Dah kweli umenikumbusha mbali sana. Gwasa bwana na mbwembwe zake na kale kamwili kamekomaa utafikiri Remires wa Chelsea..ha ha ha. Mama Manyama nae alikuwa anachukia sana wasichana wazuri au tudume tulitwoonekana mbegu, na shoto lake lahaula..!!
Kweli kabisa inaelekea ni miaka hiyo hiyo mkuu. Mimi nilikuwa Maiko Jodan wa enzi hizo 🙂 piga sana ball pale ktk uwanja ule uliokuwa katikati wa zege !! Pia yale mambo ya disko na yule DJ Bulushi (maiko jackson wa Mbeya, na push back lake la nguvu na don't touch dah...ama kweli vya kale dhahabu (demu wa DJ alikuwa anasoma pale mbele yetu, Hellen ? Enzi za mtemi wa mujini Biso na trupu zima la Sangu sec... !! Sisi tulikuwa pia tunakipiga sana kiputa pale na mara kadhaa tulizichapa sana na Iyunga na Meta !!
Nisajile alikuwa balaa, moto wa kuotea mbali na fegi zake 24/7
Hawa akina mulugo ndo walikuwa hawalali usiku, wanasomea miguu ikiwa ktk mabeseni na kwenda kuiba chapati kwa wamama wa jirani, nyumba za FFU ??