Kwanza nitangulize shukrani zangu za dhati kwako mkuu wa wilaya yetu ya Kisarawe!
Napenda juhudi zako,u bunifu wako na fighting spirit chanya juu ya wilaya yetu.
Sambamba na juhudi zako ndani ya muda mfupi kumekuwa na mabadiliko mazuri ndani ya wilaya, nakupongeza sana.
Nije kwenye kiini cha uzi wangu;
Shule yetu mpya inayotarajiwa kutoa elimu hivi karibuni IWE YA O'LEVEL YA WASICHANA WENYE UFAULU MZURI KUTOKA DARASA LA SABA.
Iwe inachukuwa japo wasichana watatu toka kila shule wilaya nzima. Hii itasaidia sana kuwawezesha watoto waliokuwa na uwezo kuendeleza taaluma zao bila ya kukumbana na changamoto za kimazingira na vishawishi.
Pia watoto wahusishwe moja kwa moja kwenye programs mbalimbali mathalani kilimo cha mboga mboga, uhifadhi wa mazingira pamoja na uzalishaji wa miche ya mazao kama minazi, maembe, mikorosho, michungwa na mipapai.
Kuwepo na mkuu wa shule mtendaji hasa atakaye simamia taaluma, nidhamu, mazingira na projects mbalimbali shuleni