Shivji asisitiza umakini uwekezaji wa ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shivji asisitiza umakini uwekezaji wa ardhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 16, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Shivji asisitiza umakini uwekezaji wa ardhi [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 16 June 2012 08:53 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  MWENYEKITI wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Profesa Issa Shivji amesema,Tume ya kuratibu maoni ya Katiba Mpya ikumbuke kujadili umakini wa suala la nchi za Magharibi kuwekeza katika ardhi kwa ajili ya kambi za kijeshi.

  Profesa Shivji alisema hayo kupitia mhadhara wake wa katiba unaorushwa na kituo cha ITV jijini Dar es Salaam na kwamba nchi nyingi barani Afrika ambazo zilifanya hivyo zimejikuta kwenye machafuko ya vita.

  “Ni lazima Tume wakumbuke jambo hili muhimu sana, nchi za kibepari wana mikakati ya kuweka kambi zao za kijeshi barani Afrika,ukitoa eneo la ardhi kwa wawekezaji wa aina hii watavuruga nchi”, alisema na kuongeza:

  Ni marufuku kutoa eneo la ardhi,anga na maji kwa ajili ya kambi ya kivita,ni muhimu kujua hilo ili kuinusuru nchi”, alisema Shivji.

  Akitoa mfano wa Mataifa ambayo yameathirika kwa sababu ya kutoa sehemu ya ardhi ndani ya nchi zao ni pamoja na Iraq,Somalia na Pakstan na sehemu nyingine barani Afrika.

  Alisema, hali hiyo inaweza kusababisha kuuza uhuru wa watu. Profesa Shivji akatoa mfano wa kitabu kilichoandikwa na Edward Sokoine mwaka 1982 kinachozungumzia Taifa kuuza uhuru wake ili kupata misaada kutoka nje.

  “Nchi za kiafrika zinasumbuliwa na tatizo la kiuchumi hivyo inatoa eneo la ardhi kwa uwekezaji ili kupata misaada ya kifedha,tumeona madhara mengi yaliyoanza kujitokeza,”alisema.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ayasemaya Profesa Shivji ni too let, Tayari Kikwete alikwisha tia sign wamarikani kutumia Anga yetu na Bahari , hii ilikuwa ni njaa yake na kujipendekeza binafsi kwa alokuwa rais wa Marekani Bill klinton.
   
Loading...