akida jr
Senior Member
- Jan 1, 2014
- 111
- 58
Habari zenu wanajukwaa,
Ndugu yangu amehitimu kidato cha sita 2018 mchepuo wa 'PCB' akafaulu kwa C kila somo. Ndoto yake ni kusoma Doctor of Medicine (MD) na hivyo aliomba kozi hiyo kwenye vyuo vitatu Muhimbili, KCMC na Dodoma (UDOM) chaguo lake la kwanza likiwa MD kila chuo. Matokeo yake amechaguliwa Udom kwa kozi ya 'Bachelor of Science in Physics (BSC-PHYS) ambayo ilikuwa chaguo la pili. Hata baada ya kufanya maombi awamu ya pili kwenye vyuo vya MUHAS na KCMC, hakukuwa na jawabu lolote.
Hata hivyo, kijana amekata shauri kwenda tu kusoma kozi hiyo hiyo aliyochaguliwa nayo, shida iliyopo ni kwamba hatujui hasa ni nini atafanya baada ya kuhitimu hiyo programu (yaani ni shughuli gani huwa wanafanya waliosoma hiyo kozi)?
Tafadhali nisaidieni mawazo kwa niaba yake.
Nawatakieni siku njema.