Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limemfungia Rais wa Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitano

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limemfungia Ahmad Ahmad kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka mitano.

Kamati ya Maadili ya FIFA imemkuta na hatia ya kufanya makosa yanayokiuka kanuni za uadilifu kwenye soka, kutoa zawadi ili achaguliwe, kufuja fedha.

Ahmad, ambaye amewahi kuwa Mtumishi wa Serikali ya Madagascar, ametozwa faini ya dola za kimarekani 220,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Milioni 510 za Kitanzania.

Kiongozi huyo wa juu wa Soka la Afrika alikamatwa na Mamlaka za Nchi ya Ufaransa Jijini Paris wakati wa maandalizi ya Michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake.

=======
GENEVA — African soccer confederation president Ahmad Ahmad was banned for five years by FIFA on Monday for financial misconduct.

The ban was announced during the Madagascan official’s campaign to be re-elected for four more years as the head of African soccer. His position also makes him a FIFA vice president.

The FIFA ethics committee found “Ahmad had breached his duty of loyalty, offered gifts and other benefits, mismanaged funds and abused his position as the CAF President.”

Ahmad, a former government official in Madagascar, was also fined 200,000 Swiss francs ($220,000).

Ahmad’s first four-year term was clouded with allegations of financial wrongdoing and misconduct at the Confederation of African Football headquarters in Cairo.

He was detained by French authorities in Paris on the eve of the Women’s World Cup for questioning about a CAF equipment deal with a company that appeared to have little connection with soccer.

“The investigation into Mr. Ahmad’s conduct in his position as CAF President during the period from 2017 to 2019 concerned various CAF-related governance issues, including the organization and financing of an Umrah pilgrimage to Mecca, his involvement in CAF’s dealings with the sports equipment company Tactical Steel and other activities,” FIFA said in a statement.

An audit of CAF finances pointed to irregularities under Ahmad’s leadership. The report was ordered by FIFA while it effectively took over running the organization for six months.

CAF appeared to pay about $100,000 for 18 people, including Ahmad and the heads of some of the continent’s 54 national member federations, to travel on the pilgrimage in Saudi Arabia.

The CAF election is scheduled for March 12 in Rabat, Morocco.

Ahmad had been supported by FIFA leaders in Zurich when he was elected in 2017, ousting FIFA senior vice president Issa Hayatou after 29 years.
 
Kwa nini waafrika tupo hivi?

Yaani akipata nafas flani ni wizi tuuu, rushwa kama yote..

Kupata nafasi ya uongozi tunaamini mpaka utoe hongo....

MUNGU wabariki wazungu
 
Hapo panaweza kuwa ni vita ya uongozi tu wale waliokuwepo awali wanaweza kuwa wanatafuta namna ya kurudi tena sasa wanarudije......
 
Kwa nini waafrika tupo hivi?

yaani akipata nafas flani ni wizi tuuu, rushwa kama yote..

kupata nafasi ya uongozi tunaamini mpaka utoe hongo....

MUNGU wabariki wazungu
Kuna kisa kimoja nilichosimuliwa huenda hakina ukweli lakini kina kitu cha kuzingatia.
Kuna mtanzania mmoja alikwenda kusoma uingereza, alipokuwa huko alipata rafiki wa kizungu waliyokuwa wakisoma wote, kwa kuwa alikuwa kichwa aliweza kurudi nyumbani na PhD. Baada ya miaka kupita swahiba wake wa Uingereza alimuandikia barua akimtaka aende kumtembelea, huyu ndugu yetu akamwambia kwamba hana fedha za ku-renew passport na hana hata suti ya kusafiria, wakati huo alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu. Yule mzungu akamtumia fedha kwa ajili ya maandalizi ya safari na hatimae akasafiri. Alipofika Uingereza alipokelewa na rafiki yake ambaye alikuwa akimiliki gari la kifahari na anaonyesha ni mtu mwenye heshima na wadhifa mkubwa nchini kwao, yule mzungu akampeleka kwake ili akapumzike ambapo alikuwa na nyumba kubwa ya kifahari. Siku ya pili alichukuliwa na yule mzungu akimtembeza sehemu mbalimbali, hasa katika miradi mikubwa iliyokuwa ikiendelea, na alikuwa akimwambia kwenye mradi huu nina 2%, mradi ule nina 3% na ule mradi mwingine nina 2.5% n.k. Yule m-bongo akashangaa mbona ana pasenti katika kila miradi ya serikali? Hapo ndipo alipowekwa kitako na kupewa mchongo mzima. Yule mzungu alimwambia baada ya kumaliza masomo yao ya PhD. yeye alijiingiza kwenye siasa, kwa kuwa alikuwa amesoma akafanya juu chini ili awe mbunge katika chama chenye nguvu aliposhinda na chama chao kushinda, akaomba awe waziri wa biashara na viwanda, hivyo katika kila mradi wa ujenzi wa viwanda au wabiashara alikuwa na pesenti fulani, ndiyo maana akawa mtu mwenye ukwasi mkubwa. Hivyo akamshauri rafiki yake aachane na kushika chaki badala yake aingie kwenye siasa. Basi ndugu yetu aliufanyia kazi ule ushauri na mwishowe aliukwaa uwaziri wa ujenzi na miundo mbinu, baada ya mwaka m-bongo alimualika yule sahiba wake mzungu, alipofika nchini alilakiwa na mwenyeji wake na kupakiwa katika gari la kifahari halafu akapelekwa nyumbani kwenye bonge la jumba la kifahari, yule mzungu alistaajabu sana katika kipindi kidogo jamaa amekuwa tajiri sana, akumuuliza amefanyaje mpaka amekuwa vile? akamwambia nitakujibu kesho, siku ya pili akapelekwa Mto Rufiji akaambiwa " unaona lile daraja pale?" yule mzungu akasema mbona silioni? yule muheshimwa akamwabia "Pale nimechukua 100%".
 
Siasa za mpira hizo. Ahmad aliwekwa madarakani kimtego ili issa hayatou atoke. Mda umefika wamemtoa waje waliolengwa .
 
Kuna ma Rais wa Football Federation kadhaa ambao ni vibaka wenzie. Lazima wamfuate.
 
Viongozi wengi wa mpira barani Africa ni wapigaji. They are there to satisfy their stomachs. Hili liwe funzo kwa viongozi wengine wa mashirikisho ya michezo hata hapa Bongo.
 
Bado rafiki zake.
 

Attachments

  • 2020_11_23_19.36.53.png
    2020_11_23_19.36.53.png
    325.8 KB · Views: 1
Hahaha! Rais wa FIFA ni swahiba mkubwa wa Dr. Patrice Motsepe nadhani tayari kamtengenezea Njia ya kupata Urais wa CAF
 
Back
Top Bottom