GE2025 Sho Madjozi: Watanzania ni watu wapole, kufikia hatua ya kupambana ni ishara kuna jambo kubwa limefikia kikomo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,661
Reaction score
59,098
‎Msanii mashuhuri kutoka Afrika Kusini, Sho Madjozi, ametoa ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram akielezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu marafiki na Watanzania kwa ujumla, kufuatia kile kinachoendelea nchini Tanzania baada ya maandamano na machafuko yaliyosababisha vifo, majeraha na kukatika kwa mawasiliano ya simu na intaneti.‎‎

Sho Madjozi amesema kuwa ameshindwa kuwasiliana na marafiki zake waliopo Tanzania na hivyo anajisikia kuhuzunishwa na hali hiyo.

‎‎Kupitia ujumbe wake, aliandika:‎‎ “Tangu jana siwezi kupata marafiki zangu Tanzania kwenye simu. Niko worried sana.

Ninachokijua ni kwamba naipenda sana Tanzania. Ninaamini kuwa Watanzania, kama watu wote, wana haki ya kuchagua waongozi wao, na haki pia ya kuandamana kwa amani bila hofu au vurugu.”‎‎Ameongeza kuwa Watanzania ni watu wapole, na kwamba kwao kufikia hatua ya kupambana ni ishara kwamba “kuna jambo kubwa sana limefikia kikomo. ”‎‎Sho Madjozi pia ametuma ujumbe kwa viongozi wa Tanzania, akisema:‎‎“Kwa walio madarakani: dunia inatazama.

Mnaweza kuzima mtandao, lakini hamwezi kuzima tamaa ya kuona mabadiliko. Maombi ya watu yanapaswa kujibiwa kwa mabadiliko, siyo kwa ukandamizaji. "Akiendelea kuzungumzia maandamano yanayoendelea nchini humo, msanii huyo amewataka wananchi kuwa watulivu na kuepuka vurugu, akisisitiza kuwa:‎‎“Vurugu ni silaha yao, siyo yetu.

Tafadhali muwe salama. Tanzania daima.”‎‎Sho Madjozi ni miongoni mwa wasanii wachache wa kimataifa waliotumia majukwaa yao kuonyesha uungaji mkono kwa amani na demokrasia Tanzania, jambo lililopokelewa kwa hisia kali mitandaoni.#ForThePeople #ToThePeople #WananchiForum #Demokrasia #HakiZaKiraia #Maandamano
 
‎Msanii Sho Madjozi wa Afrika Kusini ametoa ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram akielezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu marafiki na Watanzania kwa ujumla, kufuatia kile kinachoendelea nchini Tanzania baada ya maandamano na machafuko yaliyosababisha vifo, majeraha na kukatika kwa mawasiliano ya simu na intaneti.

‎Sho Madjozi amesema kuwa ameshindwa kuwasiliana na marafiki zake waliopo Tanzania na hivyo anajisikia kuhuzunishwa na hali hiyo.

‎Kupitia ujumbe wake, aliandika:

‎“Tangu jana siwezi kupata marafiki zangu Tanzania kwenye simu. Niko worried sana. Ninachokijua ni kwamba naipenda sana Tanzania. Ninaamini kuwa Watanzania, kama watu wote, wana haki ya kuchagua waongozi wao, na haki pia ya kuandamana kwa amani bila hofu au vurugu.”

‎Ameongeza kuwa Watanzania ni watu wapole, na kwamba kwao kufikia hatua ya kupambana ni ishara kwamba “kuna jambo kubwa sana limefikia kikomo.”

‎Sho Madjozi pia ametuma ujumbe kwa viongozi wa Tanzania, akisema:

‎“Kwa walio madarakani: dunia inatazama. Mnaweza kuzima mtandao, lakini hamwezi kuzima tamaa ya kuona mabadiliko. Maombi ya watu yanapaswa kujibiwa kwa mabadiliko, siyo kwa ukandamizaji.”

‎Akiendelea kuzungumzia maandamano yanayoendelea nchini humo, msanii huyo amewataka wananchi kuwa watulivu na kuepuka vurugu, akisisitiza kuwa:

‎“Vurugu ni silaha yao, siyo yetu. Tafadhali muwe salama. Tanzania daima.”

‎Sho Madjozi ni miongoni mwa wasanii wachache wa kimataifa waliotumia majukwaa yao kuonyesha uungaji mkono kwa amani na demokrasia Tanzania, jambo lililopokelewa kwa hisia kali mitandaoni.
 
Msanii wa Nje anaandika kwa uchungu ,hawa wasanii wetu wanakebehi watu
 
Wasanii Watanzania machawa tu makupe wa mfumo, pia huyo anatokea SA ambapo walimenyana sana na makaburu.
Sure! Wapo kimya wakiumwa wanataka misaada
 
Huo ndio ukweli, ukikuta mbuzi juu ya mnazi ujue kapandishwa huyo, VIONGOZI WETU ndio chamzo cha haya yote kwa tamaa zao za madaraka na uroho wao wa mali
Ila hao uliowaita viongozi hawataki kuliona hilo, wao wanakimbilia kusema ni watu wa nje wanatuonea wivu na rasilimali zetu. Ina kera sana. Siku wakitambua kwamba wao ndiyo tatizo la nchi kufika hapa tulipo itakuwa too late
 
Aisee nahisi kuna siri nzito sana hawa watu wanaogopa wakitoka madarakani zitawaharibia hadi kizazi chao.. Sidhani kama ni madaraka haya haya tu ndo yanapambaniwa kwa kiasi hiki.
Kwa kweli. Lazima kuna kitu
 
Ila hao uliowaita viongozi hawataki kuliona hilo, wao wanakimbilia kusema ni watu wa nje wanatuonea wivu na rasilimali zetu. Ina kera sana. Siku wakitambua kwamba wao ndiyo tatizo la nchi kufika hapa tulipo itakuwa too late
Unadhani hawatambui kwamba wao ndio tatizo?. Shida sio kutambua shida ni kukiri kwamba wao ndio tatizo!
 
Ila hao uliowaita viongozi hawataki kuliona hilo, wao wanakimbilia kusema ni watu wa nje wanatuonea wivu na rasilimali zetu. Ina kera sana. Siku wakitambua kwamba wao ndiyo tatizo la nchi kufika hapa tulipo itakuwa too late
Wanaongea ujinga huo sababu wanajua watanzania sisi ni wajinga wajinga, lak8ni wakae wakijua wajinga wameanza kupungua, werevu umewaingia, hii sio mwaka 97 huko, ama 2002.. miaka hii watu wanapata maarifa kirahisi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…