Shirika la ndege la Etihad limezindua programu ya simu za mkononi kwa ajili ya wateja kupata taswira

John Mwelele

Member
Apr 16, 2016
18
17
Etihad Airways Mobile App.jpg

Etihad Airways ambalo ni shirika la ndege la taifa la UAE, limezindua programu ya simu za iPhone ambayo inasaidia wageni kupangilia na kuratibu safari zao kwa urahisi zaidi kadri ambavyo shirika linavyoendelea kuendana na teknolojia ya kiuvumbuzi ya kupata taswira ya safari.


Wateja wa Shirika la ndege la Etihad watafurahia punguzo la asilimia 10 ya gharama za safari za ndege na wanachama wa programu ya uaminifu ya shirika la ndege la Etihad, watapokea ziada ya maili 250 kwa kila tiketi watakayonunua kupitia programu ya simu kabla ya tarehe 30 Mei 2016. Wale watakao hudhuria katika kituo cha shirika la ndege la Etihad (ME 2310) katika soko la safari la Arabia Dubai kuanzia tarehe 25 – 28 Aprili 2016 wataweza kujaribu vipengele mbalimbali vya programu hiyo na utendaji wake wa kazi.


Programu ya simu ya Shirika la Ndege la Etihad ni rahisi na inafurahisha kutumia, inakupa uwezo wa kuratibu safari zako kikamilifu kwa kutumia mbinu za uvumbuzi wa kisasa zaidi katika teknolojia ya simu za mikononi. Wageni wanaweza kupangilia safari zao katika programu hiyo ikijumuisha kukata tiketi, kufuatiliana na kuangalia hali halisi ya safari.


Shirika hili la ndege vile vile lina ubia na mamlaka ya viwanja vya ndege Abu Dhabi, kuwasaidia wageni kutembelea sehemu mbalimbali za mamlaka ya viwanja vya ndege Abu Dhabi kwa kutumia ramani za ndani ya nyumba – ya kwanza katika mashariki ya kati nzima. Programu hii ya simu vile vile inajumuisha mwonekano wa kiwango cha juu, ramani ya viti vya kukaa iliyoboreshwa, inawapa wasafiri maelezo ya kutosha ya mpangilio wa chumba cha ndege ikiwemo kiti chao walichochagua.




Afisa biashara Mkuu wa shirika la ndege la Etihad bwana Peter Baumgartner, amesema: “shirika la ndege la Etihadi limejidhatiti kutoa huduma za kiwango cha juu kwa kila mgeni atakaye wasiliana nao, iwe ana kwa ana au kwa njia ya mifumo ya kidigitali. Tunafanya bidii ya kutoa masuluhisho ya kiuvumbuzi ambayo yanahakikisha wageni wetu wanafurahia huduma za kiwango cha kimataifa zisizo na kasoro. Tuna uhakikia kuwa wageni wetu watafurahishwa na kasi ya programu hii ya simu, urahisi wake wa kutumia na utendaji wake mkubwa. Wasafiri wa mara kwa mara wataweza pia kufurahia uwezo wa kupangilia safari kwa haraka – zote zinazopatikana katika programu moja ya simu.”


Programu ya simu ya shirika la ndege la Etihad inawawezesha wasafiri kufuatilia safari zao kwa kutumia simu zao za mkononi kwa kuskani kurasa yao ya pasi zao za kusafiria. Pia wageni wanaweza kulipia tiketi kwa kuskani kadi zao za manunuzi, jambo hili linaondoa usumbufu wa kutakiwa kuweka maelezo ya msafiri na taarifa za malipo kwa mkono.


Utaratibu rahisi wa kukata tiketi una ruhusu wageni kulinganisha machaguo mbalimbali ya nauli na kuboresha machaguo yao. Katika kipengele cha ‘MyTrips’ wageni wanaweza kuangalia safari zao zilizopita na zile zijazo, ambazo zimeunganishwa moja kwa moja na akaunti zao za programu za wageni za Etihad. Wanaoingia katika ndege wanaweza kuonekana kupitia katika programu ya simu au kuhamishiwa moja kwa moja kwenye iOS Wallet.


