Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,191
- 157,349
Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho:
Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu,
Je unachagua kwenda wapi?
MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote.
Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?