Shivji apinga Afrika Mashariki kuikodolea macho Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shivji apinga Afrika Mashariki kuikodolea macho Marekani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ustaadh, Feb 10, 2010.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  PROFESA Issa Shivji amepinga msimamo wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa kutaka nchi za Afrika Mashariki kuweka malengo ya kupata chochote kutoka Marekani kutokana na kuongozwa na Rais Barack Obama .  Amesema itakuwa fedheha kama nchi za Afrika Mashariuki zitabweteka na kusubiri fadhila kutoka Marekani na kwamba kwa vyovyote vile hakuna kitakachotolewa Marekani bure.  Juzi, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala akizungumza kwenye kongamano la jinsi ya kunufaika na utawala wa Rais Obama alisema Afrika Mashariki ni lazima inufaike na uongozi wa rais huyokwa kuwa ni mwwenye asili ya Afrika Mashariki.

  Kamala alisema Afrika Mashariki ingalie ni vitu gani ambavyo vitaiwezesha Marekani kuisaidia ikiwa ni pamoja na kuboresha miundo mbinu kudumisha amani na demokrasia ya kweli.  Lakini Shivji alisisitiza kwamba ni bora Afrika Mashariki ikajitegemea ili kuepuka kutawaliwa kiuchumi na Marekani.  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Shivji alisema Afrika Mashariki isitegemee kunufaika na uongozi wa Barack Obama kutokana na ukweli kwamba hakuna sera iliyobadilika nchini Marekani na kwamba Obama anaendeleza Sera za Bush.  "Suala hili tutapoteza uhuru wetu, kwanini tutegemee Marekani kutuamlia mambo yetu, Marekani ni nani ?, sanasana Marekani watatusaidi silaha za kijeshi, je tunataka kujenga bara letu kijeshi? "alihoji Shivji ambaye ni Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  "Mbona kipindi cha chama cha TANU hakikuwa chini ya taifa lolote na tuliendelea mpaka tukapata CCM sasa hapo

  "Kwa kifupi mimi nataka Marekani iwe mbali na Afrika Mashariki, Afrika isitegemee mjomba , ikitaka kupata maendeleo ipigane yenyewe kama ni kudumisha amani tudumishe kwa manufaa yetu wenyewe sio Marekani ije"alisema.

  Hata hivyo, alisema wasomi wa Afrika Mashariki wanapaswa kulaumiwa na kujilaumu wenyewe kwa kutowaelimisha watu juu ya ubaya wa kutegemea wafadhili kwa kuwa bara letu kihistoria ndefu.


  Source:http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=17852
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Feb 10, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,285
  Likes Received: 40,520
  Trophy Points: 280
  Oh Africans..Africans...Africans...Yaani kweli wanaandaa 'kongamano" la jinsi ya kunufaika na utawala wa raisi Obama? Na huyo "Dk" Kamala kweli alisema lazima Afrika Mashariki inufaike na uongozi wa Obama kwa vile babake alitokea Kenya? Ingekuwa vyema tukapata nukuu kamili ya alichosema "Dk" Kamala.

  But even the whole idea of having a symposium on how to benefit from the Obama administration is.....(you fill in the blank). I'm fighting myself not to go in on these negro muthafuckas. I guess my signature says it all.
   
 3. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Well said kamanda....Miafrika ndivyo tulivyo we can't think for ourselves!
   
 4. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Huyu 'dr' Kamala ni design ya akina Nchimbi,Nagu,Makongoro etc.
  Shame anatuwakilisha EAC ,yeye na so called ,'dr' Nangale.

  Naona Wakenya na Waganda wanatuona sisi ni fake of fakers
   
 5. Z

  Zebaki Member

  #5
  Feb 10, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  OMG yaani badala ya ubunifu wa jinsi ya kujiboresha tunawania misaada, duh kwa mwendo huu tutafika kweli???!!!
   
 6. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,681
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Mtegemea cha nduguye hufa hali ya kimasikini sana.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Feb 10, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,285
  Likes Received: 40,520
  Trophy Points: 280
  Ila binafsi sishangai kwa huyu waziri kusema haya yanayosemwa alisema. Kwa sababu si Waafrika wa Afrika Mashariki tu wafikiria hivi bali hata kipindi kile Obama alipoenda Ghana, raisi wao mstaafu John Kufour alihojiwa na essentially akasema kama hayo yanayodaiwa kusemwa na Kamala. Hata Marekani wanugu wengi walikuwa wanadhani na kuna baadhi ambao bado wanadhani kuwa Obama atafanya mambo kuwasaidia wao kwa sababu ni nusu mzungu nusu mweusi.
   
 8. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  HAkuna haja ya kumsema Dr. Kamala maana ni yeye anajumuisha tu dhana ya Miafrika NdivyoTulivyo ... Julius JF Senior Expert Member
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Feb 10, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,285
  Likes Received: 40,520
  Trophy Points: 280
  Kweli viongozi wetu ni wana akisi watu wanaowaongoza.
   
 10. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Uko sahihi mkuu, tangu lini mbuyu ukazaa embe? Au mpera ukatoa nanasi?
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Feb 11, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  You have said well Julius but please people hebu nisaidieni kuitafsiri hii heading
  "African Development Policy Goals and Strategies: Implications of the Obama Presidency"
  Kwa sababu hii ndiyo ilikuwa heading ya kingamano hili ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania na Kenya. Sidhani kama lengo au tafsiri ni jinsi ya kunufaika na utawala wa Obama bali ni kuangalia implication ya utawala wa Obama katika malengo na mipango ya maendeleo ya Africa. Kwa uelewa wangu mdogo nilielewa kuwa utawala wowote wa nchi ambazo zimekuwa zikitupatia misaada mbalimbali una affect maendeleo ya Africa iwe ni Bush au Obama kufuatana na zile priority areas zao.

  Kwenye kongamano hili Dr. Kamala nakumbuka alitaja maeneo kama nane ambayo utawala wa Obama umejaribu kuyapa kipaumbele na maeneo hayo yote yana theme kuu za African peace and Security. Dr. Kamala alijaribu kuelezea namna ambavyo tunawezatoa ushirikiano katika kutekeleza malengo haya ikiwa ni pamoja na kupanga mipango yetu katika kuaddress hizi areas ili kuunganisha nguvu na Obama.
  Si nia yangu kuwapinga mitazamo yenu but nilitaka kutoa ufafanuzi wa yaliyojiri pale kwenye kongamano na pia kuwezakupata uelewa zaidi juu ya hii hoja.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...