Shirika la Posta Tanzania kununua ndege yake

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,948
Shirika la Posta Nchini lipo katika mchakato wa kununua ndege kwa ajili ya kusambaza vifurushi na huduma nyingine ili kurahisisha huduma kwa wateja wao.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Hassan Mwang’ombe, alisema ununuzi wa ndege hiyo unatokana na mafanikio yaliyopatikana tangu bodi iteuliwe mwaka 2016.

Alisema mchakato wa ukamilishwaji wa ndege hiyo unaendelea na kwamba utawapunguzia muda wateja kupata mizigo yao pindi inapotumwa kupitia shirika hilo.

Katika hatua nyingine, alisema kutokana na kukua kwa teknolojia, shirika hilo limeanzisha duka la mtandaoni, ambalo tayari lina wateja kutoka duniani kote.

Alisema tayari wameunganisha ofisi 125 za posta kwenye mfumo wa kutolea huduma kielektroniki unaojulikana kama Postglobal netsmart na mpango wa kuunganisha nyingine 27 utakamilika mwishoni mwa Septemba, mwaka huu.

“Maboresho na mifumo hiyo ya mawasiliano inalenga kuboresha huduma ya biashara mtandao nchini na nje ya nchi na kuwafanya wateja wa shirika hilo kufurahia huduma zetu’’.

Aliongeza kuwa, wamefanikiwa kuboresha huduma za kisasa katika ukanda wa Afrika kwenye kufikisha huduma kwa wateja, hasa maeneo korofi kwa kutumia ndege zisizo na dereva zijulikanazo kama ‘drones’.

Naye Mwenyekiti wa bodi wa Shirika hilo, Dk. Haroun Kondo, alisema tangu bodi yake iteuliwe wameweza kuzalisha faida.

Dk. Kondo alisema kutokana na hilo, kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 walitoa gawio la Sh milioni 250 kwa Serikali, huku mwaka huo wa fedha 2017/2018 wanatarajia kutoa gawio la zaidi Sh bilioni moja.

Dk. Kondo alisema hilo limetokana na jitihada za Bodi na Menejimenti ya Shirika katika kulifanya lijiendeshe kwa faida tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, ambapo lilikuwa likizalisha hasara tu.

Amesema lengo lao kuanzia sasa ni kuchangia pato la taifa kwa kutoka gawio la kuanzia Sh bilioni na kuendelea, kwa madai kuwa shirika lina uwezo huo kupitia rasilimali ilizo nazo, ikiwamo majengo na viwanja wanavyovimiliki.

Alisema katika mafanikio hayo alipitia changamoto mbalimbali, kama Mwenyekiti, ikiwamo kulalamikiwa kuwa mbabe kwa kuwaondoa baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kulisababishia shirika hasara na kufikishwa katika vyombo mbalimbali, lakini hakujali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Easier wspigaji tu... Nchi hii tuna kuwa na mashaka na watendaji wa umma kila uchwao...
 
Ndege inayoendeshwa na rubani au zile zisizotumia rubani "Drone"?
 
Isije ikawa wananunua ndege ili kurahisisha huduma kwa wateja, na kumfurahisha mkulu..... wakati huo ndege hiyo isiwe kwaajili ya kuongeza mapato na faida kwa muda mfupi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angalia nchi na mashirika ya wenzetu....
Kwa watu million 50..tukiwa hata na boeng moja ya postal service haina tatizo
IMG_20180903_111146.jpg
IMG_20180903_111126.jpg
IMG_20180903_111107.jpg
Screenshot_20180903-111026.jpg
Screenshot_20180903-110944.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanunue helkopta siyo ndege. Barua zinachelewa sana vijijini ambako ndege haiwezi kufika.
Kuna anayetuma barua binafsi katika ulimwengu huu wa simu ? Labda za kiofisi na vivurushi.
 
Wangeingia ubia na shirika la atcl, si nayo inakuwa na kufika mikoa yote. Kununua ndege ni gharama na uendeshaji wake ni gharama zaidi kuliko kulipia gharama za kusafirisha kutumia atcl, ukizingatia haiko kiushindani, na inapata ruzuku ya serikali, hivyo bei zao ziko chini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja niongeze bidii ya kuandika barua maana kwa sasa kuna uhakika wa kufika mapema tu.
 
GO GO GO TPC

ingekua ni shirika la posta la nchi fulani watanzania wangsifia kweli ila kwakua ni tanzania wapinzani lazima wabeze na kupinga vikali

TABU ZIKO PALEPALE HAZIEPUKIKI
 
nI MCHAKATO WA KUPIGA HELA TU HAPO...MTAWEZA KUPAMBANA NA DHL? au FedX? nyie endeleeni kuwa SHIRIKA LA POSTA.
 
Back
Top Bottom