singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,538
Ukiitwa mtanzania anza kujilaumu kwa maana English hatujui kiswahili mpaka tunawekewa penati Sasa kichina tutakiweza kweli. Serikali fikirieni Mara ya pili mnaweza kuwa mlikosea kufikiri kwa Mara ya kwanza. Tusidanganyike na ubia tukasahau uwezo wetu WA kielimu
Watu kama wewe ndio mnafanya uchumi wa nchi hii uzidi kudidimia, unakaa unamshawishi mtu aendelee kujifunza lugha bila mpangilio eti ili akaajiriwe huo ni ugonjwa wa upungufu wa kufikiri kichwani.Tatizo kuna watanzania wamelala!!! Wawekezaji wakubwa sasa hivi wanaoibukia duniani ni wachina.Ukiwa na ujuzi na ukawa unajua kichina ni rahisi kuajiriwa na wawekezaji wa kichina popote duniani.Nakumbuka kuna kipindi kampuni moja ya mafuta ilikuwa ikitaka marketing manager mtanzania awe na digrii moja ya marketing lakini awe anajua kifaransa.Hakupatikana walipatikana watanzania wana hadi PHD za marketing lakini hawajui kifaransa hadi wakaomba kibali kuajiri raia wa nje na raia waliyempata ni mkenya ambaye alikuwa na digrii ya marketing na alijisomea mwenyewe kwa kujilipia kusoma kifaransa hadi akakimudu barabara.Walipoulizwa kwa nini wanataka mtu ajuaye kifaransa wakasema wanataka asimamie soko lao la mafuta lililoko kongo na burundi ambako wanatumia kifaransa.
Taabu ya baadhi ya watanzania hasa UKAWA huwa ni kubeza tu kila kinachofanywa na serikali!
Watoto wanatakiwa waandaliwe kimataifa ili washindane ajira kimataifa ziwe za kichina,kifaransa,kiingereza n.k Naipongeza serikali ya Magufuli.
Kichina muda si mrefu kitakuwa moja kati ya lugha kubwa mno duniani kutokana na influence yake kwa dunia.
Walimu wa ufundi china wamesomea ufundi kwa lugha ya kichina na wanafundisha vyuoni kwa lugha ya kichina.Ukiwaleta hao walimu hapa hawataweza kufundisha sababu hawatumii kiingereza ndio maana serikali inaleta walimu wa kichina kwanza waje wafundishe watoto wengi kichina kwanza kisha ukiwaleta hao walimu wa ufundi wa kichina inakuwa rahisi kufundisha vyuo VETA .Kwanini serikali isiende kuchukua walimu wa ufundi china waje kufundisha vijana jinsi ya kutengeza simu, radio nk
Ningekuwa mimi ningeimarisha zaidi somo la kiingereza. Huwezi kupinga kwamba lugha namba moja duniani ni English. Hata ukienda huko China kwenyewe wanagombania madarasa ya kiingereza. Ukikutana na mfaransa, mGerman, Mreno, MuItaliano wanajua sana lugha zao lakini utashangaa hata English wanajua. English ni lugha ya dunia ambayo ukiijua ina fursa nyingi mno. Leo hii Mtanzania ukitaka uombe scholarship Marekani na UK bila cheti cha lugha (TOEFL) hupokelewi wakati nchi za Africa magharibi wao cheti cha form four yao tu kinatosha. Tunakosa scholarship mamia wanabaki kwenda watoto wa vigogo tu waliosoma English Mediu. Leo mnatuletea kichina sisi wana wa maskini inauma.WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imeteua shule sita za sekondari nchini kuingia katika mpango maalumu wa wanafunzi wake kufundishwa somo la lugha ya Kichina kuanzia mwaka huu.
Kutokana na uamuzi huo, walimu 12 kutoka China wamekamilisha utaratibu wa mpango kazi wa namna ya ufundishaji wa somo hilo kwa shule zilizoteuliwa mara zitakapofunguliwa rasmi mwezi huu.
