Hatimaye Chama cha Mapinduzi kimemaliza ule mchakato wake wa kuwapata wawakilishi wa "MKOA WA SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU" watakaowakilisha kama "WANEC" kwa chama cha Mapinduzi.

Uchaguzi huo wa kihistoria ulifanyika chini ya usimamizi wa Ndugu J.Silaa,Meya wa Manispaa ya Ilala

Uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulihusisha vijana wanafunzi toka vyuo vya Elimu ya Juu vya Tanzania Bara na Visiwani.Katika nafasi ya UNEC kulikuwa na Wagombea 13 ambapo wagombea watatu kura zao zilitosha na watakuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi wakiwakilisha Mkoa Wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu,waliopata nafasi hiyo ni:
(1)Joseph M. Chitinka
(2)John Lipes Kayombo.
(3)Tabia M. Mwita(Znz)

Nafasi ya Mwenyekiti imechukuliwa na
***Zainabu Abdalah Mussa
Makamu Mwenyekiti ni
**Hamid S.Muhina.
Itakumbukwa mara baada ya Serikali kupiga marufuku ushiriki wa siasa ktk maeneo ya vyuo vikuu,Chama cha Mapinduzi kilibuni "MKOA WA VYUO VYA ELIMU YA JUU" ili kuwaandaa vijana ktk ushiriki wa siasa na uongozi nje ya maeneo ya vyuo

Katika jumuiko hilo Mh.Rais Jakaya Kikwete ambaye ndie mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi amewaasa vijana kutokutumiwa kama ngazi na wanasiasa wenye uchu wa madaraka,na akasisitiza kuwa Taifa lililo na maono huwaandaa vijana kuja kushika nafasi ndani ya serikali na jamii na kwa Chama Cha Mapinduzi,UVCCM na Shirikisho la Vyuo Vikuu ndio mbadala.

Rais Kikwete alihitimisha kwa kusema "Mustakhabali wa Taifa letu,upo kwa Vijana walioandaliwa"