutoweka?

  • Umoja wa Kitaifa hauko hatarini kutoweka?

    Votes: 0 0.0%
  • Umoja wa Kitaifa hauko hatarini kutoweka?

    Votes: 0 0.0%
  • Umoja wa Kitaifa hauko hatarini kutoweka?

    Votes: 0 0.0%
  • Umoja wa Kitaifa hauko hatarini kutoweka?

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    0

SAMUNGE TZ

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
254
Reaction score
23
:fish2:Kwa sababu ya uchache wa shule za sekondari nchini na kwa sababu ya kudumisha umoja wa kitaifa baada ya uhuru, serikali ya Tanganyika iliamua kwa dhati kabisa kila mwanafunzi anayefaulu kwenda kidato cha kwanza mathalan kutoka kaskazini ni budi akasome kanda ya kati na kutoka kanda ya ziwa magharibi ni budi akasome kaskazini au mashariki n.k. na warrant yake mkononi.Hii ilikuwa njia moja ya kudumisha umoja wa kitaifa lakini kwa sasa hali ni tofauti kabisa.Unasoma shule Dar unamalizia kila kitu,unasoma Kilimanjaro unamalizia huko kila kitu,unasoma Kagera unamalizia huko masomo yako yote hadi chuo kikuu.Pamoja na kuwa ni mafanikio lakini je kesho ukimwambia kijana kuwa Mtwara kuna wamakonde wa Msumbiji na Tz,Mara kuna Wajaluo wa Kenya na Tz au Tz kuna Wamaasai na Kenya atakuelewa?

Je hatujengi misingi ya kikabila na kikanda ambayo waasisi wa taifa hili alifanikiwa kuiondoa kwa kiwango kikubwa?

Leo hii serikali ikipeleka mtumishi kufanya kazi ktk halmashauri fulani unasikia wenyeji wana pinga[mkurungenzi wa halmashauri],mamlaka za uteuzi mathalani wakiteua mkurugenzi kwenda kuhudumu kwenye taasisi fulani ya umma wenyeji wanaandamana kumkataa hadi apelekwe wa kwao[mamlaka ya Ngorongoro].

Wanajf toa hapa ushauri namna bora ya kutatua changamoto hii kabla haijaleta madhara nchini mwetu maana hatuna nchi nyingine ya kuishi zaidi ya Tanzania.:help:
 
Naunga mkono hoja mkuu, uamuzi wa kuanzisha shule za kata ni janga....Ni uamuzi wa hatari kwa umoja na ustawi wa taifa letu.
Uwepo wa shule za kata ndio umeleta mserereko mkubwa wa sekta ya elimu nchini, ndio umezalisha idadi kubwa ya vijana wasio na elimu licha ya kwamba wamekaa shuleni miaka 4.
 
How can I give my poll while the a,b,c,d is the same?
 
Naunga mkono hoja kweli ili ni janga la kuleta ukabila ktl nchi hii ya Tanganyika
 
Back
Top Bottom