Shule za Feza wanatumia mitaala ipi hapa Tanzania?

nation

Member
Jan 11, 2017
54
40
Mara nyingi nilikuwa nafuatilia sana matokeo ya mitihani za shule za Feza sekondari kila matokeo yakitangazwa unakuta wameshika kumi bora kitaifa.

Sasa kwa hili hawa wanatumia mitaala gani hapa Tanzania, mbona shule zetu za kata zinanyonga tai kila matokeo yakitangazwa. Sijawahi kuona na kusikia ipo kwenye kumi bora.

Jamani mnisaidie wanatumia mitaala gani hapa Tanzania ili hata wadogo zetu wafaulu kama wa Feza secondari.
 
labda watusaidie walimu wanaofundisha feza sekondari wanafanyafanyaje mpaka kufaulisha kiasi hicho.kama wapo humu watusaidie
 
feza wanasoma elite students
kabla ya kuingia unafanya interview ukipata daraja la juu unakubaliwa kujiunga

mfano A level hata kama ulipata division 1 o level lazima ufanye paper yao ukipata A's unajiunga na wale special students wanasomeshwa bure

1.walimu wazuri
2.wanafunzi wanajielewa/wanapenda kusoma
3.wanafunzi elites

hiyo ndio sifa pekee
 
wanatumia mitaala ya kawaida sema namna notice wanavyoziandaa wanapangilia vzr sana, me nilipata material yao advance sikuhangaika na wakina nyambari nyangwine maana wao sehemu yenye point 4 wanalazimisha ziwe 7
 
Sifa ya kwanza kujiunga na shule za Feza ni kujua hesabu, masomo mengine kipaumbele ni kidogo, bila hesabu Feza hawakuchukui
 
iko hivi...siri ya kufaulu ni kujaza majibu mengi sahihi kwenye mtihani..so feza wana hakikisha wanafundisha topics zote ..na pia wanafunzi wanapewa mitihani ya kutosha kupima uelewa...wanafunzi wanapewa test nyingi zinazowaandaa na kuwaweka fiti hata wakiingia kwenye mtihani wa taifa wanakua wana confidence coz wanakua washasoma kila kitu...
 
wanatumia mitaala ya kawaida sema namna notice wanavyoziandaa wanapangilia vzr sana, me nilipata material yao advance sikuhangaika na wakina nyambari nyangwine maana wao sehemu yenye point 4 wanalazimisha ziwe 7
Nisaidie kijana ili umpe binti yangu yuko form five
 
Mbona huulizi shule kama st Francis, Marian etc. Shule zote zinazoongoza kitaifa ama kuwa na matokeo mazuri inzsaidiwa na
-mazingira mazuri/rafiki ya kujifunza kama vitabu, Maabara etc
-walimu wazuri na wanaojituma katika kazi zao
-kuna mchujo kutoka darasa moja kwenda mwingine, kwa student ambaye hatafikisha wastan uliowekwa either arudie darasa ama ahame shule
-kuna mitihan ya ndan ya shule ya kujipima uwezo ya kutosha
- wanafunz kiandaliwa vzr na kujitambua wako shule kwa ajili ya nn
 
Mara nyingi nilikuwa nafuatilia sana matokeo ya mitihani za shule za Feza sekondari kila matokeo yakitangazwa unakuta wameshika kumi bora kitaifa.

Sasa kwa hili hawa wanatumia mitaala gani hapa Tanzania, mbona shule zetu za kata zinanyonga tai kila matokeo yakitangazwa. Sijawahi kuona na kusikia ipo kwenye kumi bora.

Jamani mnisaidie wanatumia mitaala gani hapa Tanzania ili hata wadogo zetu wafaulu kama wa Feza secondari.
Hongera sana umeuliza swali zuri sana, lau tungekuwa na maswali kama haya katika kila sekta kuangalia watu waliofanya vyema walifanyaje, kama nchi zinazofanya vyema zinafanyaje kwenye sekta hizo tungekuwa mbali sana.

Feza wanafanya vyemabkwa sababu zifuatazo:-

1. Ada kubwa - hili jambo wengi hawata lielewa lakini ada kubwa inawafanya wazazi waone uchungu pesa zao wanazozitoa hivyo hawawezi kufanya uzembe kuwaachia watoto wao wacheze viduku huku mamilioni yanateketea. Kayumba ukienda sawa usiende sawa, mzazi hana uchungi kwani hana anachopoteza, walimu ndo kabisa hawana wanacho gain, hawajisumbui.

2. Hawafuati mtaala kwa ukamilifu - hapa namaanisha wao wanajiongeza. Mitaala ya masomo mengi kama sio yote iko hovyo kuliko hovyo yenyewe. Kama kuna walimu wa English humu pitieni mtaala wa english muangalie madudu. Mada zinazo muwezesha mtoto kuunda maneno na sentensi zimetikewa mwanafunzi hasomi syntax, semantics, word formation, phonology. Sasa walimu wengi wanafuata hizo syllabus za hovyo pepa ikija hivyo visivyokuwepo kwenye mtaala vyote unavikuta - unazungusha zero grazing.

3. Walimu wazoefu - feza haikusanyi makapi tu kisa unavyeti hapana, wanatafuta walimu waziefu na wenye ujuzi kidogo ili kumudu changamoto za wanafunzi vipanga. Sio mchezo ni mchakamchaka hasa. Vilaza hawamalizi mwaka wanasepa.

4. Huduma bora kabisa. Kuna baadhi ya vyuo na hostel hazifikii hadhi ya majengo ya feza hata robo. Ukiingia getini unaona kabisa hapa kuna shule, sio kama umeingia ukonga au keko. Watoto wanasoma mazingira safi, madarasa safi, mabweni kama ulaya, dining ndo acha kabisa. Psychologically watoto wanafeel to be there. Hakuna mtoto anayesema baba mm sipataki feza kuna kunguni.

Mengine ni siri - siwezi kuyaweka wazi hapa kwani ndio mbinu zinazowafanya wawe walivyo, chukueni hayo machache mkajaribu bahati zenu.
 
Back
Top Bottom