Shule nyingi za Private zimekufa kimtindo...!

Shule nyingi za Private zimekufa kimtindo...!

Baba Mama

Senior Member
Joined
Apr 1, 2018
Posts
107
Reaction score
138
Kuanzia mwaka 2015 na kuendelea kuna wimbi kubwa la shule nyingi za Private kufungwa ama kubadilishwa matumizi.

Hata zile ambazo bado zipo zina survive lkn zinajikongoja kwa taabu kubwa sana. Ukiangalia kwa mfano shule unakuta ilishiriki NECTA exams 2015 lkn ghafla imepotea haipo 2016 wala 2017. Nina mifano hai.

Mostly, wameshindwa kushinda kwa sababu kuu nne.

1. Uwezo wa kielimu wa wanafunzi wenyewe

2. Uwezo wa ufundishaji wa walimu wenyewe

3. Uwezo wa wazazi kumudu ada kipindi hiki

4. Utawala kwa ujumla wa shule

Hayo niliyoyataja hapo juu, hupelekea wanafunzi kupungua sana na hatimaye shule kukosa wanafunzi kabisa.

Lakini, kuna jambo la kushangaza sana. Ukitazama Sekondari ya Jitegemee ina wanafunzi wengi sana japo ni ya private, ingawa matokeo ya kimitihani si makubwa saaana. Jambo hili linashangaza sana.

Jamani, tufanye hv. Kama una shule na unaona kabisa inaweza kukushinda muda si mrefu, pls tuwasiliane tupeane ABC za hapa na pale kunusuru shule yako, huenda mawazo haya yakakufaa.

On top of this japo itakuwa inachanganya mada: Kama una hitaji la walimu wa:

1. Physics
2. Chemistry
3. Biology
4. Mathematics

5. Book Keeping
6. Commerce

7. Georgraphy
8. Kiswahili
9. History

Tuwasiliane, tukuunganishe nao bure.

Nawasilisha.
 
Nje ya mada: Hivi serikali mbona imechelewa sana kupanga shule wanazokwenda vijana wa form five mwezi wa saba?!!!🙁🙁🙁
 
Yaani mie nashindwa kuelewa mkuu Baba Mama. Wangepanga fasta ili kama ikitokea mtoto amepangwa shule ambayo haiko njema, basi wazazi wajiandae kumpeleka shule ya binafsi
Nakuelewa sana NAHUJA lakini, ktk maisha kuna jambo lipo nje ya uwezo wako, mojawapo ni hili. Lkn kuna kuna suluhisho za aina mbili: moja, subiri mbili, ujiandae km vile mtoto hajapangwa shule nzuri
 
Mkuu umetengeza tangazo kwa kiwango cha juu sana.

Hongera.
Hahahahaha.....sisi watz 'angle' yetu ya kufikiria jambo, nahisi ni ya hali ya juu sana, basi tu dunia imekataa kututambua kwa kuwa angle hiyo haina msaada wowote kwenye dunia hii.
 
Hahahahaha.....sisi watz 'angle' yetu ya kufikiria jambo, nahisi ni ya hali ya juu sana, basi tu dunia imekataa kututambua kwa kuwa angle hiyo haina msaada wowote kwenye dunia hii.

Kabisa mkuu...

Ila changamoto nyingine kwenye hizi shule ni vile wamiliki wakichukua ada wanazi-channel kwenye miradi mingine, sasa hivi miradi mingi inajikongoja sana.

Halafu kuna ada kibao ziko overpriced, sasa kwa uchumi huu wazazi wanabanwa.
 
Yeah, nakuelewa sana. Nadhani unachojaribu kusema ni kuwa pamoja na wazazi kulipa ada bado wenye shule hawana mawazo endelevu ya kusimamisha shule isimame vizuri kiushindani badala yake wana focus kwenye miradi iliyo nje ya shule. Nakubaliana nawe!
 
Kabisa mkuu...

Ila changamoto nyingine kwenye hizi shule ni vile wamiliki wakichukua ada wanazi-channel kwenye miradi mingine, sasa hivi miradi mingi inajikongoja sana.

Halafu kuna ada kibao ziko overpriced, sasa kwa uchumi huu wazazi wanabanwa.
Kingine, ada ni kubwa haiendani na uhalisia wa ki uchumi. Pia, nakubaliana nawe.
 
Back
Top Bottom