Nursery school na Standard 1- No. 6. Gari la baba na mama. Mama ndio alikuwa anatupeleka na siblings.
Std 2- No. 4 kwa miguu mwanzoni as saa ya kwenda shule ilichange from morning to afternoon, baadae kaka yangu akani-offer kunipeleka na kunichukua kwa baiskeli (nivyoanza kwenda kwa miguu nilikuwa naona mbaaaaali, majuzi nikaenda nikachukua Taxi nikamwambia Taxi driver anipeleke tulipokuwa tunaishi halafu shule ya msingi niliyosoma Dodoma- nikambishia nikasema sio hapa penyewe palikuwa mbaaaali japo niliona majengo ni copy right. akasema hii ndio shule yenye jina hili hapa Dodoma- ha ha ha , kumbe ule umbali niliouona ilikuwa utoto tu wala sio mbali kihiiiivyo).
Std 4 - 7 no. 4 kwa mguu, shule ilikuwa kariiibu. Form 1 -number 6 mpaka nilivyozoea form 2 to 4- number 3 kwa UDA. Form 5 &6 nilikuwa Hostel ilikuwa raha saaana, tunatoka hosteli kwenda darasani.
Jamani nimekumbuka mbali, enzi zile UDA zilikuwa kwa Time. Kituo chetu likuwa 12. kamili( Yaani form one ndio ilikuwa basi letu/ lao), 12.30 mhh maform 2 na kuendelea. Baadae UDA ikaelemewa marehemu Sokoine akamshauri Mwalimu Nyerere ili kuboresha usafiri lazima kuingiza Private sector. ( sio viongozi wengine kila anachosema Mkuu wake , ndio Mzee)On another note, Hebu Mwaibula Mwingine aibuke ili kuboresha zaidi usafiri wa DSM ukisupotiwa na mabasi ya mwendo kasi!