shule ina utamu wake jamani!

GreenCity

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Posts
5,872
Reaction score
4,604
mfagiaji wa kwenye ndege aliokota kitabu ndani ya ndege kilichokuwa kimeandikwa hivi:
1. ukitaka kuwasha ndege bonyeza kitufe chekundu. jamaa akabonyeza ndege ikawaka grrrruuuummmm!
2.ukitaka ndege ianze kutembea bonyeza kitufe cha kijani. jamaa akabonyeza na ndege ikaanza kutembea aaaangghhh!
3. ukitaka ndege ipae bonyeza kitufe cha njano. jamaa akabonyeza na ndege ikapaa uwaaaaaaa!
SASA kuona vile yule jamaa akasema "yaani kuna watu ni mabwege kweli yaani wana poteza pesa kwenda kwenye mavyuo kusomea urubani wakati kitu EASY tu, pumbavu kabisa"
baada ya ndege kwenda zaidi akaanza kuperuzi kile kitabu ili atafute maelezo zaidi jinsi ya kutua na kusimama, lakini akakuta hii:
4. ukitaka kujua mambo mengine zaidi kuhusu kuendesha ndege, jiunge katika vyuo vyetu kwa anuani zetu zilizopo pale airport. jamaa kuona vile akazimia palepale.... baadaye akazinduka na kupitia dirishani akagundua ndege iko juu ya bahari na alarm na kitaa chekundu kinawaka kuonesha "you are running out of fuel".......!
 
Chezea taaruma ya watu weyee!
 
utani na uongo mwingine kama kweli
 
ukweli mwingine bhana kama uongo na utani
 
Ikiwa unaona elimu ni ghali basi jaribu ujinga.
 
Ukishagundua na ujinga pia ni ghali basi usijaribu chochote.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…