Programu hii inatoa kipimo cha ‘muda uliobakia kabla ya ndege kuondoka’ kipengele hiki kinawasaidia wageni kufika katika lango la kuondokea katika muda wa kutosha. Taarifa za papo kwa papo za hali ya safari inatolewa kuwawezesha wanafamilia na marafiki za abiria kufuatilia safari yao.


Programu ya simu ni moja ya mbinu za kiuvumbuzi zinazofanyika katika shirika zima la ndege la Etihad kama sehemu ya mkakati wake wa kidigitali wa uvumbuzi. Mkakati huu wa kiteknolojia unahakikisha kuwa shirika la ndege la Etihad na mashirika mabia ya ndege yanatumia teknolojia ya kiwango cha juu ulimwenguni kuwasaidia kutoa huduma na bidhaa ambazo zinaongeza uzoefu wa wageni na kuhakikisha matarajio ya abiria wa anga yanafikiwa.


Afisa habari Mkuu, Kundi la wasafirishaji wa Anga la Etihad, Bwana Robert Webb, Amesema: “programu ya simu inaonesha hatua kubwa mbele katika mkakati wa uvumbuzi wa wageni wa kidigitali. Kwa kupitia teknolojia tunatengeneza huduma na bidhaa binafsi zaidi za kidigitali kwaajili ya kuwafaidisha wageni wetu. Huu ni mwanzo tu kadri tunavyoendelea kuwapa wageni wetu uwezo mkubwa na udhibiti na urahisi katika ukataji wa tiketi na uzoefu wa safari ikijumuisha jinsi wanavyochagua kuongea na sisi.”


Programu mpya ya simu za iPhone ya shirika la ndege la Etihad sasa inapatikana kwaajili ya kuidownload katika simu yako kupitia App store.



-Mwisho-

Kuhusu Shirika la ndege la Etihad

Shirika la ndege la Etihad lilianza shughuli zake mwaka 2003, na mwaka 2015 lilibeba wasafiri wapatao million 17.4. Kutoka katika makao makuu yake ya Abu Dhabi, Shirika la ndege la Etihad litafanya safari zake kwenda au limetangaza mipango yake ya kuhudumia wasafiri na mizigo kwenda katika vituo 116 katika Mashariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Marekani. Shirika hili la ndege lina ndege 120 ambazo ni Airbus na Boeing, pamoja na ndege 204 zilizoko katika hali nzuri zikiwemo Boeing 787 zipatazo 71, Boeing 777Xs zipatazo 25, Airbus A350 zipatazo 62 na Airbus A380.

Shirika la ndege la Etihad lina uwekezaji sawa katika shirika la ndege la berlin, Shirika la ndege la Serbia, katika shirika la ndege la Seychelles, Alitalia, Shirika la ndege la Jet, Virgin Australia na shirika la ndege la Darwin lenye kakao yake makuu Uswiss, inayofanya biashara zake kama Etihad Regional. Shirika la ndege la Etihad, pamoja na Shirika la ndege la Berlin, Shirika la ndege la Serbia, Shirika la ndege la Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Shirika la ndege la Jet na NIKI, Vile vile shiriki katika ushirika wa shirika la ndege la Etihad ambayo inaleta pamoja wasafirishaji wenza kuwapa wateja nafasi zaidi katika kuboresha mtandao na ratiba na kukuza faida za kuruka mara kwa mara. Kwa tarifa zaidi, tafadhali tembelea: www.etihad.com


Kwa mawasiliano zaidi:

Afisa wa Vyombo vya habari wa Shirika la ndege la Etihad

Tel: +971 50 818 9596

Barua pepe:dutymediaofficer@etihad.ae
 
Back
Top Bottom