Shule hizi ni shule gani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule hizi ni shule gani.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 3, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Shule niliyo somea darasa la kwanza mpaka la nne ilikuwa na Bush school pembeni, ambayo leo inaitwa chekechea.Hii ilisaidia kumuandaa mtoto ili awe na mkao wa kusoma anapoingia darasa la kwanza.Nilipo faulu kwenda darasa la tano, nilijiunga na iliyoitwa middle school, ambayo pamoja na kuwa na waalimu mahiri,pia ilikuwa na carpentry unit,ambayo nadhani ilikuwa na nia ya kutuandaa kujiajiri baada ya elimu ya middle school, kwa vile ilikuwa dhahiri wote tusinge faulu kwenda sekondari.Na kweli, nilifaulu peke yangu kwenda sekondari.Nimesahau jambo moja au mawili hivi ya msingi.Ingawa shule hii haikuwa shule ya bweni,lakini mchana tulikuwa tunapata chakula.Na hapa nadhani nia ilikuwa ni kutufanya tuweze ku-concetrate vizuri kwenye masomo ya mchana.Jambo la pili ni kwamba kuanzia darasa la tano, ilikuwa huturuhusiwi kuzungumza Kiswahili.Nakumbuka wengi tulipofika darasa la sita tulikuwa tunazungumza kingereza fasaha kabisa, hata tukawa na 'debating socities,' achilia mbali umahiri mkubwa katika Hesabu,Science,Geografia,Historia nakadhalika.Sekondari hali ilikuwa ya kufurahisha zaidi.Shule ikawa imesheheni waalimu wazuri kwa kila somo.Library ilikuwa imesheheni vitabu achilia mbali vile vinavyogawiwa madarasani kwa kila somo.Tena vya waandishi wanao heshimika kimataifa wakina Abbot,Mackean nk.Maabara ndio usiseme, kila mwanafunzi alikuwa na kifaa chake.Chemicals wala usiseme, hakuna siku tuliyoambiwa kwamba hatuwezi kufanya practical kwa vile chemical fulani hakuna.Kiswahili hakikuwa kinazungumzwa hadharani labda mkikutana rafiki wazuri wawili au nje ya shule.Mazingira ya shule yalikuwa mazuri mno.Niseme nini, kila kitu kilikuwa kinafanyika kwa umakini na umahiri mkubwa.Sasa jinamizi hili lililoingia katika elimu na kuharibu kila wazo zuru limetoka wapi? No, kuna haja ya kujiuliza.Watanzania jamani, tujiulize watoto wetu wataendelea kupewa elimu hii feki mpaka lini?Mimi kama mzazi nasema haikubaliki.Nadiriki kusema watanzania mmepigwa sindano ya ganzi.Amkeni basi mtetee haki zenu.
   
Loading...