Ofisa Elimu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Salum Salum, alitaja shule zilizoingizwa kwenye mpango huo katika awamu ya kwanza ni Benjamin Mkapa na Chang’ombe (Dar es Salaam), Msalato na Dodoma (Dodoma), Morogoro na Kilakala za mkoani Morogoro.
Salum alitoa taarifa hiyo juzi wakati akifungua mafunzo ya kazi na mipango mikakati iliyoandaliwa na Taasisi ya China inayojihusisha na lugha ya Kichina kwa walimu wake walioteuliwa kufundisha somo la lugha ya kichina katika shule hizo.
Alisema kabla ya kufunguliwa kwa shule, viongozi wa China wamekutana kwa siku mbili mjini Morogoro kufanya mafunzo ya kazi ya kujiandaa kuingia darasani baada ya shule kufunguliwa.
“Mafunzo kazini ni ya kujiandaa na kupeana mikakati na nini kifanyike kabla ya shule kufunguliwa ili kuingia madarasani kufundisha wanafunzi wa kitanzania lugha ya kichina,” alisema Ofisa Elimu Mkuu.
Alisema wanafunzi watatahiniwa somo hilo la lugha ya kichina katika mitihani yao na watakapohitimu watahesabiwa alama za ufaulu sawa na yalivyo masomo mengine yanayofundishwa katika shule za sekondari kama ilivyo kwa Kifaransa na Kijerumani.
Alisema wizara inaona ni njia nzuri kwa vijana wa Kitanzania kuwa na lugha ya mawasiliano katika kuwasaidia kujifunza zaidi na kutumia fursa zitakazopatikana China ikiwemo kujiendeleza na elimu ya juu zaidi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya China ya lugha ya kichina, Ambar Zheng, kutoka katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alisema walimu 12 wa China wameshapatiwa mafunzo ya namna ya kufundisha somo hilo kwenye shule husika.
Alisema kila shule ya sekondari iliyoteuliwa katika mikoa hiyo ya Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro, zitapangiwa walimu wawili kila moja kwa ajili ya kufundisha somo hilo kuanzia mwaka wa masomo unaoanza mwezi huu.
Alipongeza ushirikiano mzuri uliooneshwa kati ya Serikali ya Tanzania na China na wizara husika kuwezesha kuanzishwa kwa somo hilo katika baadhi ya shule za sekondari nchini. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Waislamu cha Morogoro, Profesa Hamza Njozi alipongeza Serikali ya China kwa kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali, ikiwemo elimu ya vyuo vikuu.
ni kweli mkuu, lugha ikifundishwa kutoka chini ni nzuri zaidiKWA NINI WASIFUNDISHE PRIMARY SCHOOL HICHO KICHINA WAMEENDA KWA SECONDARY SCHOOLS
Swala si kwamba hiyo lugha ni namba moja au ngapi swala ni kuwa hiyo lugha ina manufaa kiuchumi kwa watu wengi au la.KWA SASA FURSA NYINGI ZA ELIMU NA KIUCHUMI kwa watanzania zinapatikana zaidi china kuliko kwenye nchi zingine zinazoongea kwa ufasaha lugha ya kiingereza.Ni rahisi watanzania wengi kwenda kufanya biashara China kuliko Uingereza au marekani.Vijana wengi na wazazi wengi wanaweza somesha watoto wao na kuweza kulipia kule ada kuliko nchi hizo za kiingereza.Ningekuwa mimi ningeimarisha zaidi somo la kiingereza. Huwezi kupinga kwamba lugha namba moja duniani ni English .
The black person's stupidity must be liberated from the mind.Swala si kwamba hiyo lugha ni namba moja au ngapi swala ni kuwa hiyo lugha ina manufaa kiuchumi kwa watu wengi au la.KWA SASA FURSA NYINGI ZA ELIMU NA KIUCHUMI kwa watanzania zinapatikana zaidi china kuliko kwenye nchi zingine zinazoongea kwa ufasaha lugha ya kiingereza.Ni rahisi watanzania wengi kwenda kufanya biashara China kuliko Uingereza au marekani.Vijana wengi na wazazi wengi wanaweza somesha watoto wao na kuweza kulipia kule ada kuliko nchi hizo za kiingereza.