Shukuru Kawambwa kwenye mgogoro wa ardhi na diwani mstaafu, Hassani Usinga. Watishiana kufungana pingu

Hii ndio shida ya watanzania, wakipata ajira sijui busara inaenda wapi. Kwani hata ukiwa na mamlaka huwezi kuongea na watu vizuri mkaeleweshana mpaka ufoke?

Sasa hata kama hakumfahamu Dr.Kawambwa, alipaswa kuongea nao vizuri tu, na hata kama unampeleka mtu polisi unamueleza kawaida hapa umefanya makosa, na ina bidi twende polisi ukatoe maelezo, au tutakushitaki ili huyu mlalamikaji apate haki yake.

Lakini Duh utafikiri mtu kaingiwa mashetani/majini anapayuka na kelele utadhani mwehu.

Uzee ni mtakuja hata uwe kijana vipi utazeeka tu, sasa kwanini usiwe na busara na hekima unapoongea na wazeee?

Tukiwa kwenye ofisi zetu tuwe na busara na ustaarabu kidogo.
Ndugu yangu ogopa mtu aliyeambatana na hawara, anaweza fanya lolote kwani anatumia kichwa cha chini kufikiri
 
Kawambwa ni mstaarabu sana sio muongeaji. Naona vijana wanampa jambajamba 😃
Mie tanguleo namwita shukuru siombwa, the guy is humble very humble, na dso mstaafu ni very professional guy, wamejifanya wasenge ili waweze kumfikisha mhalifu kwenye vyombo vya dola. Hawa wazee wana vyuma majumbani mwao wangepiga simu watoto wakavileta pasingetisha, halafu jamaa fala sana unamfunga kamba professor? Yaani kadhalilisha udsm yote cammon,

Anajikata network tupeni detail zake tukutane nae mtaani sio ambao tunajua kusoma na kuandika tu kama dotto magari tudeal nae
 
Mimi nilichokuwa najiuliza hapo anaenda kumpeleka polisi kama nani? Anachomaanisha kwamba yeye anauwezo wa kuwaamrisha polisi wafanye anayoyataka.ndio maana anamuambia kuwa yeye ana nguvu.
Inaonekana hata serekali ya mtaa inamuogopa ndio maana wakawatuma hao wazee wawili.
Na pia huyo mzanzibari inaonekana kichwani hamna kitu kabisa.unamuitaje mtu muhalifu kwa kufunga barabara.kwani hiyo barabara ni mali yake?
Raia yeyote ana haki ya kumkamata mtu na kukfikisha kwenye vyombo vya dola na ikibidi nguvu kidogo itumike. Hapo kwenye kupima nguvu kidogo ndo shida tu basi
 
Mleta mada huna adabu.
Prof. Kawambwa ninafahamiana naye.
Hawezi kujiingiza kwenye udalali. Hakua na elimu ya kudesa huyu bwana. Amesoma uhandisi UDSM akasoma PhD yake masuala ya engineering Australia
Hakua na skendo za kipuuzi na si mtu wa kujikweza na mpuuzimpuuzi kama walivyo CCM wengi.
 
Issue sio udalali hapa. Malori ya mchanga yanaingia kwenye eneo lenye barabara ya kuingia kwake na pia kwenda shule ya sekondari na kufanya uharibifu wa barabara. Yeye Kawambwa na huyo mwingine aliyedhalilishwa DSO Mstaafu wa Kawe na Bagamoyo Madondola waliamua kuweka vigogo vya mnazi ili malori yasipite na kuharibu barabara ndipo walipokutwa na huyo Hassan Wembe Diwani mstaafu wa Kiromo na beki ya zamani ya timu ya Malindi Zanzibar. Wembe ni mmiliki wa mashimo ya mchanga huko Kiromo kwahiyo kuzibwa Kwa barabara kunazuia malori kuingia na hivyo kukosa fedha. Mhusika huyo wlWembe na washirika wenzie walikamatwa jana na wako lokapu hadi sasa. Nadhani jambo limekuwa kubwa kwani mmoja ya waliodhalilishwa ni DSO Mstaafu na DSO Bagamoyo kasimamia zoezi zima kuhakikisha wanakamatwa !
Kawambwa na JK ni ndugu kabisa wale! Kijana atajua,hajui! Watampoteza kwa msala watakaompa
 
Nimeludia kuitizama vzr video ya jamaa anavyomshambulia Dk. Kawambwa, kiukweli jamaa alikosea sana na bila shaka atajuta sana kwa ujinga mwamba alioufanya??

Hivi ujasili wa kumfanyia vivyo kiongozi mstaafu aliutoa wapi?

Pia nimpongeze mzee Kawambwa kwa busara kubwa sana alioionesha! Ingekuwa mtu mwingine pale pangechimbika vibaya sana. Mimi mwenyewe sikubali unyonge wa namna hiyo.
 
Kawambwa ni mstaarabu sana sio muongeaji. Naona vijana wanampa jambajamba 😃
Kweli jamaa namkumbuka sana kipindi kile cha Hawamu akiwa waziri Elimu...kuna kamgogoro flan hivi tulikafanyaga akiwa na Naibu waziri wake anaitwa somebody Mrugoo walituzingua sana...Ila huyu Mwamba alikuwaga Mpole sana ata ukikutana nae anaongea poa sana.
 
Kweli jamaa namkumbuka sana kipindi kile cha Hawamu akiwa waziri Elimu...kuna kamgogoro flan hivi tulikafanyaga akiwa na Naibu waziri wake anaitwa somebody Mrugoo walituzingua sana...Ila huyu Mwamba alikuwaga Mpole sana ata ukikutana nae anaongea poa sana.
Philip Mulugo - much know 😃
Alitoa boko Mulugo nakumbuka la kijiografia.
 
Back
Top Bottom