Viti maalum vya CHADEMA vinakwenda kwa watu maalum , Kanda maalum na familia maalum. Hivyo vilitengwa kwa watu wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha tu, na kwa familia za Slaa, Mbowe na Ndesamburo
Kwenye bold hata mimi pananipa mashaka kama uongozi umeshasema tuhuma hazina msingi still mtuhumiwa anasisitiza uchunguzi haujaisha sijui anataka aambiwe tuhuma ni za kweli, kama hivyo basi yeye Shitambala atuambie kama tuhuma ni za kweli.Shitambala usijivunjie heshima katika jamii. Madai yako ni ya msingi kabisa lakini namna unavyoyaleta katika jamii unazidi kutoa mianya ya utata juu ya shutuma za rushwa kwako. Nadhani kama uliweza kutuhumiwa kupokea fedha ili uuze Ubunge basi si ngumu kuhisi tena kuwa umepokea ili uisambaratishe chadema huko Mbeya. Katibu mkuu amekuandikia barua kuwa tuhuma hizo hazina msingi na si za kweli lakini wewe unasisitiza kuwa uchunguzi ahujaisha... ni uchunguzi gani huo na unaendeshwa na nani???? Sasa unakuja na dai jipya ... ngoja tusubiri uongozi wa juu utasema nini kuhusu hilo!
Nafikiri Mh. Shitambala unaweza kutenda vyema zaidi ya msimamo ulionao kwa manufaa ya chama na maisha ya baadae ya watanzania.
Viti maalum vya CHADEMA vinakwenda kwa watu maalum , Kanda maalum na familia maalum. Hivyo vilitengwa kwa watu wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha tu, na kwa familia za Slaa, Mbowe na Ndesamburo
How ironic it is to look for seniorship member in JF by posting hearsayings and feelings. I thought here we talk/writting only when we have fact and data! I am getting tired now with this forum!
mbowe hajaweka ndugu yeye hupitisha mahawaraViti maalum vya CHADEMA vinakwenda kwa watu maalum , Kanda maalum na familia maalum. Hivyo vilitengwa kwa watu wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha tu, na kwa familia za Slaa, Mbowe na Ndesamburo
Jamani hapa lazima tuwekane sawa na tuwe wawazi ili kukinusuru chama vinginevyo chadema itatufia mikononi kama ccm inavyoelekea kufa mikononi mwa rais kikwete. Mimi lazima niseme ukweli kwa manufaa ya chama atakayecheka acheke, atakayenuna anune, atakayelia alie ilimradi ujumbe umefika. Tukubali tusikubali, tutake tusitake uteuzi wa viti maalum kwa chadema ulikubwa na mizengwe fulani ambayo kwa namna moja au nyingine isipodhibitiwa siku zijazo chadema KITAKUFA! Nasema hivi kwa sababu kuna harufu ya undugunaization ambao umesababisha baadhi ya maeneo ambako chadema kimepata viti viwili au zaidi vya majimbo lakin yamekosa walau kiti 1 maalum. Kwa mfano, kulikua na sababu gani kwa mkoa wa singida kupata viti 2 na kilimanjaro kupata viti 3 hadi 4 maalum halafu mkoa kama shinyanga ambako chadema wamezoa majimbo 4 na kuibiwa la shy mjini na mbeya ambako wamezoa majimbo mawili kukosa walau kiti kimoja maalumu!? Pia kuna sababu gani zanzibar kupewa viti maalum 3 wakati chadema wanajua no matter what they do out there, the island will remain CUF-CCM dominated! Nadhan zanzibar kiti kimoja au 2 vingetosha walau kimoja kikaenda shinyanga! Katika mazingira kama haya kwa nini mtu asihoji wakati anaona jina la christina lissu (sijui uhusiano wake na tundu lissu) na la binti ndesa to mention but a few, yakiwa kwenye orodha!!? Viongozi wa chadema lazima walione hili na walifanyie kazi mapema wasituletee tabia za kubebana kama za ccm. Chadema ndo kwanza kinakua na hakijawa na wawakilishi wengi sana kwa hiyo basi wapinzani wake wanaangalia kila pungufu linalotokea na wanapata cha kusema na kuandika. Naomba tusiwape nafasi wapinzani wetu wasije sababisha chama chetu kife na wao ccm wakaendelea kutamba wakati wananchi wamesha wachoka!! TAKE CARE., LONG-LIVE CHADEMA..
nadhani viti maalum viendane na uwiano wa ushindi wa majimbo, mkoa ulioshinda majimbo mengi upewe viti vingi uliokosa usipewe
Siku hizi kila mtu anaijua sana CDM na utaratibu wao duuTabia hii ya upendeleo katika kuteua wabunge wa viti maalum(Wanawake) ilianza tangu mwaka 2005. Marehemu chacha wangwe alilipigia kelele lakini hakusikilizwa kwa sababu wachaga wameshika nafasi nyingi za uongozi wa kitaifa wa chama. Hata huyo Dr. Kitila alikuja na hiyo formula yake ili apendelee mkoa wake wa Singida(Kitila ni mzaliwa wa Singida). Tabia hii isipokomeshwa hakika CHADEMA itakosa uaminifu mbele ya umma wa watanzania.
Upendeleo unaofanywa katika CHADEMA si katika uteuzi wa viti vya wanawake tu, bali hata katika kugawa rasilimali za chama kwa maendeleo ya chama. Wagombea katika baadhi ya makoa husaidiwa fedha kwa ajili ya kampeni; wagombea katika mikoa mingine huachwa bila msaada wowote. CHADEMA ITABADILISHWA NA WANACHAMA NA SI VIONGOZI. WAJUMBE WA KAMATI KUU, BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU WASIKUBALI UPUUZI HUU. Si makosa ya kibinadamu yaliyotokea katika uteuzi wa wabunge wanawake bali ni makusudi mazima kwa ajili ya familia, ndugu na marafiki za viongozi wa juu.
WANACHAMA WA CHADEMA KAMWE MSIKUBALI CHAMA KIFE. CHUKUENI HATUA MADHUBUTI KUREKEBISHA MAMBO; WANACHAMA NDIO WENYE UAMUZI WA MWISHO KWA MUSTAKABALI WA CHAMA NA SIYO VIONGOZI. Shitambala na wenzako wa Mbeya unganeni na wanavchama wengine kurekebisha mambo ndani ya chama; Kamwe usikubali kutoka ndani ya chama, CDM ni mali yenu