Shule ya JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule ya JK

Discussion in 'Jamii Photos' started by MaxShimba, Aug 15, 2011.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [FONT=d742ee695d1fc2180a36a1f8#200e00]Serikali Yaazimia Kuifanyia Marekebisho Mitaala Ya Elimu Ya Msingi Na Sekondari[/FONT]Posted by Mjengwa |

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  <TBODY>[TR]
  [TD][​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Anna Titus na Salama Juma
  Maelezo
  Dar-Es-Salaam
  SERIKALI imekusudia kuifanyia mabadiliko mitaala ya elimu katika shule za msingi na sekondari ili mabadiliko hayo yaende sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoukabili ulimwenguni kwa sasa.
  Haya yamebainishwa ( leo) na Afisa Elimu wa elimu maalum wa halmshauri wa wilaya ya temeke Bw.George Vahaye , katika maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru wa mkoa wa Dar-Es-Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja.
  Vahaye alisema kuwa kubadilishwa kwa mitaala hiyo ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji yaliyopo kwa sasa nchini, ambayo ni pamoja na ufundishaji wa masomo mapya yakiwemo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika shule za msingi.
  Kuhusu mfumo wa elimu wa ya zamani na ya sasa, Vahaye alisema hapo zamani hakukuwepo na somo la TEHAMA lakini kutokana na uwepo wa maendeleo ya mfumo wa teknolojia duniani kote somo hilo limeanzishwa katika elimu ya shule za msingi hapa nchini.
  Aliongeza kuwa katika miaka ya hivi kariuni siku teknolojia mbalimbali zimevumbuliwa katika tasnia ya elimu, hivyo wahusika ambao ni walimu na wanafunzi hawana budi kufahamu na kuchukulia ukuaji huo kama changamoto kwao.
  Akizungumzia ukuaji wa sekta ya elimu katika halmashauri hiyo, alisema awali kabla ya uhuru manispaa ya Temeke ilikuwa na shule zipatazo 9 lakini baada ya uhuru manispaa hiyo ina shule zipatazo 108 ambazo ni sawa na asilimia 98 hii inadhihirisha kukua kwa elimu na kiwango cha taaluma" alisema Vahaye.
  Bw.Vahaye alisema kuwa tasnia ya elimu nchini inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa madawati , vifaa vya kufundishia , majengo imara kwa ajili ya wanafunzi pamoja na uhaba wa walimu wenye taaluma ya kutosha kufundisha masomo mbalimbali hususani somo la hisabati na sayansi kwa shule za msingi na sekondari.
  ''Hatuna budi kuisadia Serikali katika kukabiliana na changamoto hizo, kwani Serikali haipaswi kuachiwa suala hilo, hivyo ni jukumu letu sote kusaidiana katika suala la ujenzi wa madarasa ili kuendeleza sekta ya elimu nchini''.
  Naye Mratibu wa Kituo cha Walimu wilaya ya Temeke Bw. Daniel Matembele amesema kuwa walimu waliokuwepo shuleni hupatiwa mafunzo maalum pindi mitaala inapobadilika ili kuendana na wakati.
  [/TD]
  [/TR]
  </TBODY>[/TABLE]
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  amehamisha watoto wake kutoka Arusha kawapeleka kusikojulikana,huyu mzee wetu ndo hivyo tena
   
Loading...