Anonymous
Senior Member
- Feb 3, 2006
- 125
- 321
Wakati mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo katika Mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro,Edward Shayo akiwa mahabusu ya Gereza Kuu la Mkoa la Karanga akishitakiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa shule yake,Humphrey Makundi,kashfa nyingine imeikumba shule hiyo.
Safari hii shule hiyo imeingia katika kashfa ya kuajiri walimu sita kutoka nchi za Kenya na Uganda ambao hawana vibali vya kufanyakazi nchini lakini ikapigwa 'deal' kati ya Wakili wa Serikali Bw,Chavula na Afisa wa Uhasmiaji ili wasifikishwe mahakamani na badala yake watozwe tu faini ya dola 600 kila mmoja.
Katika makubaliano hayo yanayodaiwa kumshirikisha Wakili mwingine wa Serikali aitwaye Kibwana ambaye imebainika naye si raia wa Tanzania,ilishauriwa Idara ya Uhamiaji isimshitaki mmiliki wa shule hiyo Edward Shayo kwa kuajiri wageni bali alimwe tu barua ya onyo.
"Sisi maofisa wa chini wa Idara ya Uhamiaji tunasikitishwa sana na double standard hii na hapa ofisini kwetu kuna jalada la uchunguzi juu ya uraia wa bwana Kibwana",wamelalamika baadhi ya maoiisa wa uhamiaji ofisi kuu mjini moshi.
Haya yanatokea wakati vijana zaidi ya 800,000 wanahitimu vyuo mbali mbali na kuingia kwenye soko la ajira wakiwamo walimu,lakini hawapati ajira kutokana na kazi zinazopaswa kufanywa na watanzania kuchukuliwa na raia wa kigeni kama kazi ya kufundisha.