Shule ya Sekondari Mtwango yaanza kuchukuliwa kiudhalimu

Shule ya Sekondari Mtwango yaanza kuchukuliwa kiudhalimu

Mdomomrefu

Member
Joined
Jan 26, 2022
Posts
19
Reaction score
17
Habari watanzania wenzangu, poleni na mahangaiko ya dunia hii.

Mnamo trh 12.8.2021 Afisa wa elimu Wilaya ya Njombe Vijijini ndugu Mbwana Ndumbalu alifika shuleni Mtwango sekondari huku akiongozana na chombo cha dola, alifika na kudai kuwa shule imeshindwa kujiendesha bila ya watumishi hao kukubali kuwa wameshindwa kuiendesha hivyo alidai kuwa inachukuliwa na Serikali.

Kisha watumishi wakakubali lakini walihoji kuhusu haki zao. Afisa huyo alidai kuwa deni lote litalipwa na pia akaenda NSSF pia akasema wasiendelee kudai shule kwa kuwa deni lote litalipwa na Serikali. Kisha wakakubaliana kuwa mwisho ilikuwa ni Desemba.

Afisa huyo wa elimu alikwenda kwa commissioner na kusajili upya Shule kama ni ya Serikali na inadaiwa commissioner huyo ni baba yake mdogo. Na ilipofika Desemba walifunga shule bila ya uwepo wa Afisa huyo.

Januari watumishi hao wameendelea na hali ya sitofahamu huku Afisa huyo akimtumia academic master aliyesaliti wenzie akidai kuwa wanapaswa kuendelea hadi mwezi wa sita. Huku Afisa huyo akijua kuwa atastaafu mwezi wa tatu so kikombe atakikwepa.

Mimi binafsi nimeaona nilifikishe hapa JamiiForums kuutarifu umma kuwa shule inataka kuchukuliwa kiudhurumati bila ya hata Serikali kuu kujua.

Asanteni Sana kwa mda wenu
 
Habari watanzania wenzangu, poleni na mahangaiko ya dunia hii.

Mnamo trh 12.8.2021 Afisa wa elimu Wilaya ya Njombe Vijijini ndugu Mbwana Ndumbalu alifika shuleni Mtwango sekondari huku akiongozana na chombo cha dola, alifika na kudai kuwa shule imeshindwa kujiendesha bila ya watumishi hao kukubali kuwa wameshindwa kuiendesha hivyo alidai kuwa inachukuliwa na Serikali...
Hapo si ndio alisoma Greyson Msigwa?
 
Hata kama wewe ni Mdomomrefu! au una Mdomomrefu , lakini bado ulitakiwa uilete hii taarifa kwa usahihi na utulivu mkubwa.

Kiukweli umeileta ukiwa una haraka sana. Tulia, relax! Lete taarifa kamili. Maana kuna jamaa yangu alipitia hapo miaka mingi iliyopita, na wakati inafanya vizuri. Alikuwa anaisifia sana hiyo shule.
Sawa mkuu
 
Nilipita pale miaka kadhaa kidato Cha tano kwa muda mfup kabla sijapata second selection shule ya serikali hapa jijin dsm

Kiukweli shule ile kwa wakat ule ilikuwa na wanafunz weng Sana na wengi wao walioshindwa shule nyingne huko kwa kufukuzwa

Wanafunz walikuwa watukutu Sana wavuta bangi

Namkumbuka mkuu wa shule aliitwa Mr mbunda walimu Kama akina kisoso wihala mbunda d

Mahusihano ya walimu na wanafunz kimapenz liliiuwa Jambo la kawaida Sana

Nadhan NDDT walishindwa kuendesha shule hii

Zama hizi kuendesha shule ya private inabid ifanye vzur Sana kuvutia wanafunz maana shule za kata n nyingi Sana watoto wanaofel std 7 n wachache Sana

Asee huko ulanz n mwing Sana mitaa ya lihalamu

Mm nilipita nyakat za mauaji ya mwanafunz maenzetu aliuawawa na wanakijiji walipoenda kula mitungi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Zama za Mr mbunda zilikwisha alishindwa kuendesha shule. Kijiti alipokea Mbunda D tangu 2013
 
Back
Top Bottom